Ni kipi sahihi zaidi kati ya kumwambia mtu sikutaki au kumzungusha?

Thad

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
13,363
31,504
Amani iwe kwenu wakuu,

Hivi ni kipi kinaumiza zaidi katika mapenzi, kuambiwa sikutaki au kuzungushwa sana na kupewa vijisababu visivyokuwa na msingi?

Tunajua kuwa mapenzi huzaliwa, hukua, hufa na mara chache mapenzi huweza kufufuka. Katika hatua zote hizo si ajabu kukumbana na kauli ya "NIMESEMA SIKUTAKI /SIKUPENDI" au usitamkiwe maneno kama hayo bali uzungushwe tu, mathalani utapiga simu mtu hapokei, utatuma sms hajibu, ukimwambia nakuja anakujibu usije sipo nyumbani lakini ukienda utamkuta yupo tu n.k

Swali langu kwenu ni je kipi kinaumiza zaidi kwa upande unaotendewa, kuambiwa kinagaubaga kuwa sikupendi au kuzungushwa? Na kwa upande unaotenda kipi ni rahisi zaidi kusema sikupendi au kumzungusha mtu?
 
Machozi yana nilenga umenigusa
Pole sana kiongozi, halikuwa lengo langu kukutoa machozi. Ila haya tunakumbana nayo sana.

Vipi umeambiwa kuwa hupendwi au umezungushwa?
 
Back
Top Bottom