Real Patriotist
JF-Expert Member
- Feb 6, 2016
- 284
- 687
Hii nchi ya ajabu sana miradi yote ya maji ni ufadhili wa wahisani kama India lakini et ndege tunanunua kwa pesa zetu, huu si ni uduwanzi kabisa.
"Yule mbunge wao alisemaga maji sio kipau mbele chake kwenye uongozi wake"Nitashangaa mkimpatia Tena Kura za ubunge.
Na ni janga la taifaNi laana mkuu
Iyo avata itazame kwa jicho la tatu ndyo utaelewa kwanini ipo apo.Wewe acha kutuchota akili hapa, Avatar yako inaonyesha unamhusudu Huyo unayemponda, Halafu unajifanya Bwege ili usikilizie siyo.
Bukoba yenyew mji haunaga stendi Zaid ya kichochoro cha matope na soko kuu la mabati.Kumbe Victorie nawe upo kwenye jiji hili! Huku kwetu Bwiru, maji, barabara usiseme. Lakini ukienda mikoa mingine wanaamini huku Kanda ya Ziwa tunapendelewa.
Jamani huku nako hamna kitu. Labda hizo teuzi za upendeleo ambazo nazo zinagusa watu wangapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uongo wewe. Bulale nyanembe sijui kigoto uko ndyo hata maji ya bomba hawajui.Buhongwa mtakuwa washirikina mbona Sahwa, Bulale na Nyanembe maji yapo ya kutosha?
Nadhani hili nalo lililetwa na wakoloniKachoteni ziwani acha lawama zenu
Huyo ni mdogo wake na ketambi, hayo ndiyo majibu ya serikali kwa wananchi, kwa akili hii kwa nini wasimchague mpinzani?Kachote na wewe
Too Sad yaani Buhongwa tunaamka tunaona Ziwa huyoooo.Eti halafu kuna shida ya maji. Stupid policies.Halafu kutwa kunyooshea vidole mabeberu. Hivi mabeberu wanazuia msijenge mabomba na kuwa na huduma ya maji yasiyokatika katika ?
Unaongea mara moja kwa wiki, nakaa Buswelu manispaa ya Ilemela na sijapata maji ya bomba zaidi ya miezi mitatu.Mimi ni mkazi wa Kanda ya Ziwa ila tunachangamoto kubwa ya maji.
Cha kwanza awamu hii gharama ya maji imepanda sana na maji yenyewe ni ya shida.
Hebu imagine ziwa lipo within 30 km ila maji mnapewa kwa mgao. Kunamaeneo mwanza hii maji yanapatikana usiku tu. Sasa afadhali na uko. Kuna pengine maji yanafunguliwa mara moja kwa wiki.
Hawa wabunge tuliochagua ndyo bure kabisa. Mbali na maji ila barabara vumbi ndyo hovyo kabisa.
Umekaribia uchaguzi ndyo wamezikwangua kihuni huni tu mvua imepiga mara moja tu kwisha mabonde kuinama kama kawaida.
Sasa ni hivi, kura mtapigiwa na mandege mliyonunua.
Wasiofika Mwanza wanaweza kushangaa km labda tunasingizia......Hapa chato Hakuna maji ya bomba,watu wanachota maji ya matumizi kwenye ziwa Victoria .Katoro mjini ambayo upo buserere wilaya ya chato ,Hakuna maji ya bomba watu wanachota na kunywa maji ya visima vifupi naziwa Victoria lipo KMS chache tu,Ila hakuna maji.
Sembuse mwanza jiji kubwa. Kupiga Kura mwaka huu lazima mtanzania ujithadhimini Sana kabla hujapiga Kura , tunadanganywa na miradi mikubwa Ila wananchi wanateseka Sana kuanzia chato Hadi mtwara.
Watu wa Mwanza amkeni acheni kuendekeza ccm, huu mfumo ni wa zamani kwa ajili ya kupigania uhuru enzi za wakoloni. Watu wa K’Njaro walishaachana na ccm tangu 1995 na mambo yao safi tu. Tuondokane na mfumo ccm wakati ni huu.Yaani ni kero acha tu.
Buswelu ipo within 30 km from lake victoria north, west na est imezungukwa na ziwa victoriaUnaongea mara moja kwa wiki, nakaa Buswelu manispaa ya Ilemela na sijapata maji ya bomba zaidi ya miezi mitatu.
Siwezi kuwapa kura CCM hata nikiwa mgonjwa wa akili
Kesho nakuja halo chadema kuangalia ndondo LA mashujaa vs KishiriMimi niko kata ya Kishili, naingia mwezi wa nne sasa bomba la maji la nyumbani halijatoa maji. Vyoo vya ndani bila huduma ya maji kweli!!! MWAUWASA wamenitumia bill ya July na ninashangaa kwa huduma ipi? Kipindi Corona inaanza March sisi huku tulikuwa na shida na maji ya kunawa. Kweli ulimwengu wa kati Afrika ni shiiiiidaaaa!!!