Ni kifungu gani kinamlazimisha mwanaume wa kikristo kuwa na mke mmoja?

Mada kuu inahusu kuoa MKE zaidi ya mmoja.
Hilo la kutahiriwa ni nje ya mada.

Hata hivyo,ni dhahiri umeonesha ujinga wako kwa kukitoa kitendo cha KUTAHILI katika MILA ya Ibrahim.
Inaelekea hata maana ya neno MILA ujui.
Nimekujibu kihivyo baada ya wewe kunihakukishia kwamba waisilamu WOOTE Ibrahim ni KIGEZO chenu CHEMA ktk kuoa wake wengi Ndipo NIKAKUULIZA mojawapo ya miratul Ibrahim ni kutahirwa nyama ya govi lake sasa umeona ugumu gani kuniwekea USHAHIDI kama ibn abd'allah naye KATAHIRIWA nyama ya govi lake?? kama ww MUUMINI weka Ushahidi ima kafir kausha
 
Utoto bwana!.Ina maana unataka nikurudishe darasani kwa kuanza kukufundisha MILA ni nini?.
 
Kuishi mke mmoja ukubali kuwa mzinzi haiwezekani hata jogoo Anishinde mimi...Jogoo mmoja Ana mitetea kumi halafu msosi anategemea mimi mwenye tetea moja ndani...Nasema hapana!! Hii sio poa....
 
Hi Ladies, gentlemen and baharias
Naomba nieleweke kuwa lengo langu si kupingana na hili bali nataka tu kueleweshwa. Katika kusoma kwangu biblia sijaona sehemu inayozuia mtu kuwa na wake zaidi ya mmoja, hata katika kusikiliza na kusoma mafundisho mbalimbali sijawahi kuona hoja yenye uzito ila naamini hapa nitapata majibu....nitaweka hapa baadhi ya hoja ambazo huwa zinatolewa

1. Uumbaji. Ukisoma Mwanzo sura ya pili Mungu alipomuumba mwanadamu aliumba mwanaume kisha kutoka kwenye ubavu wa mwanaume akamuumba mwanamke kwa hiyo Mungu alimpa Adamu mke mmoja. Lakini je kulikuwa na haja ya kuumba wanawake wengine wakati wanaenda kuzaana? Ina maana alimaliza kila kitu kwenye hizo sample mbili, ndio maana hatuoni aliumba mzungu, mwarabu, mwafrika n.k Na kama jambo hilo ni haramu kiasi hicho mbele za Mungu kwa nini aliruhusu watakatifu wale wa zamani mf. Yakobo, Daudi na wengineo kuwa na wake zaidi ya mmoja?
2. Mafundisho ya Bwana Yesu. Baadhi ya mafundisho yanayorejewa ni

Mathayo 19:4, 5
4 Akawajibu: “Je, hamkusoma kwamba yule aliyewaumba tangu mwanzo aliwaumba mwanamume na mwanamkea 5 na kusema: ‘Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’

Hapa Bwana Yesu alikuwa anajibu kuhusu talaka, lakini mimi nadhani mtu mmoja anaweza kuwa mwili mmoja na huyu na akawa mwili mmoja na mtu wa pili pia bila kuathiri muunganiko wa kwanza

3. Mafundisho ya Mtume Paulo
1 Wakorintho 7:2
2 lakini kwa sababu ya kuenea kwa uasherati,* kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewea na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.

Hapa kilichokatazwa ni uasherati, sioni uhusiano wa idadi ya wanawake na hili andiko maana hata ukiwa nao wawili bado ni wake zako mwenyewe.

1Timotheo 3
1 Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. 2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkarimu, ajuaye kufundisha; 3asiwe mtu wa kulewa, asiye dhalimu; bali awe mpole; asiwe mbishi wala asiwe mwenye kupenda fedha;.......
Hapa amezungumziwa askofu au mwangalizi wa kanisa, je kama sio askofu? KItu kingine kinachonitatiza hapa ni kuwa Paulo alikuwa anazungumzia watu wanaoamini (kanisa), anaposema askofu awe mwanaume wamke mmoja in maana katika kanisa kuna watu wenye wake zaidi ya mmoja? kwa sababu ni wazi askofu hawezi kutoka nje ya kanisa bali miongoni mwa haohao waumini.
Kama hawapo watu wasio na mke mmoja kwa nini aliweka hicho kigezo?

Samahani siko vizuri kwenye kuandika na kupangilia hoja lakini nadhani mmenielewa.

NB; Nimejikita upande mmoja wa wanaume ili tusitoke kwenye mlengo wa mada

Kwanza ninakupongeza kwa hoja yako fikirishi na yenye utafiti ndani yake, HONGERA!!!!

Pili: Unapouliza chochote kuhusu dini huwa ni suala mtambuka ukizingatia wale ambao tulipaswa kuwauliza maswali hayo (Mitume na Manabii) walishakufa hivyo kila mmoja wetu ana uelewa wake kulingana na mapokeo, mazingira alimokulia, malezi na mafundisho aliyopitia. Ndyo maana unakuta dini moja lakini ina madhehebu ( hiyo inawakilisha utofauti wa fikra katika kuyaelewa mambo).Hivyo usitegemee jibu la moja kwa moja.

Tatu: Nijuavyo mimi kuhusu kuoa ni kuwa MUNGU hakuruhusu wala kukataza wanaume kuoa au wanawake kuolewa, hayo yamejili baada ya kusema enendeleni mkazaane muujaze ulimwengu. Sasa kwa kuwa binadamu ni tofauti na wanyama (Sisi tulipewa akili ya kujua baya na jema) ndiyo wakaweka utaratibu wa ndoa kulingana na tamaduni za kila kabila. Hii ya kusema Ndoa ya kikristo ni mke mmoja ililetwa na utamaduni wa Roman Empire maana wao ndio waliueneza ukristo duniani (madhehebu mengi ya kikristo yalijitenga kutoka RC) lakini haukusisitizwa popote katika Biblia.

Nne: Kutokana na uvivu wetu wa kufikiri (Wakristo wa mwanzo), tulishindwa kuhoji vitu vingi tulivyokua tukifundishwa ndio maana hata wamisionary walitubatiza majina ya kikwao (Kizungu) kwa kutudanganya kuwa eti ni majina ya kikristo (Siyo kweli maana dini haina majina). Wengi wetu tunakariri dini badala ya kuielewa.

BINAFSI SIJAWAHI KUSIKIA/KUSOMA MTU AMEHESABIWA DHAMBI KWA KUWA NA MKE ZAIDI YA MMOJA MAANA HATA KWENYE AMRI KUMI ZA MUNGU HAKUNA SEHEMU AMEKATAZA.

Nne:
 
Ahsante kwa majibu mazuri, nadhani unaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom