Ni kipi kipindi bora cha asubuhi kwenye radio?

Clouds FM ni radio ambayo unaweza sikiliza siku nzima ina vipind bomba.

Kidogo siku hz baada ya kuondoka b12,xxl nakuwa sielew kwasasa,b12 alkuwa anajua kuwaongoza vizur na mahojiano na wasanii yalkuwa poa sana.

Ukisikiliza clouds kuanzia asubuh mpaka jion,hakuna haja ya kununua gazeti,kuangalia taarfa ya habari,hata hakuna haja ya kutembelea mitandao ya kijamii.
Leo tena dahuu yule simwelewagi kabisa angetoka angekuja demu mwingine hata dina kipindi kingekuwa kitamu sana kwa sasa kipo vagaravagara, pb kipo poa na xxl kama kawaida bdozen hajapunguza chochote kuondoka kwake
 
Well said mkuu... Vipi kipindi cha Leo tena? Huwa wananivutia sanaa, hasa kipindi akiwepo yule Musa kama sikosei kwenye ile timu yao.
Kipindi hicho kimekuwa kibaya tu zaidi ya heka heka na zilizokiki tu ndivyo navyosikilizaga labda wamtoe dahuu wamrudishe dina
 
Hakuna kitu kama hicho kwa sababu zifuatazo:-
1: Ifahamike kwamba kuna tofauti kubwa programe za asubuhi na jioni, MF kipindi cha asbh cha Radio 1 kilifaa kuwa jioni kwani wao wanaongelea mada zaidi na ndiyo maana wachangiaji wa simu ni wengi kwani jioni ni muda ambao watu wametoka kazini, wamepumzika nk. Tofauti na asubuhi ambapo Mara nyingi ni muda ambao hakuna mtu mwenye muda wa kupiga simu, ila ni muda ambao mtu anahitaji kupata habari na mambo yaliyojiri kwa wakati huo (Current story) na ndicho wanakifanya PB (Hongera kwao kwa ubunifu huo?

2: Utangazaji wa sasa ni modern si kama zamani, yaani media zinatakiwa kuwa na watu wenye ubunifu na zaidi ufahamu wa kuchambua mambo nyeti kulingana na nyakati, , , , kama utakumbuka ndani ya PB zamani kulikuwa na Segment inaitwa Jicho la Ng'ombe ilikuwa inaonesha ukosowaji wa moja kwa moja kwa njia ya mafumbo kwa serikali ila waliishtia na kuifuta hiyo segment, baadaye wakaleta kitu kinaitwa Kuperuzi na Kudadisi(Kwa sasa ni Kudonoa na Kudadisi) baada ya serikali kukataza media kusoma story kwenye magazeti na badala yake ikawa ni Headlines tu, wakamleta Sasali kwa kazi hiyo na bilashaka anaifanya vema kuliko PJ alivokuwa akifanya hapo kabla.

3: Kwa idadi ya watu kwenye vipindi hasa asbh na jioni karibu media zote kwa sasa ziko sawa kwani ni ngumu kipindi cha Massa 3/4 afanye mtu mmoja au wawili, ukweli ni kwamba Audience wanahitaji ladha tofauti masikioni, , , , hapo media zote ziko sawa.

4; Mwisho ni kwamba utangazaji siyo kuongea tu kwenye Mic, Bali uwezo wa kufikiri, kuchambua, ku- challenge nk, , , Nisem Clouds wamejitahidi kwa hilo ingawa Radio 1, E FM na Wasafi wanawatangazi wazuri lkn huwezi walinganisha uwezo wao na Kipanya, Cza, au Sasali, , , ,

Kama huyu Kitenge wakati yupo IPP alikuwa na akili lkn tangu aende Wasafi anaropoka ropoka tu studio na mwenzake Zembwela utadhani wanapita mtaroni wakati naye akiwa East Africa alikuwa timamu, Na huyu Mwaipaya sijui nani ndo hata hana kitu wao asbh asbh simu na mada za Ndoa kila siku kama vile wahubiri wakati kuna mambo nyeti ya kuzungumzia.

Sasa hawa niliowataja utaweza kulinhanisha uwezo wao na Kipanya, Cza au Sasali?
Yaani fikiria Kitenge, Zembela au Mwaipaya afanye Interview na Prof Lipumba, Zitto, Lissu, Majaliwa (wataishia kucheka tu)

Kwangu PB ni Bora zaidi!
hakuna kitu kama hichoo mkuu na maelezoo yako marefu ambayo sijaona point hapoo...sijui watangazaji sijui kipanyaa.... sijui ubunifuu
naona unaongelea ushabiki tu mandazi
siku tafuta bbc ithaa ya kingereza inapofika asubuhi kule kwao program za vipindi vyao vinakuajee.....
 
Leo tena dahuu yule simwelewagi kabisa angetoka angekuja demu mwingine hata dina kipindi kingekuwa kitamu sana kwa sasa kipo vagaravagara, pb kipo poa na xxl kama kawaida bdozen hajapunguza chochote kuondoka kwake
Ruge alkuwa mtu mbaya sana,sijui kwann almfanyia vile dina,alivyoenda kujfungua akaweka mtu mwingine na ndo ikawa mazima
 
Tatizo GoodMorning utani mwingi na kuchekacheka sana. Inatakiwa wajipange. Angalau David Rwenyugira anajitahidi

Kipind kilikua magic fm orest kawau, marry, jamaa mwingine nnimemsahau na mzee mmoja walikua wanamuiita google dah back days iyo 2014 kushuka chin kabla haijawa ccm
 
Leo nimesikiliza kipindi cha Good morning cha wasafi fm hadi nikashangaa..wale jamaa wanapiga kelele kama wako kijiweni..kila mtu anataka kuongea na kila mtu anatamani asikike kiasi kwamba hata kama mwingine anaongea huwa anatamani aropoke chochote..Mzee zembwela ndo usiseme mikelele kama yote..Mara waanze kuimbishana nyimbo kama watoto kwakweli inafikirisha..Ukiacha matangazo ambayo yanachukua karibu 50% ya kipindi, hakuna content ya maana ambayo unaweza kuipata kutoka kwa wale jamaa..Kila mtu anajifanya mjuaji na masikhara mengi yaliyopitiliza

cc sinza pazuri Slowly najua nyinyi mnaweza mkawafikishia huu ujumbe..waambieni kipindi ni kizuri ila basi wapunguze utoto utoto na sauti zisizo na mpangilio.​
 
Back
Top Bottom