Ni kiongozi gani wa kisiasa ana hotuba kali za kumbadilisha mtu?

12STONE

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
1,183
398
Kati ya mwaka 2008 hadi 2010 niliwahi kumsikia Mh.Mbowe akihutubia Uwanja wa Mkendo Manispaa ya Musoma.

Alizungumzia mambo mengi ila alipoanza kulizungumzia suala Ufisadi wa EPA ndani ya BOT.

Nakumbuka siku ile watu walikuwa wengi sana walihudhuria wakiwemo wanachama na wapambe wa CHADEMA,CCM,CUF na wengi wasiokuwa wanachama wa chama chochote kile.

Kijana aliyeonekana kavalia Tisheti ya njano ikiwa inaashiria yeye ni mwana ccm aliyekunywa mpaka maji ya Bendera kama kiapo cha kutokukiuka masharti ya chama hicho.(kama wasemavyo watu)

Kijana huyo alionekana kumfuatilia Mbowe kwa makini wakati akiongea,Kijana aliyeaminiwa na ccm kuwa kamwe haitatokea akikane na kukiacha CHAMA CHA MAPINDUZI,ailiposikia fedha zile zikipangwa moja moja kutokea TZ zitafika Cairo Misri alipiga Yowe la nguvu UUWIIIII!!! HUKU AKICHANA ILE TISHITI ALIYOKUWA AMEIVAA MBELE YA HADHARA YOTE AKABAKIA KIFUA WAZI.

Kwa tukio hilo kutokea yamkini ilituthibitishia kwamba Hotuba ya Mbowe ilibeba ujumbe mzito mpaka kijana akaona haina maana ya kuendelea kuvaa Tisheti ya CCM huku akizidi kuwa masikini na Wakati huo huo Wengine wakiyala mema ya Nchi kwa kuifisidi Nchi kaa Mchwa anayatafuna Nyasi.

Wewe unaonaje? Mh. Mbowe aweza kuwa kiongozi wa Kisiasa mwenye Hotuba kali kiasi cha kuwabadili wengi na kuacha vyama vyao na kujiunga na CHADEMA?

Nawasilisha kwenu Wanajamii.
 
Binafsi namkubali sana Kamanda Mbowe kwa hotuba zake! Nilianza kufuatilia umakini wa hotuba zake wakati wa harambee ya chama katika uchaguzi mdogo Arumeru.

Nimekuja kuthibitisha juzj pale Bwiru Mwz aliposema atatoa hotuba iliyokita katlka historia ya chama. Watu wengi wwaliguswa na wengine kutoa machozi. Jamaa anajua kuteka jukwaa kwa maneno ya kugusa na wakati mwingine ya kuchangamsha hasa akitumia lugha za vijana!
 
mh.mbowe hana mpinzani katika jukwaa la kisiasa katika utoaji wa hotuba na maccm wanamwoga zaidi ya kuku anavyo ogopa mwewe dhidi ya vifaranga wake.
 
Nilidhani unaacha Uhuru kwa waendeleza uzi watoe maoni yao........kumbe una yako....napita kuepusha kuchafua hali ya hewa.
 
Kati ya mwaka 2008 hadi 2010 niliwahi kumsikia Mh.Mbowe akihutubia Uwanja wa Mkendo Manispaa ya Musoma.

Alizungumzia mambo mengi ila alipoanza kulizungumzia suala Ufisadi wa EPA ndani ya BOT.

Nakumbuka siku ile watu walikuwa wengi sana walihudhuria wakiwemo wanachama na wapambe wa CHADEMA,CCM,CUF na wengi wasiokuwa wanachama wa chama chochote kile.

Kijana aliyeonekana kavalia Tisheti ya njano ikiwa inaashiria yeye ni mwana ccm aliyekunywa mpaka maji ya Bendera kama kiapo cha kutokukiuka masharti ya chama hicho.(kama wasemavyo watu)

Kijana huyo alionekana kumfuatilia Mbowe kwa makini wakati akiongea,Kijana aliyeaminiwa na ccm kuwa kamwe haitatokea akikane na kukiacha CHAMA CHA MAPINDUZI,ailiposikia fedha zile zikipangwa moja moja kutokea TZ zitafika Cairo Misri alipiga Yowe la nguvu UUWIIIII!!! HUKU AKICHANA ILE TISHITI ALIYOKUWA AMEIVAA MBELE YA HADHARA YOTE AKABAKIA KIFUA WAZI.

Kwa tukio hilo kutokea yamkini ilituthibitishia kwamba Hotuba ya Mbowe ilibeba ujumbe mzito mpaka kijana akaona haina maana ya kuendelea kuvaa Tisheti ya CCM huku akizidi kuwa masikini na Wakati huo huo Wengine wakiyala mema ya Nchi kwa kuifisidi Nchi kaa Mchwa anayatafuna Nyasi.

Wewe unaonaje? Mh. Mbowe aweza kuwa kiongozi wa Kisiasa mwenye Hotuba kali kiasi cha kuwabadili wengi na kuacha vyama vyao na kujiunga na CHADEMA?

Nawasilisha kwenu Wanajamii.

Mkuu nnaomba kuwa tofauti kidogo sababu mimi nnaamini katika falsafa hii "UONGOZI IMARA SIO UTAALAMU WA KUTOA HOTUBA AMA KUPENDWA ,BALI UONGOZI NI KUTOA MATOKEO YALIYOTARAJIWA".kama wapo viongozi waliosimama ktk hili nitawakubali.
 
Binafsi namkubali sana Kamanda Mbowe kwa hotuba zake! Nilianza kufuatilia umakini wa hotuba zake wakati wa harambee ya chama katika uchaguzi mdogo Arumeru.

Nimekuja kuthibitisha juzj pale Bwiru Mwz aliposema atatoa hotuba iliyokita katlka historia ya chama. Watu wengi wwaliguswa na wengine kutoa machozi. Jamaa anajua kuteka jukwaa kwa maneno ya kugusa na wakati mwingine ya kuchangamsha hasa akitumia lugha za vijana!
Mi nkidhani unamaanisha mwanasiasa kumbe unamaana ya mwanacdm? Hapo tena unapiga propaganda za cdm njomba. Huo ukali wa hotuba kumbe ni sawa na ukweli ati? Au unamaanisha hotuma yenye fujo au ya magomvi? Kwa taarifa yako kila mtanzania ni mwanasiasa mzuri akipewa nafasi utamwona tu.
 
ingawa umeshakuja na maoni yako lakini hotuba za mbowe ni za ukweli,zinavuta hisia za kiharakati za ukombizi,lema anafatia.
 
Mbowe ni kiboko anaijua historia ya hii nchi na chama chake kweli na hamungunyagi maneno huyu jamaa,na anapozungumza huwa anaangalia anaongea na watu wa rika gani walio wengi ili ajue jinsi ya kufunguka ati
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom