Ni kinyume kwa wabunge kutoka Zanzibar kuchangia mambo yasiyo ya muungano. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kinyume kwa wabunge kutoka Zanzibar kuchangia mambo yasiyo ya muungano.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Feb 14, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hushughulika na masuala ya aina mbili; kwanza, yale masuala ya muungano kama yanavyopitishwa mara kwa mara kwa mujibu ya sheria. Na pili masuala yanayohusu Tanzania bara pekee. Haya yanajumuisha masuala yote yasiyo ya muungano. Katika kuwa na usawa napendekeza wabunge kutoka Zanzibar wasiwe wanaruhusiwa kuchangia au kupiga kura kwa masuala yanayohusu Tanzania bara pekee. Nawasilisha
   
 2. T

  Tata JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Orodhesha masuala ya Tanganyika ambayo unadhani wazanzibari hawatakiwi kuchangia wakati wa mijadala. Na je kama masuala hayo yana athari kwa maslahi ya Zanzibar ndani ya muungano bado wanatakiwa wakae kimya tu?
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndiyo kama masuala hayo siyo ya muungano wanapashwa wakae kimya hata kama yana maslahi kwa Zanzibar. Hii inatokana na ukweli kwamba hata baadhi ya masuala yanayojadiliwa katika baraza la wawakilishi huwa yanagusa maslahi ya Taznania bara lakini huku hatuna fursa ya kuchangia.
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Daini Tanganyika yenu kwnza halafu mje na nyimbo kama hizo!
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  :roll: Tanganyika ikija CCM inaweza kufa.
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Wewe pia umekuwa kama kasuku hapo red weka Tanganyika, sote tungekuwa tunaitaja Tanganyika kila leo basi watawala wetu pia wangejua kuwa kasumba waliyotulisha haifanyi kazi....sote tuitaje na tudai jina rasmi litumike Tanganyika badala ya Tanzania bara.
  Tanganyika, Tanganyika,Tanganyika.Tanganyika.........
   
 7. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanganyika,Tanganyika, Tanganyika Tanganyika, oyee
   
 8. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa kama mambo si ya muungano kwa nini yajadiliwe bungeni ? na lile ni bunge la mungano na yatakayojadiliwa mule ni masuala ya muungano tu kama munataka mambo yasiyo ya muungano yasijadiliwe bungeni basi yapelekeni Diamond Jubilee mukajadili maana hayawahusu wazanzibari lakini kama yatajadiliwa bungeni yatawahusu pia
   
 9. T

  Tom JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2011
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umesema kweli waende Diamond Jubilee, wanaCCM wa Tanganyika wapo radhi kua na huu muungano ili mradi kulinda mshikamano wa chama na ufisadi.
   
 10. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  umejibu vyema sana. tatizo liko kwenye muundo wenyewe na sio uchangiaji ndani ya bunge. so fursa hii ya kuandikwa upya katiba itumiwe vizuri kupata muungano unaokidhi kiu ya wakati huu tulionao
   
 11. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwa mawazo yangu haifai kwa wabunge wa zanzibar kuchangia hoja zinazohusu Tanganyika kwa sababu ushahidi upo kwamba wengi wao hawaitakii mema Tanganyika. Anayeuliza masuala ya Tanganyika ni yapi ni mjinga.
   
Loading...