Ni kawaida yao hata mwaka 2015 walisema anatekeleza ilani ya CHADEMA

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Dr Nchemba, waziri mpya wa fedha nenda kachape kazi kweli kweli watanzania walio wengi wanakutegemea na wanajua makusanyo yatapanda kutoka Trillion 1.3 ya sasa hadi Trillion 2 kwa mwezi, hii itatuhakikishia sisi watanzania miradi yetu mikubwa ya kimkakati kuendelezwa na kumalizwa kabisa.

Watanzania tunataka SGR , BWAWA LA NYERERE, UMEME KILA KIJIJI, HUDUMA ZA AFYA KUBORESHWA, BARABARA ZA LAMI KILA KONA, tusipoona haya hatutakuelewa.

Dr Nchemba usiende kuingia kwenye mtego wa wafanyabiashara wakwepa kodi wanaotaka uwafutie kodi zote alafu hizo kodi uwarundikie watanzania masikini mama ntilie na machinga kama ilivyokuwa zamani unakuta mfugaji au mkulima analipa kodi 10 ili amfikishe Ng'ombe wake mnadani, hatutarajii hili kutokea.

Dr Nchemba umejionea mwenyewe ulivyotukanwa na kuchambwa sana baada ya uteuzi wako na wakwepa kodi ( Chadema) wasiolitakia mema taifa hili kwao hata miradi yote ikikwama ni sawa tu, kwa hiyo hao siyo wenzako, hata siku moja usije kusikiliza ushauri wao. Hao ni nyoka kwa taifa hili.

Dr Nchemba kwa miaka mitano iliyopita hatujaona waziri wetu wa fedha akizunguka kuombaomba Ulaya ,kwa hiyo hatutarajii kukuona kila siku upo uwanja wa ndege unaenda kutembeza bakuri.

Dr Nchemba kwa miaka mitano iliyopita tumeambiwa Tanzania ni tajiri na watanzania tunaweza , hatutarajii waziri wetu mpya uanze kuimba Tanzania ni masikini na hatujiwezi kwa lolote ,ukifanya hivyo watanzania hatutakuelewa
 
Tunataka Trioni 12 zilizokopwa na mwendazake kwenye hifadhi za jamii zirudishwe.

Madaraja na mishahara hampandishi na wastaafu mnataka muwadhulumu pia?
 
Back
Top Bottom