Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 11,634
- 26,373
Habari wakuu,
Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na mlipuko wa magonjwa mbalimbali ambayo katika jamii zetu hayakuzoeleka hivyo yanapotokea huleta shida tangu hatua za kugundua na matibabu yake na hivyo kuwagharimu wagonjwa pesa nyingi.
Swali langu ni Je magonjwa haya ambayo yote huenezwa na mbu na tayari yamesharipotiwa kutokea hapa Tanazania katika vipindi tofauti yanagundulika kwa kutumia vifaa gani?( diagnostic)
Tunajua malaria inapimwa kwa darubini na njia nyingine ambayo wataalam wanajua
Je ugonjwa wa Chikungunya na Dengue wanapima kwa kutumia kifaa gani maana kuna kipindi mtu akipata dengue ilikuwa anatoa hadi 50,000 kupata kipimo tena kwenye baadhi tu ya hospitali mjini.
Lengo ni kujua namna gani vijijini watapata huduma kama hii maana mtu anaweza kuugua mfano Chikungunya halafu akakosa vipimo au akanunua dawa akidhani ni malaria ambayo imezoeleka matokea yake ikamuathiri
Karibuni wataalamu.
Sent using Jamii Forums mobile app