Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,316
- 33,125
Tofauti kati ya Madhiy na Manii hebu soma hapo chini hii ni faida kwa watu wote.
Manii
Shahawa (manii) ya mwanamume ni maji meupe mazito. Kwa mwanamke ni ya rangi ya manjano na mepesi. Manii kwa kawaida huwa ni maji yanayotokwa kwa mwanamume au mwanamke wakati wa kilele cha raha wakati wa mapenzi.
Sifa zifuatazo tatu ndizo zenye kujulisha manii ya mwanamume:
1. Kutoka kwake kunaambatana na kilele cha raha na kufuatilia uchovu.
2. Harufu yake ni kama chavuo (pollen) ya mtende ambayo huwa kama harufu ya unga uliokandwa.
3. Hutoka kwa kububujika kwa nguvu.
Mojawapo katika sifa hizo inatosha kutambulisha kuwa ni manii.
Ikiwa mtu ametokwa na maji na hazikupatikana sifa hizo basi hayatakuwa ni manii.
Sifa mbili za manii ya mwanamke:
1. Yana harufu kama harufu ya manii ya mwanamume.
2. Kutokwa kwake kunaambatana na hisia ya kilele cha raha na hufuatilia na uchovu.
Madhiy
Madhiy ni maji yenye kunata na yanamtoka mtu aidha anapokuwa anawaza au kutamani kujimai, au hata bila ya kuwaza kama ilivyo katika hali ya muulizaji. Na hazina sifa kama sifa za manii tulizozitaja hapo juu. Na pia huwatokea wanawake na wanaume ila aghlabu huwatokea sana wanawake.
B-Tofauti kuhusu ya hukumu yake baada ya kutokwa
Manii:
Yanapotoka manii, inampasa mtu akoge kwa ajili ya kujitoharisha (janaabah) ikiwa yamemtoka mtu manii wakati wa kujimai au kwa hali yoyote nyingine ikiwa yu macho au ameota ndoto n.k.
Madhiy
Yanapomtoka mtu madhiy humpasa kufanya aoshe tu kwa maji ajisafishe tu haipasi mtu kuoga.
Manii ni Tohara sio najisi.
Kwa vile manii ni tohara, basi yatakapoingia katika nguo hayafanyi nguo kuwa ni najisi, na anaweza mtu kuswalia nayo nguo hiyo. Lakini ni bora kuyafuta Hata kama inasemekana kuwa manii ni tohara, lakini ni bora kuyafuta,
Madhii ni najisi
Madhii yakiingia katika nguo inatosheleza kurashia maji juu yake kwa sababu kuepusha mashaka ya kuoga kila mara.