Ni kama Bahati vile ila unaweza sema Mungu kampendelea Rais Samia

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Amani iwe nanyi wadau,

Huko soko la dunia hapatoshi! Bei ya Mafuta na Gesi inazidi kupanda kwa Kiwango cha kutisha.

Haya yanatokea huku Ulaya na Marekani kukiwa na uhaba wa bidhaa hii adhimu kiasi kupelekea Makampuni ya Gesi na Mafuta kuamka mbio kutoka usingizini na kuanza kufufua zile fursa walizokuwa wamezitupa kando kwa miaka karibu 6 mpaka 7!

Ulaya walipokuwa wanategemea nishati mbadala sasa wameona hawawezi tena kwenda bila gesi! Baridi inayoongezeka Ulaya inafanya Gesi kuhitajika zaidi kuliko bidhaa zingine Kwa ajiri ya kupata nishati!

Ndo mana hivi Karibuni Makampuni Makubwa yameanza kujileta Tanzania! Wiki mbili zilizopita Makampuni ya Exon Mobil yalifanya kikao na Waziri Makamba.

Juzi hapa Mtendaji Mkuu wa Kampuni kubwa ya Gesi na Mafuta ya Shell ya Uholanzi kafanya kikao na Rais Samia.

Vikao hivi bila shaka ni vya makampuni haya kujaribu kupata nafasi ili yapewe nafasi ya kufanya biashara hii Tanzania. Kusema kweli huu ni upepo mzuri kwa Mama Samia maana haya yanatokea chini ya uongozi wake!

Rais Samia akikaa vizuri kwenye Mazungumzo na watu hawa na tukaingia mikataba mizuri nadiliki kusema Mradi huu wa LNG ndo utakuwa mradi wa kipekee na faida zaidi kwa Tanzania na Watanzania kuliko mradi wowote uliowai na utakaowai kuja kufanywa Tanzania.

Dunia inahitaji Kweli Gesi na wako kwenye panic state ya kupata fursa ya kuchimba na kuuza Gesi. Tanzania ikicheza vizuri hapa , hata Tozo za simu tutaachana nazo.

Wito wangu kwa Mama Samia! Hii ni kete adhimu, una bahati sana, itumie vizuri hii nafasi na hutasahaulika kwa Watanzania vizazi na vizazi!​

F32927E8-CE8C-40D0-9BB4-B73581B19CBB.jpeg
 
Sababu ya kutoka kalemani ni hili la gesi bila shaka.
Warusi wanaradi wao wa steam 1 na 2 ambao utawawezesha kuuza gesi ulaya.
 
Unachukua muda mrefu kivipi?
Mradi wa lng wa Angola, ujenzi ulianza 2008 na ukamalizika 2012. Uzalishaji ukaanza 2013.

Kwa hiyo piga mahesabu kama mpaka hivi tunavyozungumza majadiliano hayajakamilika, unadhani ujenzi utaanza na kuisha lini? Na uzalishaji utaanza lini?
 
..mradi wa lng wa Angola, ujenzi ulianza 2008 na ukamalizika 2012. Uzalishaji ukaanza 2013.

..kwa hiyo piga mahesabu kama mpaka hivi tunavyozungumza majadiliano hayajakamilika, unadhani ujenzi utaanza na kuisha lini? Na uzalishaji utaanza lini?
Kwani shida iko wapi? Ikichukua miaka iyo?
 
Naunga mkono hoja 100/100.

Keyword: mikataba
Mikataba ndo kila kitu

Tuandae mikataba yetu na namna tunavyotaka biashara hii iendeshwe huku tukishiriki kwenye sehemu zote nyeti!

Hapo ndo tutahakikisha nchi yetu inanufaika Kweli!

Kwenye hili tunaweza kuwa nchi ya mfano Africa na hata duniani kwa kuingia mikataba Bora inayonufaisha watanzania na Taifa kwa ujumla
 
Back
Top Bottom