Ni kichaa pekee anayeweza kusimama akipinga Matumizi ya DDT

Kabwela

Member
Feb 11, 2008
76
5
Napenda kuanza kwa kusikitika ninapoona mtanzania hasa mwenye dhamana kubwa kama mhariri wa gazeti linalosomwa na watanzania idadi ya kutosha akiingilia kupiga kampeni ambayo hana utaalamu nayo hasa kuhusu suala la DDT.

Tatizo lililopo ni wanahabari nao kuingia kwenye siasa. Mhariri wa gazeti la Mtanzania katika tahariri yake ya tarehe 16 Februari 2010 toleo Na. 5026 anaongelea mambo mengi kuhusu Malaria na kilichonisukuma hapa ni hoja ya “Ni kichaa pekee anayeweza kusimama akipinga Matumizi ya DDT”. Angefahamu utaratibu unaotakiwa na shirika la Afya duniani (WHO Indoor Residual Spray guidelines) za kupulizia DDT wala asingeshauri i nyunyizwe nje kwenye mazingira. Ulaya na marekani walipiga marufuku matumizi ya DDT miaka ya 1970.

Anachokiongelea muhariri katika kuonesha Ngao haifanyi kazi kikamilifu yaweza kusababishwa na Kutofuata taratibu katika uwekaji wa ngao kwenye vyandarua na Kutumia ngao feki.

Kuwepo kwa kemikali feki ni tatizo kubwa sana kwa Tanzania na nchi nyingi za Afrika na hii unaweza kuona vizuri zaidi ukubwa watatizo wa mipaka isiyodhibitiwa pia kwenye zebaki ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ambao wanatumia zebaki kwa wingi lakini hakuna muagizaji aliyesajili Tanzania kwa muda wa miaka 10 iliyopita. Na kuna utafiti ulifanywa na TPRI ukaoneha kuwa zaidi ya 35% ya viuatilifu vinavyopatikana mbeya vimeingia kwa njia za panya. Kwa Dar es Salaam ni tatizo kubwa zaidi kwani hata kariakoo zimejaa pia wanaouza sumu za panya mpaka kwenye mabaa na barabarani ni wengi mno ambyo ni kinyume na sheria na taratibu za nchi.

Kuondoa mazalia ya mbu hakufanikishwi kwa kupulizia kemikali tu hata kufyeka majani, kuzibua mitaroo, kuondoa mazalia yao, kufunga milango asubuhi sana na jioni vina mchango mkubwa sana kupunguza mbu kumng’ata binadam.

Kinachonisikitisha ni kuwa muhariri huyohuyo atatuhamasisha tuchangie katika kupima na kutibu kansa ambayo husababishwa na kuwepo DDT kwenye mazingira na pia ongezeko la ugonjwa wa kisukari dinuiani kumehusianishwa na DDT pia (soma matokeo ya utafiti wa karibuni wa WHO). Ukiangalia matatizo ya kansa yameonekana kuwa mangi zaidi maeneo ambayo ilitumika kwa wingi kwenye mazao ya biashara kama kahawa, pamba na mengineyo.

Pia mhariri hajasoma sheria za masoko ya bidhaa za kimataifa zinavyokataza kuwepo hata kwa kiasi kidogo cha DDT kwenye bidhaa (pesticides residues in products) hizo, sasa anataka Tanzania tuzuiwe kuuza mazao mbalimbali na hata samaki waliotuletea kashfa ya mapanki ulaya na marekani. Ywezekana amekurupuka au ametumwa na watu ambao wamepata dili la kuagiza hiyo DDT nchini.

Namshauri mhariri asome matokeo ya tafiti na afanye utafiti wa kutosha kabla hajaanza kutukana watu bila sababu na mwishowe yeye ndiye anaonekana hajui hata moja katika analoliongelea.

Namsikitikia mhariri wa gazeti la Mtanzania anapoonekana mjinga kwa kukurupuka kuongelea asilolijua.
 
Huyo Mhariri hata hakuingia kwenye website yo yote akaangalia madhara ya DDT, yeye alijiandikia tu (samahani sana).

Ni kweli kama mdau wa kwanza alivyosema, mazao yote yenye residues za DDT huwa hayakubaliwi kwenye soko la ulaya, iweje leo ishereheshwe kwa nguvu zote katika nchi zetu?

Baada ya muda utakuja kusikia ooooooh kumbe ile DDT bado ina madhara sisi hatukujua!
 
Nimesikia ZNZ wamefanikiwa kudhibiti MALARIA...wametumia nini wenzetu?

Pia Wa-china wamefanya tafiti za Dawa Malaria na wamefanya test Visiwa vya COMORO..na success imekuwa zaid ya 90-99%..Japo WHO wamekataa Tafiti za Wachina.

Watafiti wa Kizungu naona kila Miaka wanatubadilishia Dawa...mara mseto...mara choroko etc. at last wanaoumia ni Watanzania.

Karibu Dawa Zote zina side effects.(Madhara)..wanachopima madaktari ni baina ya Madhara na Faida iliyopo. Ikiwa Faida ni kubwa basi dawa hio hutumika.

Ukiangalia Muda gani waingia ktk NET kulala na muda gani upo Nje...bado inasaidia lkn Mbu wataendelea kukung'ata. Hata Kufunga Milango, itategemea Milango hio ipoje, kwa Uswahilini.....Kufunga Milango pia Hakusaidiii maana Milango yenyewe Bomu....Madimbwi ya Maji machafu...Vyoo vyetu na Complex ya Uchafu...Manispaa walitakiwa wawe wasafi. na Kila Mwananchi awe MSAFI.

Nakubaliana na Suala zima la ELIMU kila Mmoja awe nayo na kuwe na Enforcement....To me kama hakuna Dawa Ingine ya kupulizia, basi DDT inaweza saidia. Nakumbuka Miaka ya Nyuma ilikuwa ikipuliziwa DAWA ENEO zima....basi hata raha kulala Nje, maana Hakuna MBU...sijui Dawa gani ilikuwa ikitumika lkn to a big extent ilisaidia MNO kupunguza Malaria....naona Hata akili zetu zinakuwa Mbovu kwa Kuumwa Mara kwa Mara Malaria.
 
Nadhani mhariri si kichaa na yupo sahihi kabisa, kwani WHO inaendeshwa na wazungu na siku zote wazungu wanaangalia suala lililo na masirahi kwao. Sasa ukiangalia kwa tanzania na afrika kwa ujumla Maralia ndio tatizo kila siku kuna mamilioni ya watu wanakufa kwa maralia na sio kansa na magonjwa ya moyo. Wazungu wanzungumzia sana kansa na magonjwa ya moyo kwasababu ndio yanawaua, na pia ni rahisi kusafirishika mpaka kwao kwa hiyo waliamua kudhibiti wasipate hayo magonjwa hata kama watanzania wote tutakufa. wapo tayari kuona kuwa DDT haizalishwi hata kama ingezalishwa ingaokoa mamilioni ya waafrika wanaokufa kwa maralia ili kuokoa wazungu wawili ambao wangathirika kwa masalia ya DDT kwenye mimea.

Mleta hoja tupe ulinganisho wa tafiti wa idadi ya watu wanaokufa kwa maralia na wale waliokufa kwa magonjwa uliyoyataja yanayotokana na matumizi ya DDT. Ndio maana Iran waliamua vyoyote iwavyo wanataka umeme wa nuclear, hawamsikilizi huyo unayesema dunia ya kimataifa. Na sisi tuamue tunataka kutokomeza maralia, njia ni ndogo tumia DDT nchi nzima baada ya miezi mitatu tu itakuwa haina maralia.
 
Back
Top Bottom