wwww
JF-Expert Member
- Mar 20, 2012
- 350
- 252
Ndugu wanajamvi naomba tuweke huu uzi hapa kwenye kibandiko ili ukisubiria kuona kiongozi atakaye kuwa wa kwanza kubadili Ibara ya 40 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuondoa ukomo wa vipindi vya kutawala.
Nawabadikia Ibara yenyewe hapa chini ili muweze kuisoma.
Haki ya kuchaguliwa
tena Sheria ya 1984
Na.15 ib.9 Sheria
Na.34 ya 1994 ib.9 40.-
(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais
anaweza kuchaguliwa tena kushika kiti hicho.
(2) Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais.
(3) Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar hatapoteza sifa za kuweza kuchaguliwa kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano kwa sababu tu kwamba aliwahi kushika madaraka ya Rais Zanzibar.
(4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa
kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini
kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi
ya Rais mara moja tu.
Tujadili kistaarabu.