Ni kawaida au huyu wangu kazidi?

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,949
4,444
Jamani dada wa watu yamemkuta maswala ya bill za pombezi na msosi anatupiwa yeye na Boy friend wake alipe au washare cost.

Mwaka huu ulipoanza nilipata mchumba ambaye wakati tunakutana mimi nilikuwa nimeajiriwa na yeye akiwa bado so unakuta tulipokuwa tunatoka out I had to share cost with him ili asijione ni mzigo kwake. Mchumba kwangu namwona ni mtu wa ajabu maana anaweza akaniita sehemu na kuagiza vitu na bill inapokuja ananirushia mpira mwanzo nilidhani kwa sababu hana kazi but now amepata kazi lakini bado anafanya the same.
Kama juzi tulitoka na rafiki zake bill ilipokuja akalipa chakula na kunirushia mpira bill ya vinywaji, kisa alijua siku hiyo nimepata pesa Ofisini. Kwa shingo upande nikatoa ma kulipia vinywaji. Aunt hii sio mara ya kwanza there are time nilifiwa na ilinibidi kusafiri kwenda nyumbani (Kijijini) wakati msiba umetokwa ilikuwa kama 3 days before birthday yake.
Niliporudi kama 2 dayz baada ya siku yake huyu Mchumba akawa ananikumbushia zawadi yake bila hata huruma kwamba nilitumia pesa kusafiri kwenye msiba tena wala yeye hakunipa hata shilingi kwa ajili ya safari.

Jamani eti hii ni kawaida au huyu wangu kazidi?
Kulekule kwa Dinahicious wa Bongoradio.

Hii ya cost sharing wadau mnaionaje wale wa vyangu vyetu na chako ni chako mtakuwa upande upi?
 
THIS IS TOO MUCH, HATA MSIBA HAUJAMUINGIA KICHWANI LINADAI ZAWADI YA BESIDEI?
aaarrrggghhhhhhhh.
 
Hii inasikitisha sana. Jamaa kamuweka demu wake kakitegauchumi.......sister si "usepe", unaumia bure na mtu ambae hata hawezi sema pole ila anakimbilia zawadi.....mijitu mingine bwana yaani haina hata haya...cost sharing iwepo ila iwe na taarifa siyo unaniita nakuja harafu unasema lipa bia, kama sina ela wanivuwe nguo....nimekasilika sana kusikia jibaba linakuwa halitumii uwelewa na uwezo wake.
 
Ndo akomee hata fataki ni mchumba!!!kumbukeni kuwa kipindi hichi hakuna kulala hata wanaume nao wanachuna si unaona kama huyo kaja narafiki zake kawanyesha halafu hakulipa badala yake amelipa mchumbaye..

Huyo siyo mchumba ila ni fataki na amuache mara moja vinginevy asilalamike tena.

Alaaaaaaaa
 
Hizo si dalili nzuri fungua macho yako wazi zaidi au kwa lugha nyingine tizama kwa kutumia akili na si macho
 
Kwanza nampa pole huyo dada,nionavyo huyo jamaa anamchuna dada wa watu,kwa sababu haingii akilini wewe Fidel80 uniite mahali nikifika hapo linapokuja swala la bill nilipe au tugawane wakati ni wewe ndo umeniita,kama ni mimi nisingelipa,na pia inawezekana huyo dada amemfia sana jamaa na jamaa analielewa hilo ndo maana anamfanyia hivyo.
Jamani watu wengine sijui wakoje mtu kafiwa ndo katoka kwenye msiba unamwuliza zawadi ya siku ya kuzaliwa hii kali yaani hapo ina maana tatizo la mwenzake kufiwa halikumwingia kabisa hii inaonyesha ni jinsi gani huyu kaka yuko na huyo dada kwa sababu ya vitu na hana mapenzi ya dhati kwa mwenzake.
ushauri kwa mdada awe wazi tu amweleze jamaa kuwa hiyo tabia inamkera na aeleze vile vitu ambavyo vimekuwa vikimkwaza na aangalie jamaa atajirekebisha au ndo atalala mbele maana kuna wengine ukishamweleza kuwa hupendi kitu fulani anakasirika na kulala mbele,akikasirika aelewe kabisa kwamba hapo anapoteza muda.
 
Kwa nini tusiadapt utaratibu wa kuwa kama tukiitana baa kila mtu analipia alichotumia ili kukata mzizi wa fitna. kwa hiyo inakuwa Lipa Kadiri Ulivotumia (LIKAU)
 
Mimi sielewi, I think in a relationship you have to share the cost equally. Ndio maana ya usawa, many women expect the man to be paying more ama the man to handle the expenses. Hiyo itakuwa sio relationship but a transaction. Kosa nililoliona hapo ni yeye kukuambia ulipe bila ya kukutaarifu mapema. Lakini ninavyojua chakula ni bei ghali kuliko vinywaji na huyo b/f wako alilipia chakula wewe you paid for the drinks, whats the big deal there sister?

