screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,792
- 15,693
Miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni kuliibuka vichwa hatari sana kwenye muziki wa Rap/Hiphop, hiki binafsi nakiona kama kizazi cha dhahabu kama ilivyokuwa timu ya Barcelona iliyomtetemesha SAF pale Wembley kwenye fainali za UEFA mwaka 2011.
Tukiachana na Records label nyingine, Ulikuwa ukienda tu pale Bongo Records kwa Majani utakutana na vichwa vikali kama Prof Jay, SoloThang, JayMo, Afande Sele, Ngwea, na wengine wengi, lakini pamoja na vichwa hivyo Sir Nature Kiroboto alikuwa treated kama mtoto mteule/mtoto mpendwa pale BongoRecords ama kwa jina jingine tunaweza muita 'The Special One', hata wasanii wenzake walilijua hilo kiasi cha kufikia kupeana maneno ya chinichini kwamba Majani anampendelea Nature, yaani Sir Nature akitaka kurekodi ngoma muda wowote ilikuwa ruksa, huku kina Fid Q wakipigwa danadana kwa zaidi ya miaka miwili.
Nadhani hii Majani hakuifanya kwa sababu ya urafiki wake na Nature tu, ni kwamba yeye kama mfanyabiashara alimuona ni mtu mwenye potential kubwa that's why akaamua kuinvest zaidi kwake, na kwakweli alifanikiwa maana show zote zilizowakutanisha wasanii wengi nilizofanikiwa kuzihudhuria enzi za 'uvulana' wangu kukiwepo jina la Juma Nature basi jua huyo ndie atakayefunga show, pamoja na vichwa kama Prof Jay kuwa na Hits kali, lakini wakikutana na Sir Nature kwenye show walikuwa wanasalimu amri tu hamna namna.
Je, ni kipi unadhani kilimfanya Sir Nature kuwa 'The Special One'? Ni zile Chorus zake kali? Flow yake? Sauti yake? Uswahili wake? Beat za Majani? Mashairi yake? Ila hapo kwenye lyrics namfananisha na mswahili mwenzake Inspector Haroun, siwezi muweka kwenye kundi la hao wakali hapo juu...