Ni JK Forum si Amani Forum

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
Absalom Kibanda

HEKAHEKA za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu zimepamba moto, na tayari vituko kadha wa kadha vya kisiasa vimeshaanza kuonekana kadiri miezi na siku za kuelekea Oktoba 31 zinavyozidi kujongea.

Matendo na kauli kutoka kwa wanasiasa wa makundi mbalimbali yanayoshereheshwa na matukio ya kutia hamasa na wakati mwingine kukera kama si kushangaza, ni mambo yanayoonekana kuwa ya kawaida kusikika wakati huu taifa linapojiandaa kuwachagua Rais wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, wabunge, wawakilishi na madiwani.

Katika kipindi cha wiki moja au mbili tu zilizopita, taifa limeshuhudia matukio kadha wa kadha mazito kuhusu mustakabali wa nchi hii, ambayo ukiyaangalia utaona moja kwa moja mwelekeo wake unatuongoza kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi huo mkuu.

Ni katika kipindi hiki cha wiki moja, tumemsikia Rais Jakaya Kikwete kwa nyakati mbili tofauti, kwanza akiwa Mwanza na baadaye akizungumza kwa utaratibu aliojiwekea wa kulihutubia taifa kila mwishoni mwa mwezi, akionyesha kukerwa na kukemea tatizo la rushwa na lile la matumizi mabaya ya fedha wakati huu tunapoelekea katika mshikemshike wa uchaguzi mkuu.

Ni wazi kwamba akiwa kiongozi mkuu mwenye dhamana kubwa pengine kuliko mwanasiasa au mtu mwingine yeyote hapa nchini kwa wakati huu, Kikwete anawajibika kiuongozi, kivisheni na kimaadili kutoa matamshi ya namna hiyo yenye kutoa mwongozo na kuonyesha njia sahihi ambayo taifa linapaswa kupita wakati huu tunapojiandaa kwa ajili ya tukio kubwa la kihistoria.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Kikwete imepokewa kwa hisia tofauti na wadadisi mbalimbali wa mambo, ambao baadhi yao wameonyesha kuiunga mkono na kummwagia sifa, huku wengine wakiitilia shaka na kuibuka na maswali mengi moja kati yao likiwa ni lile linalohoji, iwapo rais ameitoa kwa moyo wa dhati au kwa sababu tu ya kutaka kuonekana akitimiza wajibu wa kimamlaka unaomtaka aseme lolote jema hata kama atafanya hivyo pasipo kumaanisha kile asemacho.

Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana wako waliotafsiri kauli hii ya Kikwete kuwa inayotoa mwelekeo sahihi wa huko tuendako, huku wengine wakiichukulia kuwa ni vitisho visivyo na maana ambavyo kiongozi huyo amekuwa na utamaduni wa kuvitoa kila mara, akijua kwa kufanya hivyo anatimiza wajibu wake wa msingi wa kiuongozi wa kuonyesha njia.

Pasipo kujali ni kundi gani kati ya haya mawili limetoa tafsiri sahihi kwa kile alichokisema JK, binafsi naiona kauli yake hiyo na nyingine nyingi zinazotolewa na makundi mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiserikali yanayomuunga mkono kuwa ni zenye lengo la kumfungulia njia pana zaidi ya ushindi wa kishindo wakati wa uchaguzi huo mkuu wa Oktoba.

Ukiacha kauli hiyo ya Kikwete, kipindi cha wiki hiyo hiyo moja, taifa limeshuhudia kuibuka kwa kikundi kingine cha msimu kilichojipa jina la Amani Forum, kikiongozwa na Mbunge wa Afrika Mashariki, Amaan Walid Kabourou na kujumuisha wanasiasa wengine kadhaa akiwamo, Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Shida Salum ambaye ni mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Kwa mara ya kwanza, nilisikia taarifa za kuundwa kwa kikundi hiki kupitia katika kipindi maarufu cha asubuhi cha ‘Jambo Tanzania' kinachorushwa na kituo cha televisheni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambako wajumbe wake wawili walijitokeza na kueleza kuhusu kuanzishwa na malengo yake.

Nilipowasikiliza wajumbe hao wawili ambao mmoja wao alikuwa Mrema, mara moja kumbukumbu zangu zilinirejesha mwaka 2005 na kabla ya hapo mwaka 2000 wakati wa kipindi kama hiki cha maandalizi ya uchaguzi mkuu, yalipoibuka makundi ya watu tofauti na zikajengwa hoja tofauti ambazo zote zilionekana kubeba ajenda moja kubwa ya kuilinda amani ya taifa hili kwa njia moja tu ya kuwahamasisha wananchi kuendelea kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aghalab kumpigia debe mgombea wake wa urais.

Kama ilivyokuwa mwaka 2000, walipoibuka watu kumpigia debe aliyekuwa rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa ndivyo inavyotokea leo hii kupitia Amani Forum ambayo viongozi wake wote kwa kauli moja wamesikika wakimpamba Kikwete kwa kila aina ya sifa na kuwaasa Watanzania waendelee kumuamini na kumchagua katika uchaguzi huo wa Oktoba.

Kwa namna ya kustaajabisha, kwanza kupitia TBC na baadaye katika mkutano wa hadhara huko Temeke Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam, viongozi wa Amani Forum wamejitokeza na kuanza kummwagia sifa Kikwete hata kufikia hatua ya kumtangaza kuwa mtu mwenye sifa za kipekee za kuachiwa kuendelea kutawala.

Kimsingi sina sababu hata moja ya kuwaona kuwa ni watu wa ajabu, wa hovyo au wasiofaa katika jamii, watu ambao kwa moyo wao wote na kwa nia njema, wameamua kumuunga mkono Kikwete, CCM au mgombea mwingine yeyote kugombea urais, ubunge, uwakilishi, udiwani au nafasi nyingine kwani wanao uhuru wao wa kikatiba kufanya hivyo.

Pamoja na ukweli huo, katika hili tatizo langu ni hii tabia ya kikachero ambayo imekuwa ikitumiwa na mawakala wa CCM walio serikalini, ndani ya chama hicho tawala na nje, kutumia ushawishi wenye hila, tena wakati usio wa kampeni kujenga hoja za kudumaza demokrasia ya vyama vingi na kuanza kumpigia debe rais aliye madarakani akipachikwa sifa hata asizostahili ili mradi tu kumhakikishia ushindi.

Ni wazi kwamba uamuzi huu wa kikachero wa kumjumuisha Mrema wa TLP na mama mzazi wa Zitto ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA katika kundi la kumpigia debe Kikwete wakati huu, kabla hata uteuzi wa wagombea haujaanza wakitumia staili za kimafia, unaweza kusababisha ufa mwingine wa kutoaminiana miongoni mwa viongozi na wanachama wa vyama hivyo viwili vya upinzani.

Lakini pengine kinachotia shaka zaidi katika hili ni uamuzi wa makachero wanaoitumia Amani Forum kuamua kutumia silaha ya amani kuwa turufu ya kumhakikishia Kikwete na CCM ushindi na kujenga taswira potofu vichwani mwa wananchi ambao ni wapiga kura, kwamba ushindi wa mgombea urais kutoka kambi ya upinzani ni kielelezo cha kuhatarisha umoja na mshikamano wa kitaifa.

Watu wenye kumbukumbu nzuri ni mashahidi wazuri kwamba, katika chaguzi za mwaka 1995, 2000 na 2005, silaha kubwa ambayo imekuwa ikitumiwa na CCM na makachero wanaofanya kazi ya uwakala wa chama hicho, ni kuwatisha wananchi kwamba, uamuzi wowote wa kuwachagua wapinzani katika nafasi za madaraka ya juu, ukiwamo urais ni sawa na kuchagua kutoweka kwa amani katika taifa.

Baadhi yetu bado tunakumbuka vyema namna katika uchaguzi mkuu mmoja, kituo kimoja cha televisheni nchini kwa kujua au kutokujua, kilitumia picha za vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchini Rwanda kama njia ya kuwaasa Watanzania kutoruhusu vyama vya upinzani ambavyo vilidaiwa kujijenga katika misingi ya udini, ukabila na ubinafsi.

Kama hiyo haitoshi, kipindi kingine kama hiki hiki ambacho Amani Forum imeanza kutumika kuwatisha wananchi, makachero wakilitumia Jeshi la Polisi walipenyeza nchini visu ambavyo vilikuwa na mipini inayofanana na rangi ya bendera ya chama kimoja cha siasa na kuvionyesha mbele ya wanahabari vikidaiwa kuingizwa nchini na chama hicho kama silaha za kujihami wakati wa kampeni na hatimaye kwenye uchaguzi.

Historia inaonyesha kuwa matumizi ya propaganda za namna hii, ambazo kwa bahati mbaya zimekuwa zikipuuzwa na kutopewa mikakati imara na ya kudumu ya kukabiliana nayo na makada na viongozi wa vyama vya upinzani, yamekuwa turufu kubwa ya ushindi kwa wagombea urais wa CCM.

Ni kwa njia na mbinu hizo basi, makachero wa CCM huku wakijua fika namna wanavyoweza kuwakoroga wananchi na kuwapiku wapinzani, leo hii wameamua kuja na mkakati huu wa Amani Forum kumhalalishia Kikwete ushindi wa kimbunga kwa namna ile walivyofanikisha ushindi wake mwaka 2005 na kabla ya hapo wa Mkapa mwaka 1995 na 2000.

Akili za kawaida zinathibitisha pasipo shaka kwamba, mkakati wa kumhalalisha Kikwete ulioanzishwa na Sheikh Yahya Hussein na kukwama baada ya kuonekana ukijengwa katika misingi ya imani potofu za kishirikina, sasa umejibadili sura na kujipambanua kwa njia ya Amani Forum ambayo naamini wajumbe wake wanampigia chapuo Kikwete huku wao wenyewe mioyoni mwao wakijua fika kwamba, hastahili kupewa sifa anazobebeshwa.

Hivi ni nani kati ya Kabourou, Mrema, na mama yangu Shida hajui kwa dhati ya moyo wake kwamba miaka mitano ya urais wa Kikwete imethibitisha pasipo shaka kuwa, kiongozi wetu huyo mkuu ametowesha matumaini makubwa aliyoingia nayo madarakani mwaka 2005?

Nitakuwa mkosefu wa hekima iwapo nitaandika kwamba katika kipindi chote cha miaka mitano Kikwete na serikali yake hawajafanya lolote katika medani za siasa, uchumi na jamii ingawa ukweli unabakia pale pale kwamba kama si kwa nguvu za kimtandao na kimfumo ambazo CCM inazo, anaweza akawa rais aliyefanya vibaya kuliko mwingine yeyote tangu taifa hili lianze mfumo wa kuwapa vipindi visivyozidi viwili marais wake.

Watu wenye nia njema na nchi hii wanaweza wakakubaliana nami iwapo nitaandika kwamba, turufu pekee kubwa aliyonayo Kikwete leo na ambayo inaonekana kumpa mwanga wa kushinda kipindi cha pili, ni ukweli kwamba chama kilichompa dhamana ya kutawala si chama cha kisiasa bali ni chama dola ambacho ustawi binafsi wa watu wanaokitumikia ni kuuendeleza urithi wa enzi wa marais kumaliza vipindi vyao viwili pasipo kuangalia na kuwapima katika mizani ya wazi kidemokrasia. Kama hiyo haitoshi, ni wazi kwamba udikteta wa kimfumo uliojengwa ndani ya CCM na madaraka makubwa ya kikatiba aliyonayo rais katika nchi hii, ni miongoni mwa mambo ambayo leo hii yanawatia hofu watu wenye uwezo mkubwa kuliko alionao Kikwete ndani ya CCM wa kariba ya akina Samuel Sitta, Edward Lowassa, Dk. Salim Ahmed Salim, Iddi Simba na wengine kuthubutu kuchukua fomu kumpinga ndani ya chama hicho na nje wakihofu kwamba kwa kufanya hivyo mwisho wao unaweza ukawa mbaya.

Ni wazi kwamba katika mazingira ya vitisho na udikteta wa kimfumo wa namna hii uliojengwa katika misingi ya kikomunisti ambayo ilirithiwa na CCM na serikali zake tangu zama za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kutoka China, Cuba, Korea Kaskazini na lililokuwa Shirikisho la Kisoshalisti la Kisovieti (USSR) ndiyo ambayo leo hii inatoa fursa kwa viongozi wa aina ya Kikwete kupewa sifa nyingi wanazomwagiwa na makundi ya aina ya Amani Forum ambazo aghalab hawastahili.

Hawa wanastahili kuitwa JK Forum badala ya Amani Forum.
 
Du, huu ni msitu wa habari kweli, yatosha kusema tu kutoka kwenye kicha cha habari kuwa JK katoka kwenye kauli mbiu ya Kasi mpya... halafu kilimo kwanza, sasa anatupelemba na kauli mbiu ya Amani, Hatudanganyiki.
 
Tutasikia mengi sana na sasa tunasubiri slogans gani zitakuja za kwenda nazo kwenye uchaguzi mwaka huu
 
Kibanda umekutana na hao watu na wame-confirm kuwa wao ni amani forum?? au unahisi?

''Watu wenye nia njema na nchi hii wanaweza wakakubaliana nami iwapo nitaandika kwamba, turufu pekee kubwa aliyonayo Kikwete leo na ambayo inaonekana kumpa mwanga wa kushinda kipindi cha pili, ni ukweli kwamba chama kilichompa dhamana ya kutawala si chama cha kisiasa bali ni chama dola ambacho ustawi binafsi wa watu wanaokitumikia ni kuuendeleza urithi wa enzi wa marais kumaliza vipindi vyao viwili pasipo kuangalia na kuwapima katika mizani ya wazi kidemokrasia''TZ-daima

we uza magazeti acha kutafuta wachawi, haiwezekani mrema, yahaya, shida n.k wakawa ndio chanzo cha ushindi kwa JK.

Mmeharibu upinzani nyie wanahabari na leo mnataka kutafuta wachawi. Ebu sema viongozi wa vyama karibu vyote hawataki kugombea urais wanakimbilia ubunge tatizo ni amani forum?

kwa nini Kibanda msiseme wazi kuwa upinzani ni dhaifu, ulikuwa dhaifu, nyie wanahabari mmmedhoofisha zaidi, JK mwaka huu hata atokee Musa na mitume wengine wote atashinda na source ya ushindi sio amani forum, wala Yahaya, wala nani is too cheap kwa analyst kwama wewe kuandika haya.

Mnajaribu kuandika lugha za kisiasa kuwapa watu moyo wananchi kana kwamba kuna upinzani nchi hii kumbe hauko

waambie hao wenyeviti wa vyama akitokea mmoja wao , akasimama, kidete kutetea haki za wananchi, hata akawa radhi kufa basi huyo kesho anakuwa rais... siyo hawa compromisers na wajasiriamali tulio nao

Leo CCM wakisema wanamsimamisha Lowassa au chenge au Rostam au Sofia Simba..., hata Kingunnge akitaka yeyote kati ya hao CCM wakisema go.. for presidential wanakuwa marais... achilia mbali uliowataja hao akina Salim.

hakuna cha amani forum, wala akina yahaya,... swala ni kuwa hakuna upinzani. period

unachofanya hapa ni kuudanganya umma, uone kuwa kana kwamba wapinzani wapo, ila mnajimu yahaya ndiyo anawarudisha nyuma.

Tukienda mbali sana basi ni tatizo la wananchi wooote, wanaharakati,n.k nimetoa mfano wa vyama vya upinzani kwa sababu wana jukumu la moja kwa moja katika kuiondoa CCM madarakani.

This analysis is too cheap, unaona kabisa aliyeandika aidha mlevi, au anaujua ukweli ila anadanganya umma, I dont see any motivation kwa mwananchi wa kawaida naona tu -kupass blame na kutafuta mchawi. Naona article iliyoandikwa na mroho wa fedha na smart wa kudumaza ubongo wa watanzania wengi wajue kuwa wanachofanya leo hii ni sahihi , ila kuna watu wachache ndio barrier

Kibanda tell people to wake up, tell me to wake up, tell opposition parties to wake up!! leave that cheap analysis for Shigongo!!
 
hakuna cha amani forum, wala akina yahaya,... swala ni kuwa hakuna upinzani. period

unachofanya hapa ni kuudanganya umma, uone kuwa kana kwamba wapinzani wapo, ila mnajimu yahaya ndiyo anawarudisha nyuma.

Kibanda anapowalaumu Amani Forum ni sawa na kukikimbia kivuli. Yani anaacha kuandika madai muhimu ambayo yanaweza kusaidia kukomboa watanzania katika uchaguzi kama tume huru na sheria zilizowazi za uchaguzi, anaangalia Amani Forum. Haya Amani Forum wasipokuwepo, bado majukwaani kila siku tunaambiwa TZ kuna amani na tuitunze amani kwa kuichagua CCM, na hata kama Amani Forum wasiwepo jee kwa taratibu za uchaguzi za TZ wapinzani watashinda.

Elimu ya uraia, na haki za wapiga kura ni kitendaili TZ, hayo ndio mambo ya kuyazungumzia, sio Amani Forum.
 
Haya yote ni mambo ya kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu baadae mwaka huu hivyo Kibanda yupo sahihi kabisa ila sisi kama watu huwa hatujui nini cha kufanya
 
Haya yote ni mambo ya kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu baadae mwaka huu hivyo Kibanda yupo sahihi kabisa ila sisi kama watu huwa hatujui nini cha kufanya
Wewe ndio hujui cha kufanya wenzio wanajua!Kalagabao na ubozi wako!
 
Kibanda anapowalaumu Amani Forum ni sawa na kukikimbia kivuli. Yani anaacha kuandika madai muhimu ambayo yanaweza kusaidia kukomboa watanzania katika uchaguzi kama tume huru na sheria zilizowazi za uchaguzi, anaangalia Amani Forum. Haya Amani Forum wasipokuwepo, bado majukwaani kila siku tunaambiwa TZ kuna amani na tuitunze amani kwa kuichagua CCM, na hata kama Amani Forum wasiwepo jee kwa taratibu za uchaguzi za TZ wapinzani watashinda.

Elimu ya uraia, na haki za wapiga kura ni kitendaili TZ, hayo ndio mambo ya kuyazungumzia, sio Amani Forum.

Asante kaka Mungu akubariki,

Just imagine mtu wa kawaida aliye mtaani anaelewaje hii nakala,
ataamini kuna umafia unaendelea, ila kila kitu kiko OK! JK hana sababu yoyote ya kutishika na uchaguzi wa mwaka huu, labda ndani ya chama chao.

wakati JF tumekuwa tukipambana mwako wa tu waamke, waandishi wetu wa habari ndio wanaongoza kuijaza jamii yetu ujinga. Hakuna inspiration, motivation and courageous ambayo mtu anaweza kuipata kwa nakala hiyo.

Hali ilivyo ni kuwa hata vyama vyote vya upinzani vipewe nafasi ya kumchagua mgombea wa CCM kwenye kiti cha urais kwa kudhani watamshinda hawataweza!

Kuna swal la katiba, tume huru ya uchaguzi, havisemi. Hasemi nini wafanye vyama vya siasa ili wapate kura!

Kama msemakweli alivyowataja PhD holder fake, like wise nitataja wasaliti wakuu wa mageuzi na ukombozi wa mtanzania katika hao Kibanda hatakosekana.

Nakala inatia hata kichefuchefu kuisoma na kujua ume-pata input fulani ya kuwaeleza hata wengine.

Kibaya zaidi; anamtaja mama Shida Salum, wakati huyu ni kiongozi mkubwa Chadema, that convey a message kuwa Chadema wote ni amani forum. Mrema yeye anaieleza jamii kuwa wapinzani woote ni walewale, wananchi sio wajinga, article hii inaipa credit zaidi CCM kuwa vyama havina mpango. huwa nawauliza analysis ya siasa Kibanda wanaijua au majungu ya siasa?

Kibanda mlafyale nkamu ghwangu acha nikueleze jambo la mwisho forget about these people hata kama ni wasaliti, let focus on this war, we are in battle field we dont have time to find out about these betrayers , we have time to fight with CCM,focus your weapon there, if our weapons will point betrayers we will start to fight within us, let betrayers know that we can even if without them we can, lets trees , children and all that surrounds us know that we can and we are determined to do that. This can only occur if you too Kibanda you are not betrayer of our and only mission to remove CCM from power
 
Back
Top Bottom