JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
salamu wanabodi!
Tanzania ina wafanyakazi wa umma wa ajabu sana.Juzijuzi tumeshuhudia mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa JULIUS KAMBARAGE NYERERE akimdanganya Rais mchana kweupe bila hata chembe ya woga! alivaa ujasiri wa ajabu sana ni kama mtu aliye tumwa na genge la wahalifu walio mtishia asipo fanya vile watamuua.Tumefika mahali pabaya sana kama Taifa.
Kinacho nishangaza mimi siyo hicho bali yaliyo fuata baada ya tukio lile.Kitendo cha kumdanganya kiongozi mkuu wa Nchi ni kibaya na hakivumiliki.Binafsi nilitegemea kwamba pamoja na kwamba Rais hakuwafukuza kazi, ilitakiwa mamlaka za uwanja wa Kimataifa wa JKN wangewafukuza kazi wale watumishi mara moja.wameliaibisha Taifa.Kama wao hawana mamlaka hayo, basi nilitegemea katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi angechukua hatua kali dhidi yao haraka sana. Lakini hadi leo kimya kimetamalaki.
Rais alikuwa sahihi kutokuwafukuza kazi watumishi wale kwasababu wako ngazi za chini sana kiutumishi, ni sawa na kutumia LMG kuua mende! ili kuonesha uwajibikaji wa pamoja nilitegemea hao wenye mamlaka nao wawafukuze kazi.Kwa mtazamo wa haraka wale hawajui kazi yao inatakiwa kufanywa vipi na ndio maana hawana taarifa sahihi za vitendea kazi vyao.
Jambo lingine linalo nishangaza mimi ni kuona watu waliofanya mauaji ya watu saba kule Sengerema mpaka leo hawaja kamatwa.Ni ufanyaji kazi wa kimazoea! Binafsi nilitegemea polisi makao makuu wangeongeza wapelelezi maradufu ili wauaji wapatikane mara moja, lakini mpaka leo hii hakuna hata mmoja aliyetiwa mbaroni. Hivi, najiuliza ilikuwaje alipo uawa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Sabas, jeshi la polisi makao makuu walituma kikosi kwenda kuongeza nguvu ya kipelelezi na kuwakamata wahusika wote ndani ya muda mfupi lakini leo hii watu saba wameuawa kikatili lakini hatuoni nguvu kama ile iliyo tumika kuwasaka wauaji wa kamanda Liberatus Sabas!
Kuna udhaifu mkubwa sana wa namna watumishi wa umma wanavyo fanyakazi zao.Ni ufanyaji kazi wa kimazoea tu ilimradi siku zina songa mbele na watu wana pata mishahara yao basi.wewe jiulize mauaji ya wale watu saba yangekuwa yametokea marekani au Nchi nyingine ya ulaya, shughuli yake ingekuwa balaa!!
Kuna wakati nawaza kuwa ni bora Magufuli afukuze watumishi wa umma wote afanye usajili upya maana hawa waliopo ni kama wana muombea ashindwe kazi ili waendelee na maisha ya kuifilisi Nchi kila mtu na mahali alipo.