Ni kipi kilicholaaniwa kati ya TANZANIA au WATANZANIA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kipi kilicholaaniwa kati ya TANZANIA au WATANZANIA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Apr 20, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kuna laana katika nchi hii. Tuchunguze ili tujue tu kuwa, laana hii tumelaaniwa wananchi au nchi. Hata hawa wabunge wa CCM wanaopiga makelele kupinga ubadhirifu wa mali ya uma ni wanafiki pia. Leo watasimama na kutoa mapovu mdomoni. Kesho wakipewa wao uwaziri wanajisahau na kuwa sawa na hawa wanaowasema. Hawa ndio wanaosababisha bunge kuwa na meno butu. Leo wanapinga ubadhirifu, kesho kwenye kupitisha sheria inayoupa mwanya ubadhirifu wapinzani wakipinga, wao utawasikia wakisema; Ndiyooooo! Kama ni laana, tumuombe Mungu atuepushe nayo.
   
Loading...