Ni kaburi la CCM au CHADEMA?

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,274
9,911
NATAKA kusema neno moja. Ni hivi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitakufa. Lakini hakifi leo, wala hakitakufa kwa sababu ya kumvua vyeo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na wenzake.

Kitakufa siku moja kama vyama vingine vyote vitakavyokufa, kwa sababu kila kilichoanza kina mwisho wake.
Kitakufa wakati wake utakapowadia. Si sasa. Si leo. Na hakitakufa kabla Watanzania hawajashuhudia kifo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Niamini.
Zaidi ya hayo, hakitakufa kwa sababu ya makundi ya wana CCM wanaojipanga nchi nzima kuzomea, kuchochea mgororo, kutisha viongozi wa CHADEMA na kubeza uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho.

Badala yake, kwa kufanya uamuzi mgumu, kwa kugusa baadhi ya wanachama na viongozi wanaodhaniwa kuwa hawagusiki; kwa kufanya kile ambacho CCM wamekuwa wanashindwa kufanya, CHADEMA kimejiweka katika mazingira mapya ya kukua na kukomaa.
Kinaonyesha kuwa sasa kimekuwa taasisi. Walio tayari kufanya kazi kitaasisi wataendelea kufanya kazi. Waliojiunga na chama kufuata watu, wataondoka na watu hao. Waliofuata sera watabaki. Chama kitapona.

CCM ilipokuwa bado imara iliwahi kufanya uamuzi mgumu. Katika kutetea kile ambacho uongozi wa chama uliona ni msimamo wao kuhusu Muungano, chama kilimfukuza Makamu wa Rais, Aboud Jumbe na Waziri Kiongozi, Seif Shariff Hamad.
Uzito na ukweli wa hoja zao ni jambo moja; na msimamo wa chama ni jambo jingine. Chama kilitetea msimamo wake. Viongozi wakubwa wa ngazi hizo wakaanguka, chama kikapona.

CCM legelege ya sasa haiwezi kufukuza hata wale inaowatuhumu kwa makosa makubwa na kuwashambulia hadharani. Inawaogopa.
Ndiyo maana kelele za kuvua magamba zilipopamba moto, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, alikejeli harakati za wenzake akisema, “gamba limekwama kiunoni. Mwenye uwezo wa kulivua aje na shoka.”
Mwaka umepita sasa, gamba la Chenge limewashinda Rais Jakaya Kikwete, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, na mashabiki wao.
Kwa hiyo haishangazi kwamba CHADEMA inapochukua hatua ndogo tu ya kubadilisha watu vyeo kwa sababu ya kukosa imani nao, wanaokerwa zaidi na hatua hiyo ni wana CCM.

Ndio wanaohaha nchi nzima wakitangaza kila kona “CHADEMA kinakufa, CHADEMA kinakufa.” Kisa, eti Kamati Kuu imemvua Zitto vyeo. Kwani yeye alivipataje? Si wale wale waliompatia vyeo ndio wameamua kumwondolea vyeo hivyo?
Na tangu lini CCM wakawa na huruma kwa CHADEMA? Iweje leo ‘CHADEMA inakufa’ halafu wanaoumia ni wana CCM?
Kwanini CCM wanasikitishwa na ‘kifo’ cha CHADEMA? Kuna jambo. Wenye akili wameshaligundua.
Iweje wanaoandaa magenge ya kuzomea viongozi wa CHADEMA na kubeza uamuzi wa Kamati Kuu ni baadhi ya wanachama wa zamani wa CHADEMA waliokimbilia CCM?

Wanatuma ujumbe gani kwa Watanzania? Zaidi ya hayo, mbona hawa wamenyang’anywa vyeo tu, tayari propaganda za udini na ukabila ndo zinaibuka tena?
Ni dini gani inayoagiza kwamba cheo ni haki ya kuzaliwa ambayo mtu akishapewa hapaswi kunyang’anywa, hata ikithibitika kwamba wenzake hawana imani naye?
CCM na makapi yao sasa wanahaha nchi nzima kuhubiri udini na ukabila. Huu nimeuita ujinga. Ni ugonjwa wa akili. Ni kichaa kama vingine.
Hivi CHADEMA ilipovunja uongozi wa chama Mkoa wa Mwanza ilikuwa inatetea dini na makabila?

Ilipofukuza madiwani wanne Arusha ilikuwa inapambana na Uislamu? Ilipomvua cheo Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo ilikuwa inajadili dini na makabila yao?
Ni lini tumeanza kuficha udhaifu wetu katika makabila yetu na imani zetu za kidini? Kwa faida ya nani?

Ndiyo! Ipo siku CHADEMA itakufa. Lakini kwa mbinu hizi za CCM ya sasa, CHADEMA itazidi kushamiri. Jipeni muda, mtaelewa maneno yangu.
Wanaotaka kutumia mwanya huu kudhoofisha chama hiki wanapoteza muda. Hawataweza. Chama kimeshawazidi nguvu. Kimewazidi kimo.
Nakumbuka miaka kama 15 iliyopita, wana CCM walikuwa wanamwaga sifa kwa CHADEMA, wakisema ni chama cha watu wastaarabu, hakina fujo wala migogoro. Walikiona ni chama cha wastaafu na mabepari wenye pesa ambao hawana papara.

Leo wanakiona ni chama chenye fujo. Wamefikia hatua ya kukizushia tuhuma za ugaidi. Sababu ni moja. Wakati ule, CHADEMA hakikuwa tishio kwa chama tawala.
Kilipewa sifa hizo kwa kuwa kilikuwa kinaonekana ni mateka wa mfumo unaotawala.
Kilikuwa chama kwa sababu tu kina usajili.
Lakini hakikuwa kinaonyesha dalili zozote za kutaka au kukaribia kushika dola. Ustaarabu wa CHADEMA wa enzi zile ilikuwa silaha ya nyongeza ya CCM.
Leo CHADEMA ndicho chama pekee kinachokua kwa kasi hapa nchini. Ndicho kinachotetemesha wakubwa katika mijadala bungeni.
Ndicho kinachoongoza mapambano ya wanyonge dhidi ya watawala. Ndilo tishio kuu la serikali ya sasa.
Kwa hali ya sasa ya kisiasa, katika kutapatapa kukubalika na kubaki madarakani, CCM inajua kuwa haitapata kuungwa mkono na watu kwa mikutano ya hadhara au sarakasi zozote za kisiasa.

Inajua kuwa wananchi wamechoka, wanataka mabadiliko. Njia ya mabadiliko inayotazamwa sasa ni CHADEMA.
Watawala wamebaki na mambo mawili ya kufanya. Ya kwanza ni kupenyeza ‘virusi’ ndani ya CHADEMA. Ya pili ni kupenyeza rupia ndani ya CHADEMA katika ngazi mbalimbali.

Kinachowakera watawala ni kwamba tayari CHADEMA imeshaanza kugundua baadhi ya hatua zinazochukuliwa na CCM.
Kinachokera zaidi ni kwamba CHADEMA inaweza kuthubutu kuchukua hatua, na kupambana na matokeo. Hili nalo ni chukizo kwa CCM.
Kimsingi, CCM inatamani kuua CHADEMA, lakini haijajipanga vema. Haijui jinsi ya kuiua. Ijipange upya.
Watanzania wanajua kipi kinaelekea kaburini kati ya CCM na CHADEMA. Waachwe waamue.
 
Mkuu hawa maccm wasikuumize kichwa kabisa,acha wafanye hujuma zao zidi ya slaa.

acha wafanye fitna zao zidi ya mbowe

acha wafanye uzandiki wao zidi ya chadema

acha wafanye unafiki wao zidi ya watanzani walioamua kujiunga na vyama vya upinzani

Ipo siku haya wanayoyafanya leo kwa chadema nao watafanyiwa kwa njia tofauti kwani "what goes around,comes back around
 
Mkuu hawa maccm wasikuumize kichwa kabisa,acha wafanye hujuma zao zidi ya slaa.

acha wafanye fitna zao zidi ya mbowe

acha wafanye uzandiki wao zidi ya chadema

acha wafanye unafiki wao zidi ya watanzani walioamua kujiunga na vyama vya upinzani

Ipo siku haya wanayoyafanya leo kwa chadema nao watafanyiwa kwa njia tofauti kwani "what goes around,comes back around

Umenena tena mwisho wao utakuwa mbaya sana
 
Zitto angekuwa mchaga kama Lema angesamehewa, hamuwezi kwepa hili, kwa nini Lema hakusibiri vikao kumshambulia Zitto?hamuwezi kwepa hili wakabila wakubwa nyie. Wekeni mkurugenzi wa fedha asiye mchaga tuone kama mna uwezo!!!!
 
Zitto angekuwa mchaga kama Lema angesamehewa, hamuwezi kwepa hili, kwa nini Lema hakusibiri vikao kumshambulia Zitto?hamuwezi kwepa hili wakabila wakubwa nyie. Wekeni mkurugenzi wa fedha asiye mchaga tuone kama mna uwezo!!!!

Utasubiri sana mkuu na uzuri tumeshawashitukia mchujueni Zitto wenu asiye mchanga mkae naye huko Lumumba kwenu mtuachie Lema wetu mchaga.

Najua sasa hivi hamna hoja mtakimbilia ukabila na udini ambao hamuwezi ngooo kwani ni old style imepitwa na wakati .
 
Back
Top Bottom