Hiyo ndio mitihani unayope kabla ya kuolewa, jamaa anakucheki kama wewe ni asset au liability. As couples you have to share costs, sio wewe mshahara wako uwe wako na wa jamaa uwe wenu. Nonononono sister.
 
Kwanza nampa pole huyo dada,nionavyo huyo jamaa anamchuna dada wa watu,kwa sababu haingii akilini wewe Fidel80 uniite mahali nikifika hapo linapokuja swala la bill nilipe au tugawane wakati ni wewe ndo umeniita.

Tatizo Msindima mkuitwa maeneo mnakuja na wapambe kama 2 hivi alafu mimi salio langu F lazima hapo tushare cost. Yeah ukipata mnyonge na wewe unamtumia mbona mimi nilikuwa nakamuliwa 70,000/= kwa wiki mlinicheka sana sasa na huyu yamemkuta.
 
Hilo jamaa Falaidid kweli, utapigaje mzinga demu? Kama ni cost sharing poa lakini si kila kitu, women are precious creatures handle with much tender love and care......! siwezi mlipisha demu vibia vya washikaji....
 
Hahahaha jamaa fikra zake kichwani ni kumkamua tu demu wake.
...Wapiiii?? mbona akichunwa mwanaume watu mnatulia tu? Kuna wanawake uki-date nae anakuja na rafiki zake na siku hiyo wanajifanya matawi ya juu wakiagiza u-drink eti Haeniken au Windhoek na Kuku bill ikiletwa utasikia mpe mzee halafu wanabonyezana waone utachemka au vipi??? Dada hiyo ni sawa kabisa ndio mapinduzi hayo!!!
 
Kwa nini tusiadapt utaratibu wa kuwa kama tukiitana baa kila mtu analipia alichotumia ili kukata mzizi wa fitna. kwa hiyo inakuwa Lipa Kadiri Ulivotumia (LIKAU)

mie clipi, umeniita wewe gharamika wewe!....huyu baadae wakifanikiwa kuoana hata ndani kila kitu kitamuhusu, mwanaume unavyompeleka ndivyo anavyozoea.....kazi kubwa mbeleni...
 
mie clipi, umeniita wewe gharamika wewe!....huyu baadae wakifanikiwa kuoana hata ndani kila kitu kitamuhusu, mwanaume unavyompeleka ndivyo anavyozoea.....kazi kubwa mbeleni...

Hahahaha nitakuita siku moja bar nakupombesha ile mbaya.....halafu utaamka asubuhi umechooooka....
 
mie clipi, umeniita wewe gharamika wewe!....huyu baadae wakifanikiwa kuoana hata ndani kila kitu kitamuhusu, mwanaume unavyompeleka ndivyo anavyozoea.....kazi kubwa mbeleni...

woke woke, weekend wapi mrs mi ndo nakutoa...sema mwenyewe..tuanzie kwenye mtura, kisha kidogo sowetu afu tukamalizie na dansi,,,,eh lakini na matongee napo hatujapapitiamuda muda..kila kitu leo mimi kuanzia wesevinywaji na nyamchom:p
 
Hahahaha nitakuita siku moja bar nakupombesha ile mbaya.....halafu utaamka asubuhi umechooooka....

Mpwa kuwa makini mke wa mtu huyo we mpombeshe alafu ukamatwe ugoni sijui nani atakunasua.
 
Tatizo Msindima mkuitwa maeneo mnakuja na wapambe kama 2 hivi alafu mimi salio langu F lazima hapo tushare cost. Yeah ukipata mnyonge na wewe unamtumia mbona mimi nilikuwa nakamuliwa 70,000/= kwa wiki mlinicheka sana sasa na huyu yamemkuta.


huyo mwanamke wa dizani hiyo hayupo serious na relation, so kila mkikaa mpo na shoga zake, sasa nyie muda wenu wa kuongea yanayowahusu ni kitandani tu? kuna wakati anaweza kweli akaja na frnd wake na wewe pia wakati mwingine ukawa na frnd wako, yani kampani tu lakini icwe sheria kukokotana....
 
woke woke, weekend wapi mrs mi ndo nakutoa...sema mwenyewe..tuanzie kwenye mtura, kisha kidogo soweto afu tukamalizie na dansi,,,,eh lakini na matongee napo hatujapapitiamuda muda..kila kitu leo mimi kuanzia wesevinywaji na nyamchom:p


haaa mr upo kwenye huu mji? j5 naingia hapo tutafutane.......
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom