Kabwela
Member
- Feb 11, 2008
- 76
- 5
Napenda kuanza kwa kusikitika ninapoona mtanzania hasa mwenye dhamana kubwa kama mhariri wa gazeti linalosomwa na watanzania idadi ya kutosha akiingilia kupiga kampeni ambayo hana utaalamu nayo hasa kuhusu suala la DDT.
Tatizo lililopo ni wanahabari nao kuingia kwenye siasa. Mhariri wa gazeti la Mtanzania katika tahariri yake ya tarehe 16 Februari 2010 toleo Na. 5026 anaongelea mambo mengi kuhusu Malaria na kilichonisukuma hapa ni hoja ya Ni kichaa pekee anayeweza kusimama akipinga Matumizi ya DDT. Angefahamu utaratibu unaotakiwa na shirika la Afya duniani (WHO Indoor Residual Spray guidelines) za kupulizia DDT wala asingeshauri i nyunyizwe nje kwenye mazingira. Ulaya na marekani walipiga marufuku matumizi ya DDT miaka ya 1970.
Anachokiongelea muhariri katika kuonesha Ngao haifanyi kazi kikamilifu yaweza kusababishwa na Kutofuata taratibu katika uwekaji wa ngao kwenye vyandarua na Kutumia ngao feki.
Kuwepo kwa kemikali feki ni tatizo kubwa sana kwa Tanzania na nchi nyingi za Afrika na hii unaweza kuona vizuri zaidi ukubwa watatizo wa mipaka isiyodhibitiwa pia kwenye zebaki ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ambao wanatumia zebaki kwa wingi lakini hakuna muagizaji aliyesajili Tanzania kwa muda wa miaka 10 iliyopita. Na kuna utafiti ulifanywa na TPRI ukaoneha kuwa zaidi ya 35% ya viuatilifu vinavyopatikana mbeya vimeingia kwa njia za panya. Kwa Dar es Salaam ni tatizo kubwa zaidi kwani hata kariakoo zimejaa pia wanaouza sumu za panya mpaka kwenye mabaa na barabarani ni wengi mno ambyo ni kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Kuondoa mazalia ya mbu hakufanikishwi kwa kupulizia kemikali tu hata kufyeka majani, kuzibua mitaroo, kuondoa mazalia yao, kufunga milango asubuhi sana na jioni vina mchango mkubwa sana kupunguza mbu kumngata binadam.
Kinachonisikitisha ni kuwa muhariri huyohuyo atatuhamasisha tuchangie katika kupima na kutibu kansa ambayo husababishwa na kuwepo DDT kwenye mazingira na pia ongezeko la ugonjwa wa kisukari dinuiani kumehusianishwa na DDT pia (soma matokeo ya utafiti wa karibuni wa WHO). Ukiangalia matatizo ya kansa yameonekana kuwa mangi zaidi maeneo ambayo ilitumika kwa wingi kwenye mazao ya biashara kama kahawa, pamba na mengineyo.
Pia mhariri hajasoma sheria za masoko ya bidhaa za kimataifa zinavyokataza kuwepo hata kwa kiasi kidogo cha DDT kwenye bidhaa (pesticides residues in products) hizo, sasa anataka Tanzania tuzuiwe kuuza mazao mbalimbali na hata samaki waliotuletea kashfa ya mapanki ulaya na marekani. Ywezekana amekurupuka au ametumwa na watu ambao wamepata dili la kuagiza hiyo DDT nchini.
Namshauri mhariri asome matokeo ya tafiti na afanye utafiti wa kutosha kabla hajaanza kutukana watu bila sababu na mwishowe yeye ndiye anaonekana hajui hata moja katika analoliongelea.
Namsikitikia mhariri wa gazeti la Mtanzania anapoonekana mjinga kwa kukurupuka kuongelea asilolijua.