EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,112
Ndugu zangu leo nimeona ni wakati muafaka jioni hii nizungumzie neno “Uzalendo”. Neno hili limeweza kutumiwa vibaya kiasi cha kuathiri kwa kiasi kikubwa ufahamu wa wananchi wetu (wake kwa waume). Ninavyofahamu Uzalendo ni mapenzi mema ya dhati mtu anakuwa nayo kwa taifa au nchi yake. Na mzalendo ni mtu anayejivunia nchi yake na rasilimali zake na anapoona baya juu ya nchi yake anakuwa yuko tayari kutetea, kupaza sauti, kukemea na kuonya ili kulinda heshima ya kile anachojivunia kisiingie doa au uchafu.
Mzalendo anajitoa nafsi yake na yuko tayari kuitetea nchi yake iwe pale inapostahili kiheshima na kimaendeleo. Lakini nashangaa sana kumekuwa na hurka kwamba yule anayetetea heshima na maendeleo ya nchi yake si mzalendo. Ukikemea kidogo au ukaongea ukweli Fulani basi unashutumiwa wewe si Mzalendo. Nimekaa na kujiuliza sana kwanini watu wanazadhi kukaa kimya au kutokukosoa ni Uzalendo.
Lakini shida inapokuja pale mzalendo anapotetea au kupaza sauti na kughazibika juu ya uchafu au ubadhilifu juu ya inchi yake anayoipenda basi anaambiwa huyu si mzalendo. Kikubwa nachojua Mzalendo ni msema kweli daima na usipojua kusema kweli basi wewe si mzalendo bali ni mnafiki. Mnafiki hawezi kuwa mzalendo hata siku moja kwenye dunia hii. Hivyo wanabodi naomba tujiulize wangapi humu wanaochangia kwenye JF ni wazalendo?
Kama kuwa Mzalendo itakuwa ni kutumbukiza kichwa kwenye mchanga na kudharau ukweli halisi yaani niwe Mnafiki basi mimi kwenye wazalendo nisihesabiwe. Lakini kama kuwa Mzalendo ni kusema kweli na kuhamsha hamasa ya ushindani ambayo itatufanya tuyakabili mapungufu yetu ili tutembee kifua mbele tukijivunia nchi yetu basi na mimi kwenye wazalendo nihesabiwe. Mwenye mapenzi mema na nchi yake hakai kimya na anayekaa kimya basi uraia wake uchunguzwe mara mbili.
Mzalendo hatamki tu mdomoni mimi Mzalendoni matendo yake pia yanaonyesha ni mtu wa namna gani. Mzalendo anayosema siku zote yanatoka moyoni na kwa mapenzi mema ya nchi yake. Lakini viongozi hususani wabunge nimeona mara nyingi wanatumia msemo huu “nalisema hili kutoka moyoni kabisa…” kiongozi kama huyu si Mzalendo.
Kwa mtazamo wangu kuna viongozi wengi sana wa inchi hii uraia wao unahitaji uchunguzwe.
Naomba mtazamo wenu ndugu zangu juu ya Uzalendo ni nini?