Ni kigezo gani unatumia kuamua kutumia aina moja ya mtandao wa kijamii?

mahwelu

JF-Expert Member
Jun 8, 2013
322
252
Wakuu,

Nafanya utafiti mahala nataka kupata idea tu juu ya maamuzi yetu juu ya matumisi ya social media platform.

Hivi ni kigezo gani kinakufanya utumie facebook badala ya twitter or instagram, snapchat or any choices tunazotumia kumake decision ni zipi?

Au najua wengi tupo kwenye vyote hivyo why mtu unakuwa mitandao yote? Je ni services au ni marafiki au nini hasa?

Mara nyingi humu JF nasikia mnasema haya mambo peleka facebook, huwa nawaza why?

Nawashukuru angalau kwa kusoma tu. Hakuna jibu sahihi ni mtazamo wa kila mtu kivyake?

Nangu Mahwelu
 
Insta nipo kwa ajili ya umbeya wa Dada Mange, JF nipo sababu member ni wengi afu kuna madini mengi sana lakini tatizo lingine kuna Wana JF hewa kibao so be careful.
 
Insta nipo kwa ajili ya umbeya wa Dada Mange, JF nipo sababu member ni wengi afu kuna madini mengi sana lakini tatizo lingine kuna Wana JF hewa kibao so be careful.
=== Thank you. So ulijiunga baada ya kujua habari za madini au ulikuwa influenced na nini?
 
Nikiwaga bado mdogo miaka kadhaa iliyopita nilikuwa natumia Facebook ila nilikuja kuona ni mtandao mmoja wa kishamba sana.

Nikatumia Insta ila nikaja kujua kuweka mapicha yako mitandaoni ni ushamba.

Tweeter nikawa naitumia ila nasoma news na updates za michezo na habari mbali mbali..

WhatsApp natumia ila huwa nina muda wa kuingia sio wakati wote.

JF niliwahi kutumia miaka miwili imepita ila nilikua sana sana ni observer sichangii nasoma tu, ila recently asee hii platform imeingia damuni mwangu kiasi kwamba muda mwingi siku hizi naumalizia humu JF. Ashukuriwe aliekuja na wazo la kuitengeneza hii sehemu japo ID asilimia 90+ ni fake ila kuna watu wana madini na kuna watu wengine inabidi ucheke tu.

Humu Jf huwa muda mwingine watu wananiona chizi kwa kuchekea simu maana kuna raha sanaa.. Unapata kujifunza kupitia mikasa ya watu wengine, kujua fursa nyingi maishani, kupata elimu nyingi sana.

Nashukuru sana kuwepo humu JF namuomba Mungu siku zote iwe kama hivi nisipate sababu ya kuondoka humu mpaka siku akiamua kumtuma agent wake mtoa roho bwana Israel aje ghetoni kwangu kuni arrest
 
Mkuu unajua kila mtandao wa kijamii Una raha yake na umuhimu wake kwa nyakati tofauti, ndo mana unakuta mtu yupo mitandao yote au yupo mtandao mmoja ni kulingana na mahitaji au kupenda tuu

>>Twitter kwa sababu viongozi wengi hata maraisi hutumia mtandao huu ku posti vitu vyao hivyoo watu Smart ambao hawapendi umbea au utaku wana uchukia huu mtandao

<<Facebook, asee umbea wote upo huku na ukikuta mtu a akwambia anatumia mtandao mmoja obviosly utakuwa ni huu, vituko, kujiachia ni huku

Instagram <<huku ndo usiseme huyu mdogo wake Facebook tatizo kila mtu ana baba yake

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
Dahh.. mpaka leo sijawahi tumia instagram... Twitter toka nijiunge sijawahi itumia...... Facebook ilinishinda sikunyingi sana..... so zaidi ya JF sina pakupotezea Mb zangu.
 
Wakuu,

Nafanya utafiti mahala nataka kupata idea tu juu ya maamuzi yetu juu ya matumisi ya social media platform.

Hivi ni kigezo gani kinakufanya utumie facebook badala ya twitter or instagram, snapchat or any choices tunazotumia kumake decision ni zipi?

Au najua wengi tupo kwenye vyote hivyo why mtu unakuwa mitandao yote? Je ni services au ni marafiki au nini hasa?

Mara nyingi humu JF nasikia mnasema haya mambo peleka facebook, huwa nawaza why?

Nawashukuru angalau kwa kusoma tu. Hakuna jibu sahihi ni mtazamo wa kila mtu kivyake?

Nangu Mahwelu
Wewe mmasai?????
 
=== Thank you. So ulijiunga baada ya kujua habari za madini au ulikuwa influenced na nini?
Madini namaanisha thamani yaani kuna taarifa nyingi za ukweli na Uhakika. Kwa kifupi kuna Wajuvi wengi wanajua nini wanachochangia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom