Ni jukumu letu, si la Dr Slaa peke yake! Tuanzie hapa, tuanze sasa

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,403
31,376
Mwaka wa uchaguzi umefika, wakati tuliousubiri kwa miaka 5 kuwatia adabu wale wasiotusikiliza, wale wasiojali maisha yetu na wale wasiojali Tanganyika ya kesho ndio huu. Hiki ni kizazi kinachojinasibu kwa teknolojia na maendeleo, lakini kwa kudhani kuwa maendeleo ni internet/ipod n.k kizazi kimejivua jukumu la ukombozi wa nchi toka lindi la umasikini. Sasa watu hukaa mbele ya kompyuta zao kusubiri kusikia nini Dr Slaa au Selelii watafanya.

Hatuwezi kuikomboa nchi kwa fikra za kukejeliana badala ya kujibu au kuandika hoja zenye mashiko na nguvu. Hatuwezi kuiokomboa nchi kama tumejikita kwenye mawazo ya kuwakosoa wale wanaojitahidi japo kwa uchache wao. Hatuwezi kuiokomboa nchi kama tutawaendekeza wale wanaotutoa kwenye hoja kwa kuchomeka ubinfsi.

Kampeni zimeanza, hatuna sababu ya kusubiri Dr Slaa atafanya nini, sisi tunatakiwa tumwambie afanye nini ili kufikia ukombozi. Sisi ndio injini ya Slaa na sio kinyume chake. Tunatakiwa tujawe na jaziba na chachu ya ukombozi ili kila asubuhi Dr Slaa ajue ana watu wanamdai, ana deni! Sio muda wa kusikiliza Dr kasema nini bali ni wa kumwambia Dr tuelekee huku! Hakuna nchi, jamii au taifa lililokombolewa na mtu mmoja, ni nguvu ya umma, na umma ni sisi.

Kampeni zimeanza, na tunashuhudia wananchi wakiimbishwa na kuchezeshwa nyimbo wasizozijua lakini wanaziimba vizuri. CCM ni nambari moja, fungua njia CCM ipite n.k.

Wakiambiwa ilani imetekelezeka wanapiga makofi ili wasije nyimwa kofia au khanga. Sio kuwa hawajui udanganyifu bali umasikini na kukosa kitu mbadala ndio kikwazo.

Tuanze kampeni ya kuisadia nchi bila magari au helikopta! tuanzie humu JF. Tuanze na wewe unayesoma, chapisha [print] picha hizo na umuonyeshe, Mkeo, Shemejio, Baba, Mama,hata Mama mkwe kisha muulize maswali haya kwa utulivu bila ushabiki!
1. Ilani ya uchaguzi kuhusu elimu imetekelezeka kivipi kwa kuangali hizo shule hapo chini?
2. Vipi ccm inunue magari 200 ishindwe kujenga shule hiyo hapo chini?
3. waulizeni, je hao watoto ni sehemu ya nambari one ya ccm ?
4. Je hao watoto wataweza kununua ma vx au watabaki kucheza ngoma kama wazazi wao?
5. Je, zile kompyuta wanazoahidiwa wananchi zitawekwa wapi kama watoto wamekaa
juu ya mawe?
6. Waulizeni wanapoimba na kucheza ngoma, ni ushindi upi wanaosherehekea, kutojenge wa shule nzuri kama zile za ''academy'' au kuwaona watoto wao wamekaa juu ya mawe kama mama zao wanapokuwa wanawapikia!!!!.

Pelekeni ujumbe bila ghadhabu wala munkari, na mwisho muwaambie je wapo tayari kuendelea na hali hii iliyodumu miaka 50!! au wapo tayari kwa maamuzi magumu dhidi ya mazoea lakini yenye tija kwa vizazi vijavyo?

Ili kujenga uthubutu kwako kwanza kabla ya mwenzako, mwambie Mama Mkwe '' Chagua wabunge chadema, chagua Slaa'' ukifanikiwa au la! nenda kwa jirani naye mpe dozi! usikate tamaa kwasababu mafanikio hayaji katika sahani ya dhahabu! yanaambatana na jasho.
 
Nguruvi umetoa mchango mzuri sana. Ni kweli wakati wa ukombozi toka ukiritimba wa wa madaraka waCCM umefika, lakini si Dr Slaa peke yake anahusika. Lazima kila mmoja wetu aweke nguvu zake. Hiyo kampeni ya nyumba hadi nyumba ni sawa kabisa.
Kila mtu ashughulike mtaani kwake. Asikae kumsubiri Dr Slaa tu.
 
hizo picha ziko wapi?
Zimejaa tele hapa JF.
Fanya homework yako uzitafute. Watoto wakiwa wamekaa chini ya miti, juu ya mawe, kwenye udongo huko mashuleni. Na wakina mama wakiwa wamerundikana kwenye wodi zakuzalia na waliolala kwenye vitanda visivyo na godoro ila kama za katani.
 
unachoongea ni sahihi lakini kuna ugumu sana kwenye mambo mbalimbali

CCM inamatawi active katika mikoa, wilaya, tarafa, kata, na vijiji vyote toka enzi za mwalimu, kuelimisha hawa watu wakuelewe wabadilishe mind itachukua muda.
vyama vya upinzani havina matawi sehemu kubwa ya nchi, kama tulivyoona kuwa sehemu nyingi hakuna madiwani wala wabunge wa upinzani. na hata kama matawi yapo yanakuwa active wakati wa uchaguzi tu.
nilimsikia Dr. Mwakyembe asubuhi leo hii alisema kuwa pale Kyela ofisi za vyama vya upinzani hususani tawi la CHADEMA limefunguliwa hivi karibuni kwa ajiri ya uchaguzi.
Hivyo hayo unayoongea inatakiwa iwe plan ya muda mrefu, baada ya uchaguzi vyama hivi viendelee kujiimarisha na si kusubili uchaguzi ndiyo kuna kuwa na kelele nyingi!!!!
Magazeti leo yanaripoti kuwa tayari 50% ya madiwani tayari wapepita bila kupingwa na ni wa CCM na pia CHADEMA imesimamisha 40% tu ya wabunge wote na hatujui watapita wangapi? hivyo utaona kazi kubwa inahitajika mbeleni
 
Mawazo maazuri sana.

Mimi nimeshaanza kila siku ni lazima niongee na zaidi ya watu wa tano kuhusu ushiriki wao katika uchaguzi mwaka huu hasa kukipigia CHADEMA na Dr SLAA.

Huwa naibua mjadala sehemu mbalimbali ili watu wajadili mambo muhimu ya uchaguzi wa mwaka huu
 
Mhh! Kazi kwelikweli! Dr Slaa kupita ni kazi (kwa mtazamo wangu)! Tatizo la vyama vya upinzani havitaki kuungana, na ukiangalia statistics utaona kabisa kushinda kwa utengano huo wa vyama vya siasa ni kazi ngumu. Wapinzani waache ubinafsi, next time waungane mapema. Hizi tamaa na uchu wa ruzuku na madaraka ya kutaka kuhodhi vyama vya siasa kwa faida binafsi kuliko kuwatumikia wananchi ndo vifanyavyo vyama vya upinzani visiungane au kukubali kushirikiana. Kama ilivyosemwa, "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu."

Inabidi kama vyama vya upinzani vinataka ushindi vikubali kuungana, kuweka tofauti zao pembeni, viongozi wake wakubali kuachia nafasi zao na kuwapa wapinzani wanao kubalika na kuwa tayari kuweka maslahi ya Watanzania mbele. Wenye moyo huo kwa viongozi wa upinzani ni wachache (kama akina Dr Slaa) kuliko tunavyofikiria.

Hivi jiulize kwanini baadhi ya viongozi wa upinzani hawataki kuachia uongozi kuwapisha viongozi wa wapinzani wengine wanaoweza zaidi kwa maslahi ya Watanzania wote pindi wanapoambiwa waungane kwa maslahi ya Watanzania? Jibu ni kwamba wanatetea maslahi yao binafsi na si ya Watanzania kwa sababu kama hafaidiki na wanajiua kabisa mioyoni mwao kwamba kiongozi fulani tukimpa anafaa lakini wanaendelea kung'ang'ania, je hapo wanang'ang'ania nini? Sasa kama wenyewe kwa wenyewe hawaaminiani je wapiga kura na watawaamini? Itakuwa ngumu kwani wanawachanganywa (wapiga kura) katika viongozi wa upinzani wamwamini nani (hapo kura huanza kugawanyika, nyingine kwa Lipumba, nyingine kwa Slaa, n.k)?

Pia kampeni hazianzi karibu na uchaguzi! Wapinzani wekezeni miaka mitano kabla ya uchaguzi! Dr Slaa una nafasi ya kujifunza hilo. Kwa kuanzia (Dr Slaa) watie kashkash CCM, pata ushindi hata wa asilimia nyingi kuliko za Mrema enzi zile, then 2015 ukianza kuwekeza tangu wakati huu urais ni wako. Waunganishe wapinzani, ongeza wanachama, tangaza mapema kuwa utagombea (isiwe late kama mwaka huu) ili watu wajiandikishe kupiga kura kwa ajili yako (kwani mwaka huu kuna watu hawakujiandikisha kwani hawakujua kama Slaa atagombea urais hivyo walijua CCM na JK wake itashinda tu, sasa kwanini wajisumbue?).

Ila kwa kuwa umeamua kugombea, kura za waliochoshwa na maovu na uzembe wa baadhi ya waliopo madarakani utazipata na kampeni tutakupigia kwa kuwa we ni mkombozi wa ukweli wa wanyonge. Nna imani hata baadhi ya wana CCM wenyewe (wasioshiriki kwenye maovu, wanaotaka kukomeshwa uozo unaoendelea ndani ya chama na serikali na wanaojua kuchambua pumba na mchele) watakupigia na pia wasiokuwa CCM tutajitahidi kukupigia debe.
 
Back
Top Bottom