Ni JK au GT wa JF ndio wasiojua ?

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,315
306
Baraza la mpito la Libya limegungua kaburi la pamoja ambalo wamezikwa watu wapatao 1200 ambapo limetangaza litatumia vipimo vya kutambua vinasaba (DNA) ili kujua ndugu wa wafu hao. Ilipotokea ajali ya MV spice landers zanzibar, Rais JK aliwaomba wataalam watumie DNA ili kutambua maiti za wale ambao waliozikwa na serikali ili kujua ndugu zao. Lakini cha kushangaza , watu humu JF walikuja juu na kumshambulia Rais kuwa alikuwa hajui asemalo. Hii yaonyesha kabisa, kumbe GT wa humu JF ndio hawajui wasemalo na kuandika vitu kwa ushabiki badala hali halisi.
 
kwa akili zangu nadhani inatakiwa kuwa na database ya dna ili kufanya comparison na zile ambazo zitapatikana,
 
'Rais' alisema ikibidi DNA itumike..........haikubidi
 
kwa akili zangu nadhani inatakiwa kuwa na database ya dna ili kufanya comparison na zile ambazo zitapatikana,

Mkuu siyo lazima kuwa na data base ya DNA profiles ili uweze kutambua maiti. Unahitaji ndugu wa marehemu ambao wanachangia wazazi ili uweze kulinganisha DNA zao.

Siyo kazi ngumu sana kwani pale kwa Mkemia Mkuu wanafanya...Kama kipimo hiki hakikutumika kwa wahanga wa Meli huko Zenji ni uzembe wa serikali!
 
Ogopa Wanasiasa bwana GB!
Ishu ya Libya haijajiegemeza kwenye u-political vampire'

Ishu ni kwamba Mkubwa alikurupuka kusema, wakati anajua wazi kuwa zoezi hilo maandalizi yake yatachukua miaka kadha, na hadi kufikia ukamilifu itakuwa yeye hayupo madarakani!
Kama ishu ndogo za kuunda kamati kuchunguza chanzo cha mlipuko wa silaha hazitoi majibu kwa miaka, itakuwa suala hilo la uchunguzi wa kisayansi wa DNA?...
JE REAGENTS ZIPO ZA KUTOSHA?...Maabara vipi?...Je related cases za kawaida zisizo za emergency zinakuwa solved kwa efficiency gani?
Kuna maswali mengi zaidi ya majibu kwenye kauli ya JK!
 
Kwani hapa hoja hasa ni nini? Rais kusema? Mambo mangapi yametolewa tamko na Rais
lakini hadi sasa hayajatekelezwa au hayatekelezeki? Kwanza tunajua gharama ya DNA?
 
Mkuu siyo lazima kuwa na data base ya DNA profiles ili uweze kutambua maiti. Unahitaji ndugu wa marehemu ambao wanachangia wazazi ili uweze kulinganisha DNA zao.

Siyo kazi ngumu sana kwani pale kwa Mkemia Mkuu wanafanya...Kama kipimo hiki hakikutumika kwa wahanga wa Meli huko Zenji ni uzembe wa serikali!
Hujamwelewa Silly alichomaanisha, Tanzania hatuna DATA BANK ya DNA hata hizo DNA za wazazi wa marehemu unaowasema hazipo sehemu yeyote ile itabidi na wao wapimwe kwanza. Nchi za wenzetu mtoto anapozaliwa anakuwa na file lake likiwa na vipimo vya DNA kwa hiyo inakuwa rahisi kumtambua janga linapotokea, kwa Tanzania ni vigumu sana kwa vile hatuna data bank yeyote mbali ya cheti cha kuzaliwa Birth certificate hata hicho kwa wazazi wetu ni vigumu kuvipata sembuse vipimo vya DNA zao. Ndio maana watu walikejeli JK aliposema maiti watapimwa DNA kutambua ndugu zao ambao hajui atapata wapi vipimo vyao.
 
Ogopa Wanasiasa bwana GB!
Ishu ya Libya haijajiegemeza kwenye u-political vampire'

Ishu ni kwamba Mkubwa alikurupuka kusema, wakati anajua wazi kuwa zoezi hilo maandalizi yake yatachukua miaka kadha, na hadi kufikia ukamilifu itakuwa yeye hayupo madarakani!
Kama ishu ndogo za kuunda kamati kuchunguza chanzo cha mlipuko wa silaha hazitoi majibu kwa miaka, itakuwa suala hilo la uchunguzi wa kisayansi wa DNA?...
JE REAGENTS ZIPO ZA KUTOSHA?...Maabara vipi?...Je related cases za kawaida zisizo za emergency zinakuwa solved kwa efficiency gani?
Kuna maswali mengi zaidi ya majibu kwenye kauli ya JK!
Mkuu, umumwambia mambo mengi ya kumtosha kabisa.

1) Anaijua maabara ya mkemia mkuu huyu?? dokezo.....reagents ni issue kubwa sana pale.
2) Kama hamuwezi kuifikia meli, mtapima vinasaba vya samaki au??.......Mmeleta wazamiaji wanaozama 53m only, wakati mnajua pale Nungwi pana zaidi ya 300m. Mlifikiri hiyo meli ingezama ki-sharobaro??

Watuwalimpiga Kikwete kwasababu alitoa political statement isiyo na mashiko.
 
kwa akili zangu nadhani inatakiwa kuwa na database ya dna ili kufanya comparison na zile ambazo zitapatikana,
kwani dhamira si kujua ndugu zao walioko hai ili wafu wale waweze kutambulika walikotoka????
data base ya nini wakati ndugu zao wapo??????
 
Wewe nawe maiti imeharibika labda imeliwa na samaki na kubaki mifupa utaitambuaje wakati kuna maiti(mifupa) zaidi ya mia mbili.
 
Rais alisema nini kuhusu waliozembea na kupelekea meli kuzama???? na akisema ni kweli atatenda??????????
 
baraza la mpito la libya limegungua kaburi la pamoja ambalo wamezikwa watu wapatao 1200 ambapo limetangaza litatumia vipimo vya kutambua vinasaba (dna) ili kujua ndugu wa wafu hao. Ilipotokea ajali ya mv spice landers zanzibar, rais jk aliwaomba wataalam watumie dna ili kutambua maiti za wale ambao waliozikwa na serikali ili kujua ndugu zao. Lakini cha kushangaza , watu humu jf walikuja juu na kumshambulia rais kuwa alikuwa hajui asemalo. Hii yaonyesha kabisa, kumbe gt wa humu jf ndio hawajui wasemalo na kuandika vitu kwa ushabiki badala hali halisi.

kuna habari za mil 600 kumwagwa ili msifie ccm na serikali yake. Vipi na wewe umepewa laptop hiyo kusifia kaka..... Hongera
 
mara nyingi viongozi wanaongea kujiongezea umaarufu tu, hata hao viongozi wa serikali ya mpito ya wali bia hamna lolote.
 
Back
Top Bottom