Ni kipi kilifanya Juma Nature kuwa spesho kuliko wasanii wengine wa kipindi chake?

Nature ana mistari adimu pia uwezo wake wa ku ghani mashairi, lazma ukimsikiliza utacheka tu maana anaimba kihuni huni na ana represent maisha ya uswahilini typical ambayo ndio yalikuwa maisha common kwa watu wengi kitambo kile.

Nadhani majani alikuwa anainjoy ile style ya rap katuni na wepesi wa Nature kuflow ukimpa beat. Ule uswahili uswahili wa nature na uhuni uhuni ile feeling itakuwa ilikuwa inamvunja mbavu sana bila shaka tofauti na wale wasanii waliokuwa wana rep ushua ushua ambayo ndo maisha ya P.Funk toka utotoni.
Kingine ni kile kisauti chake cha ndani anachokitumiaga kwenye koras. Wimbo Kama Ya Leo Kali, Mzee wa Busara, Nampenda Nani, Mapacha wa Soggy etc.
 
Back
Top Bottom