Ni kesi zipi mtumishi wa umma anaweza kusimamishwa kazi zikifika mahakamani?

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Wanasheria naomba kuzijua ni kesi zipi mtumishi wa umma zinaweza kumsimamisha kazi zikifikishwa mahakamani?
 
Wanasheria naomba kuzijua ni kesi zipi mtumishi wa umma zinaweza kumsimamisha kazi zikifikishwa mahakamani?
f

Kwa mujibu Wa standing order pomoja na sheria ya ajira na mahusiano kazini ni makosa ya jinai pekee mtumishi akishitakiwa ndio huwa anasimamishwa kazi kama ni kesi ya madai kazi huwezi kusimamishwa
 
Kuna mtumishi wa umma alikamatwa kwa tuhuma za rushwa na kesi ipo mahakama ya kinondoni lakini mbona anaendelea na kazi?
 
Kuna mtumishi wa umma alikamatwa kwa tuhuma za rushwa na kesi ipo mahakama ya kinondoni lakini mbona anaendelea na kazi?
Kusimamishwa kazi hizi sheria pamoja na kwamba zimetoa mwongozo huo lakini pia zimempa nguvu mwajiri kutoa uamuzi huo kwa kadiri yeye atakavyoona uzito wa kosa la mtumishi yaani(his/her own discretion),ndo maana pia utaona wapo watumishi wana jinai na kazi wanaendelea.(ukisoma vizuri standing order pamoja na sheria ya ajira na mahusiano kazini utalielewa hili vizuri)
 
Na hii jinai huchunguzwa na Mwajiri au ni Jeshi la Polisi?
Jinai inachunguzwa na polisi ila uzito wa tuhuma kwa mwaajiri makini anauwezo wa kuuona na kwa discretion yake akafanya maamuzi kwa maana sheria inampa nguvu mfano una mtumishi ana tuhuma ya rushwa ndogo na mwingine ana tuhuma ya kupigana akiwa bar na akasababisha majeruhi kwa mlalamikaji nani utamsimamisha kazi na nani utamuacha?,maana zote hizo ni jinai(jibu hapo kama unapewa discretion ya kufanya maamuzi utaangalia .wenye kosa zito kati ya hayo ndio utamsimamisha kazi)
 
sijui ila ninafikiri kuwa huwa mtumishi hasimamishwi kazi kabla ya hukumu ( maana ya mshahara) na kama ni madai hamna shida sana ila kama ni jinai na kifungo kikazidi miezi 6 utasimamishwa kazi, pia inategemea na aina ya lalamiko.
 
Sio kweli!

Ukishafikishwa mahakamani tu kwa kesi ya jinai basi mwajiri anaweza kukusimisha kazi huku ukiendelea kupokea mshahara wako wote ukisubiri hukumu.( Rejea regulation ya 39 ya public service regulations of 2003)

Hukumu ikishatoka ukahukumiwa, basi mwajiri anakufukuza kazi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom