Ni kifungu gani kinamlazimisha mwanaume wa kikristo kuwa na mke mmoja?

Ahsante kwa mchango wako mkuu, lakini nadhani hakukuwa na haja...hivi ukienda kuprint document unaprint kwa idadi ya copy unazotaka au unaprint moja then unatoa copy?
Kama printa ninayo na mimi mwenyewe ndo nimetype kuna anayenizuia kuprint idadi ninayotaka kuanza nayo ili wengine wakatoe copy katika hizo originals??
 
Mojawapo ya Mila ya Ibrahim ni kutahiriwa nyama ya govi niwekee Ushahidi ibn abd'allah katahiriwa nyama ya govi lake
Mada kuu inahusu kuoa MKE zaidi ya mmoja.
Hilo la kutahiriwa ni nje ya mada.

Hata hivyo,ni dhahiri umeonesha ujinga wako kwa kukitoa kitendo cha KUTAHILI katika MILA ya Ibrahim.
Inaelekea hata maana ya neno MILA ujui.
 
Kwnye kitabu cha mwanzo
Huwa wanapenda kulisoma kwny misa ya ndoa
Mwanaume ataacha wazazi wake and viceversa ataambatana na mkewe..nao watakua mwili mmoja

Adamu aliumbwa mmoja na Hawa mmoja
So its implied.,

Waliooa wake wengi hamna ubarikio wa ndoa
kuhalalisha mke wa pili...atleast mi sijaona ibada ya mke wa pili na kuendelea..wajuvi watasaidia
Mfano Ibrahim mke wake Sara..yule mjakazi ilitokea kama default na badae kuishi pale ilishindikana sio kwamba aliolewa official or anything

Ubarikio wa ndoa ya mke mmoja tumeona
1.Adam na Hawa
2.Rebeca na Isaac,
3.Yakobo na Rachel...japo kimazingira alifosiwa kuoa dadake kwanza /Leahh..ye alimpenda Rachel pale
4.Mtaongezea
Unaweza tusaidia maandiko ya maelekezo ya jinsi ya ufungaji ndoa ndani ya biblia?.
Je,taratibu zitumikazo kanisani kufungisha ndoa,zimepatikana toka katika kifungu kipi cha maandiko ya biblia?.
 
Kwnye kitabu cha mwanzo
Huwa wanapenda kulisoma kwny misa ya ndoa
Mwanaume ataacha wazazi wake and viceversa ataambatana na mkewe..nao watakua mwili mmoja

Adamu aliumbwa mmoja na Hawa mmoja
So its implied.,

Waliooa wake wengi hamna ubarikio wa ndoa
kuhalalisha mke wa pili...atleast mi sijaona ibada ya mke wa pili na kuendelea..wajuvi watasaidia
Mfano Ibrahim mke wake Sara..yule mjakazi ilitokea kama default na badae kuishi pale ilishindikana sio kwamba aliolewa official or anything

Ubarikio wa ndoa ya mke mmoja tumeona
1.Adam na Hawa
2.Rebeca na Isaac,
3.Yakobo na Rachel...japo kimazingira alifosiwa kuoa dadake kwanza /Leahh..ye alimpenda Rachel pale
4.Mtaongezea
Unataka ubarikio upi ikiwa Yakobo(Israel) na watoto wake(wanna wa Israel) walibarikiwa?.Na wakati wana wa Israel ni watoto wa matumbo tofauti?.
 
Kwenye 1 WaFalme 11:1-3, kwa nini Suleiman alikuwa na wake 700 na Masuria 300, kinyume cha amri ya Mungu ya kwenye Kumb 17:17?

Jibu: Kumbukumbu 17:17 inasema mfalme asiwe na wake wengi, na kwa kitendo hicho, Suleiman alifanya dhambi. Kuoa wake ilikuwa ni njia ya kuimarisha ushirikiano na falme nyingine, lakini pia ilikuwa ni makosa kutokumtii Mungu. 1 Fal 11:1-6 inasema kuwa Suleiman alifanya dhambi kwa kuoa hawa wake wageni, na kuugeuzia moyo wake kuwa mbali na Mungu.


1 Wafalme 11: 1-11

1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,

2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.

3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.

4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.

5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.

6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.

7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.

8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.

9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,

10 akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.

11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako.
Ebu muelezee na Yakobo (Israel) basi,maana yeye pia alikuwa na wake wengi.Na makabila 12 ya wana wa Israel,yametokana na wanawake wengi.
 
WANAWAKE SABA...MME MMOJA !

ISAYA 4:1 Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema ,tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe,lakini tuitwe tu kwa jina lako,utuondolee aibu yetu.

A. SIFA TANO ZINAZOWATAMBULISHA WANAWAKE SABA
I. Wanawake Saba wanatarajia au wanakusudia kuolewa na mume mmoja.
II. Wanawake hawa watakula chakula chao inamaanisha hawatamtegemea mume mmoja.
III. Wanawake hawa pia watavaa nguo zao hawatamgemea mume mmoja
IV. Wanawake hawa wanachohitaji kingine ni kuitwa kwa jina la huyo mume mmoja
V. Kusudi kubwa la kutaka kuolewa na mume mmoja wakati wao wako saba Wanachohitaji ni kuondolewa aibu yao

B. JE MWANAMKE KATIKA UNABII HUWAKILISHA NINI?
Mwanamke huwakilisha kanisa ;
YEREMIA 6:2 Binti sayuni aliye mzuri, mwororo……
WAEFESO 5:25-27 Enyi wanaume wapendeni wake zenu ,kama Kristo naye alivyolipenda kanisa ,akajitoa kwa ajiri yake ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno. apate kujiletea kanisa tukufu ,lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo ,bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

C. JE KWANINI KUNA WANAWAKE SABA NA SIO ZAIDI AU PUNGUFU
Namba Saba inamaana ya kutimiza au kukamilisha

D. JE WANAWAKE SABA HUWAKILISHA NINI?
Kwa sababu katika unabii mwanamke ni mfano wa kanisa , mwanamke safi akiwa kanisa safi na mwanamke muovu kanisa chafu. Hivyo wanawake saba huwakilisha makanisa mbalimbali yatakayotokea dunia.

E. JE MUME MMOJA ANAMWAKILISHWA NANI?
2 WAKORINTHO 11:2 Maana nawaonea wivu,wivu wa Mungu ;kwa kuwa kuwa naliwaposea mume mmoja,ili ni mletee Kristo bikira safi

MAELEZO MAFUPI
Mume mmoja hapa anamwakilisha Kristo,

F. JE CHAKULA WANACHOSEMA WATAJITEGEMEA HAO WANAWAKE KINAWAKILISHA NINI?
Chakula kinawakilisha -Neno la Mungu soma
MATHAYO 4:4 Naye akajibu, akasema imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu;
LUKA 22:19 Akatwa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema,[huu ndio mwili wangu uliotolewa kwa ajiri yenu fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu]

MAELEZO MAFUPI
Chakula ambacho hawa wanawake (makanisa) wanadai kujitegemea wenyewe bila kumtemea mume mmoja ambaye ni Yesu, huwakilisha mafundishisho mbalimbali yanayofundishwa kwenye hayo makanisa chanzo chake hayatokani na Kristo bali kila kanisa linajitegemea mafundisho yake.;

G. JE MAVAZI WANAYOVAA AU NGUO ZINAWAKILISHA NINI
Nguo nyeupe huwakilisha matendo mema ya wacha Mungu, na nguo chafu huwakilisha matendo maovu

H. JE NI AIBU YA AINA GANI WANAHITAJI IONDOLEWE?
I. Kama tulivyojifunza mwanamke huwakilisha kanisa hivyo wanawake wanawakilisha makanisa mbalimbali ya siku za mwisho kwa hiyo makanisa hayo yanachohitaji ni kutumia tu jina la Mungu au Yesu yaani. Ionekane tu kuwa nayo ni miongoni mwa Kanisa la Mungu, lakini uhalisia sio makanisa ya Mungu.kwa sababu mafundisho yanafundishwa humo hayatokani na Mungu mwenyewe ndio maana wanawake wanasema tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu wenyewe.
Sasa weka andiko lilokupa hiyo tafsiri.Maana usije ukawa ni muongezaji na mpunguzaji was maandiko.
 
Back
Top Bottom