Ni kina nani hawa wanaotishia usalama wa Rais wetu kiasi hiki?

Anayeandika andiko refuu kama hiki kuongelea hoja legevu yeye atakuwa nani?
Yaani unaoga mtoni,kuchaa anatokea na kubeba nguo zako na kukimbia,wewe unatoka mtoni kama ulivyo na kuanza kumfukuza,hivi hapo kichaa hasa ni yupi?
Augustino Chiwinga
0659438889.

Sasa hivi wapinzani baada ya kuishiwa hoja wamehamia katika kujadili aina ya ulinzi alionao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Daktari John Pombe Magufuli.

Huku ni kukosa hoja kufikia kutaka eti apunguziwe ulinzi na wengine wakiuliza maswali ya kipuuzi kama vile gari la machumachuma (Convyoy Protection Jammer) katika msafara wa Rais lina kazi gani?

Jamani tuelewane Rais ni kiongozi mkuu wa nchi hivyo anastahili ulinzi kwa kadri ya vyombo ya ulinzi na usalama vitakavyoona inafaa.

Tukumbuke usalama wa viongozi ni jambo nyeti sana hivyo tuwaachie wanaohusika kushughulika nao.
Hoja wanayoisema eti kwamba Rais Magufuli ulinzi wake ni mkali kuliko marais wa awamu zilizopita, na kwamba ulinzi wake unajenga hofu kwa wananchi na Bajeti kubwa.

Jambo hilo sio kweli kwa raia mwema hawezi kuingiwa na hofu hata kama Rais atalindwa na vifaru, bali hofu huwapata wale wenye nia ovu na kuhusu Bajeti hiyo pia sio kweli kwa sababu Bajeti hupitishwa Bungeni baada ya uchambuzi na majadiliano ya kina hivyo Wabunge waliopitisha wameipitisha kulingana na mahitaji ya sasa na maslahi ya nchi kwa ujumla.

Wanataka Rais apunguziwe ulinzi , ili iweje napata mashaka kwa nini wanataka ulinzi upunguzwe.
Rais wetu amefanya mambo na maamuz makubwa ya kizalendo ambayo bila shaka yamewajeruhi baadhi ya watu wabaya wa ndani na nje ya nchi hivyo kuongozewa ulinzi ni jambo la umuhimu mkubwa.

Sio wote wanaofurahia tunavyopiga maendeleo kwa haraka, sio wote wamefurahi tunavyojenga bwawa la Stiegelers Gorge, reli ya Sgr au kukamua majipu ya mafisadi chini ya mzalendo nambari moja Jpm.

Lazima hatua za tahadhari zichukuliwe kwa manufaa ya nchi.
Kuna mambo mengi mazuri tunayoweza kujadili lakini sio ulinzi wa mkuu wa nchi hao tuwaachie wanatasnia wenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
(Convyoy Protection Jammer) katika msafara wa Rais lina kazi gani?

Mkuu hilo si swali la kawaida sana, hata wewe huenda ulikuwa hujui kazi ya hilo gari na hata wana JF kibao tu hawajui, sasa kuuliza hvo kuna ubaya gani.???

Hakikisha lumumba wamekupa posho yako, usisahau hilo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wazungu tuliozuia wasiondoke na mchanga, wauza unga na mitandao yao, wa meno ya tembo na mitandao yao, wapiga dili sekta za umma na matajiri mafisadi na wakwepa kodi huwa ni watu hatari sana unapoendesha vita vya uchumi
Hamna vita ya uchumi hapo..!
 
Wasiwasi wangu kuna siku yanaweza kutokea mauaji ya raia ya bahati mbaya,
Woga ukizidi unaweza kupiga yowe pasi na kitu,
Nachelea kusema isije tokea siku moja wakafyatua hizo machine zao kwa hofu zao.
 
Jana msafara wake ulienda kuaga mwili wa "afisa" mmoja wa TISS, kila kona ya bara bara kukawa na askari wenye mitutu ya bunduki. Leo pia vivyo hivyo.

Nimejikuta najiuliza hivi ni adui au maadui gani hawa wanamtisha na kumuogofya Mkuu wetu wa nchi anayependwa na wananchi wake kiasi hiki?

Isije tokea siku tukapoteza risasi zetu kwa kuua Inzi..!

Mafisadi na mabeberu wanamsaka saka, labda
 
Dikteta Magufuli amejitengenezea maadui kwa matendo yake maovu kwa Jamii ya Watz!

Dikteta Muamar Gadafy alikuwa akilindwa na Makomandoo 300. Where is he now?
Hata akiwa na ulinzi wa Makomandoo milioni 1 siku Wananchi wakikinukisha atang'oka tu!

Fuatilia vizuri. Bila madege na msaada mkubwa wa wazungu waandamanaji wasingefua dafu. Saa hizi walibya wangekuwa wanaendelea kula bata kwa kulipiwa mahari, umeme bure, elimu bure na nk. Saa hizi wanapata taabu sana. Chunguza kinachoendelea siku hizi pande zile
 
jamani kama kuna kitu cha kuogopwa kama ukoma ni uoga
1. Enzi zile za kusoma novel james hardley chase aliandika novel yake akaiita "the guilty are afraid".
2. Nyakati nyingine vyombo vya usalama na wanufaika wa makandokando ya kuwa karibu na mfalme humjengea na kumwaminisha kuwa wao ndio wana dhamana ya usalama wake ili wajikite zaidi karibu naye.
 
Maskini huwa hana madhara kwa kiongozi wa juu hata kama hapewi upendeleo.
Tajiri anamadhara makubwa kwa kiongozi wa juu endapo maslahi yake yasiyo ya haki yakiingiliwa.
 
Na zaidi, kila mwananchi alikuwa ni mwanausalama. Kwa sisi tuliokuwa vijijini, wageni walitolewa taarifa kwa balozi wa nyumba 10. Kulikuwa na uzalendo wa kweli. Sasa hivi tunadanganyana tu. Na kila mtu anajua hivyo. Wanajua kuwa wameharibu uzalendo.
hilo ndilo jibu halisi la Nguruvi3 na wenzake na iwe fundisho, Raia ndio walinzi wa kwanza kuliko hayo masilaha, taarifa zote za yaliyotaka kutoea kwa Mwl Nyerere RIP yalitolewa na raia km dereva Taxi, wanajeshi waliokuwa kambini na sio TISS
Ndo yule afisa aliyeshiriki kumpiga Lissu risasi aliefia muhimbili???
ndio huyo huyo, na maisha yake yote alifichwa ghorofa la pale mwisho wa reli bandarii akiwa na wenzake, sasa katangulia kamuacha mwenzake mzima, yeye kaitia aibu familia yake na mazishi yake wayalinde hivyohivyo HAPOKELEWI popote acheni akakae anapostahili kwa dhambi zake
 
hilo ndilo jibu halisi la Nguruvi3 na wenzake na iwe fundisho, Raia ndio walinzi wa kwanza kuliko hayo masilaha, taarifa zote za yaliyotaka kutoea kwa Mwl Nyerere RIP yalitolewa na raia km dereva Taxi, wanajeshi waliokuwa kambini na sio TISS

ndio huyo huyo, na maisha yake yote alifichwa ghorofa la pale mwisho wa reli bandarii akiwa na wenzake, sasa katangulia kamuacha mwenzake mzima, yeye kaitia aibu familia yake na mazishi yake wayalinde hivyohivyo HAPOKELEWI popote acheni akakae anapostahili kwa dhambi zake
mwisho wa ubaya ni aibu
 
Tatizo mambo serious unaleta utani..hapo kuna issue bado zipo kwenye upelelzi unazileta hapa za nini..? Kumbe jibu lako ni la kihisia zaidi..nilidhani unaleta mifano hai..lakini nikutonye jomba, kati ya hayo uliyoyataja, kuna baadhi ya kesi wanasema yapo hukohuko kwenu yanajulikana...sasa mmeshafanya Serikali ni jamvi la bibi..madudu yote mnarushia huko.....be careful...mnachinjana wenyewe kwa wenyewe halaf mnasingizia serikai..huu ni ujinga wa division nine
Naona una matatizo, na hujui ufanyalo au uandikacho, unafikiri hiyo kalamu na kiti utavikalia mpaka lini?
Trump anakosolewa na hatumii ubabe wake wa Rais wa USA
 
Jana msafara wake ulienda kuaga mwili wa "afisa" mmoja wa TISS, kila kona ya bara bara kukawa na askari wenye mitutu ya bunduki. Leo pia vivyo hivyo.

Nimejikuta najiuliza hivi ni adui au maadui gani hawa wanamtisha na kumuogofya Mkuu wetu wa nchi anayependwa na wananchi wake kiasi hiki?

Isije tokea siku tukapoteza risasi zetu kwa kuua Inzi..!
Ukiwemo wewe na wasaliti wenzio!
 
Alitekwa MO dewj anaependwa na asie na maadui kwa sababu tusizozijua,wametekwa kina rOMA,...Watu kibao wanapotea hovyo kwasababu zisizo julikana na hao wote hawana maadui,hawajulikani kama RAIS ila mnashangaaa RAIS kwanin analindwa Si eti??

Jaribuni kupita pita maeneo alipo MO au msogeleeeni sasa hivi muone Kama anafikika tena kirahisi kama zamani? hiii nchi kila mtu na ajali usalama wake,na afanyacho Rais hata ungekua wewe ungeimarisha ulinzi TU tena ikumbukwe Rais ndio ana maadui kila hatua anayopiga kwanini asijiwekee ULINZI??

au mnafikiri Rais haogopi yanayowakuta kina MO,ROMA,waandishi wa habari wanaotekwa,nk mnafikiri yeye sio binadamu eeeh HAOGOPI??? hata ingekua wewe ungeogopa na inawezekana ungejiwekea ulinzi kuliko hata anaojiwekea RAIS wetu leo.

Rais haogop mtu ana jihami tu na hiyo ni kawaida...Nendeni mbuga za wanyama alafu katembeeni kwa miguuu mpishane na simba Tuone kamaa mnaweza,maana mnajitia hamuifahamu TANZANIA na watu wasiojulikana.
 
Angalia kinachotokea Venezuela kisa Maduro anazuia mafuta kama mtangulizi wake Hugo Chavez ambaye inasemekana walimpa sumu ya kufa taratibu alipoenda mikutano ya kimataifa kwao. Hata Kim Jong Un, usipozuia maslahi yao huna haja hata ya ulinzi seriously, malawi wana tumbaku na Chai tu umeona wazungu wanahangaika nao??, Hata ziara za kuelekea Malawi hakuna. Inafaa kuwaangalia wazungu kwa upeo mkubwa, hapo Uganda kabla jamaa hajagundua mafuta kelele kila siku umekaa muda mrefu ustaafu, alivyogundua mafuta kelele Imeisha wanajua bora wanaemmudu kuliko aje mpya kama Magufuli. Unatakiwa kuwa na upeo kuwaelewa wale jamaa
kwaio unahisi magufuli anauwezo wa kupambambana na wahisani. ..never on earth's miaka ya 70 pekee ndo walitokea maraisi kama akina sankara na wengine wale walipambana live kabisa na kukataa kabisa misaada...huku akina magufuli wanaitaka hiyo misaada afu uku kwa wananchi wanajidai wanapambana ushawahi ona wapi hiyooo
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom