Ni kazi gani uliyowahi kufanya ambayo unafikiri hautoweza kuisahau kamwe?

ridhiwani.jpg
 
Mh. mafunzo ni mengi. Frankly speaking nazidi kuwashukuru wazazi wangu ( RIP) kwani nikisoma wengine walikopitia kwa kweli nifundisho kubwa sana.
All in all zipo kazi pia huwa sizisahau. Mama alikuwa anafuga kuku hawa wa kisasa sasa alikuwa na tenda kupeleka bandarini na uwanja wa ndege. Sasa walitakiwa asubuhi saaana hivyo ilibidi mama na sis watoto ( wakati huo nikiwa darasa la saba/ form one). Ilibidi kuamka alfajiri wanachinjwa ( kuku) tunawanyonyoa mama saa moja anawapakia kwenye gari kuwapeleka. Haikuwa kazi ngumu shida tu ilikuwa kuamaka alfajiri.
Sasa kazi nyingineambayo sitaisahau ni katka kujiongezxea kipata wakati nasoma - UK. Kazi za kufanya usafi. Kwanza kuipata kazi yenyewe niliipata kibahati ilikuwa ngumu mno , mtakumbuka wakati wa recession. Basi nilipewa eneo kubwa sana kufagia, kufuta vumbi , kupiga deki. Basi siku ya kwanza nilichoka mnooo, kufika saa12 kuondoka 2.30. lakini hupumziki. Kuna siku nilipofika supervisor akaniambai inabidi niende kufanya kazi kwa mwenzangu ana udhuru. Sitakaa nisahau kumbe pa mwanzo ilikuwa ni shushi. Nikaenda Jumba la sinema loooote usafi ilikuwa juu yangu. Kulifagia loooote- si unajua tena popcorn jengo zima. Baada ya hapo kulipiga deki ( kasoro to kwenye carpet) na kufuta vumbi. Sitakaa nisahau Mjengo wa sinema wooote. Basi kuna mzungu mmoja ( mkazi wa huko na anafanya hizo kazi) alijua fika sitaiweza hiyo kazi akajitolea kunisaidia kufagia vingine nikafanya mwenyewe. Nikaangal;ia anavyofanya siku ya pili nikafanya mwenyewe, ila hiyo siku sitakaa nisahau. Kuinama kwenye viti vile vya ukumbi na kuzoa kwa kizoleo. Jamanai pesa zinatafutwa kwa tabu! Ila uzoefu huo unanisaidia kwa sasa!
 
Kupika Gongo maeneo ya Kitunda na kisha kuisafirisha mpka manzese uwanja wa fisi na maeneo ya kizuiani mbagala... asikwambie mtu ilikuwa hatari sana kukimbizana na askari
 
Kuna binti mmoja alikuwa anafanyakazi shoppers ana jina la kipwani mwasiti or something like that nilimuelewa sana nikaamua nimtokee.

Siku ya siku nimeibuka sehemu wanakulaga lunch namuulizia naambiwa kaacha kazi kaenda kuanza chuo UDOM! Sio wewe kweli?
Mi jina langu la kikristo halina upwani hata kidogo, na chuo nilikua hapa hapa mjini.
 
Sidhani kama ana nia ya kushinda bali ni katika kuelezea ugumu wa kazi alizofanyaa nam ni kweli kazi alizofanya ngumum mnoo!
Aar wapi sio ngumu kawaida tu, Utazilinganisha na kazi za watu wengine humu Jf waliokua wanakata mikaa maporini huko nzega wanakaa wiki nzima na wanaendesha baiskeli na magunia yao ya mkaa mpk Shinyanga na waulize ujira wao ulikua ni kiasi gani.Unamlinganisha na mtu anayelipwa kwa Sterling pound(£).Acha utani aisee,hio kazi ni ya kichumba tu.
 
Nusu roho initoke 2002 nmemalza six nkapata kazi ya upagazi(uporter) mlima Kilimanjaro tumefika kambini tukapewa dumu ( pukudu) tufate maji sitasahau ule mlima ...waone wakilewa tu Ile kazi ni ngumu hapo bado umetoa jembe kwa guide, mnazidishiwa kilo na kwenye tipu guide anafunga kirunji

mkuu hiki ni kilugha au,
 
Kuna binti mmoja alikuwa anafanyakazi shoppers ana jina la kipwani mwasiti or something like that nilimuelewa sana nikaamua nimtokee.

Siku ya siku nimeibuka sehemu wanakulaga lunch namuulizia naambiwa kaacha kazi kaenda kuanza chuo UDOM! Sio wewe kweli?

mnh huku Jf kuna story ukizimwaga, unakuta umeshaivua nguo ID yako. :D:D:D
 
Nishabeba Zege......nimeuza gongo na dawa za majani.......nishakuwa konda.....na kuuza genge......
yote maisha....
 
Hiyo ya kujenga tiles ndiyo ilikua ishu, nilikutana na wadada wawili huku nimebeba mashine ya kukatia tiles, wale wadada tulikua darasa moja. Ngoma imenikuta Magomeni hospitali hakuna pa kuingia pale.
Umenichekesha sana mkuu kwani mmoja wapo ulikua unampango wa kumtongoza
 
Kuna jamaa mmoja aliniambia kuna kazi ya marketing elimu yoyote ile.Kufika tunapewa vyombo vya ndani tukauze mitaani jamani hii kazi ngumu nilifanya kwa saa mbili tu kurudi nnakuta wenzangu washabwaga manyanga sa nyingii.
 
Kaz ya kuuza duka aiseee
Af duka n la,wachaga
Umeajiriwa na mangi
Hyo kaz acha tu
Huend popotecn ww na duka
24/7 unalala hapo
Unaamka hapo
 
Back
Top Bottom