Kwanza napenda kuwatakia watanzania wote, mafanikio mema katika kumaliza mwaka huu, mimi binafsi ni mwananchi nchi wa tanzania, naipenda nchi yangu sana, lolote linalo tokea au kusemwa kuhusu nchi hii, linanihusu.Kama ni zuri au baya lina nihusu, na hasa lina nifurahisha au lina nichukiza, kwa sababu mimi ni mtanzania.Ndugu zangu nchi yetu inamiaka ,50 na zaidi toka uhuru, yametokea mengi mazuri, mazito, mepesi, yakukatisha tamaa, mfano kutofanikiwa kushinda hasa kwenye mchezo wa soka hasa kipengele cha club bingwa afrika na kombe la dunia, kwa kweli mimi kama mtanzania inaniuma sana, lakini kuna zuri la kujivunia, na hasa hapa sifa apewe Mwenyezi Mungu, kwa namna kubwa sisi ni wamoja kama ndugu wa jamii moja, tunashirikiana, kwenye mambo mbali mbali kama kwenye harusi, maziko na shughuli mbalimbali za kijamii.Ndugu zangu sisi ndio watanzania, baadhi yetu tunapenda kusifia sana bila kufanya uchambuzi, lakini wachache wetu huamua kufanya utafiti baadhi yao huu toa uo utafiti ili utumike kuleta ustawi bora wa maisha yetu. Baadhi yetu husubiri jambo liharibike wajekusema "sinlinkwambia" wanasubi liharibike wapate cha kukosoa, mwanzo hawakuongea kabisa kutoa ushauri kwa wahusika, hubaki kuuzungumza ukweli huo vibaradhani kwao kwenye kaya zao.Ndugu zangu dhumuni la kuandi maandishi haya nikutaka kuweka taarifa sahihi kwa namna tunavyo enenda kama familia moja, taifa moja na nchi moja yenye lengo la kufanikiwa na kuwa na mustakabali mmoja wakuwa na jamii bora kwa ustawi wa taifa letu.Najaribu kuangalia viongozi tulio wahi kuwa nao toka tupate uhuru, katika ngazi ya uraisi, na msingi wa wao walicho amini katika kuboresha taifa lao kwa maslai ya wote, au kuboresha taifa lao kwa maslai ya wachache,("sasa zamu yetu").Ndugu zangu raisi ni taasisi pana sana, laki taasisi hiyo bila mtu moja anae anzisha jambo(raisi),haiwezi kuwa na maana yoyote, nataka nimuangalie raisi kama mtu personal, na mna anavyoweza kuwa salama, katika hali zote, raisi wa nchi hasa kama tanzania, hana haja ya kuwaza pesa, hana haja ya kuangaika usiku na mchana kuakikisha na yeye anakuwa na vitalu vya uwindaji, raisi wa nchi hana haja ya kuangaika kulimbikiza hela na kuwa na utajiri kama mlima kilimanjaro. Raisi wa nchi kama yakwetu, atakula, atavaa, atalala, atatembea sehemu salama, kuliko mtu yoyote katika taifa letu.Na ili uwe na maisha mazuri ya raha na furaha siku zote hapa duniani, jitaidi kusaidia wengine. Nasema raisi wa nchi hasa za kwetu hana tofauti sana na mfalme, anapewa kipaumbele kwanza kuliko mtu yoyote, kwa hiyo hana haja ya kujaribu kuzoa malizote za taifa na kujimilikisha, au kujimilikisha yeye, akihisi kwamba nikistaafu naweza kuanzisha biashara nzuri, au kuwa kama wafanya biasha flani wakubwa, ni aibu raisi wa nchi kuwa na miradi mikubwa au kuendesha miradi mikubwa kama wafanya biashara, ni aibu na wala sio sifa nzuri na wala upendezei baada ya kustaafu wewe kama raisi ukajulikana kama na wewe ni mfanyabiasha, ukawa unakaa na wafanya biasha wakubwa mnajadili jambo, na watu sasa hivi wasikuone tena kama raisi kwani uraisi ulikwisha kwa hiyo wewe uko huru kufanya lolote, kwenda popote, kuona kama lolote linawezekana, hapana haiko ivyo, uraisi au taswira ya uraisi au haiba ya uraisi haiishi mpaka unachimbiwa chini ya ardhi.Usitegemee kunasiku utajiamulia unavyo taka, mfano kwenda kucheza karaoke, kwenda kunywa togwa, ukajiamulia tu, alafu ukaenda na mambo yakawa kawaida, hajawai kutokea, hata wewe ukiamua unaweza jaribu kufanya, ila jamiii ya eneo husika itakuwacha usakate rumbaa mwenyewe.Kwa hiyo uraisi sijambo la mzaha.Mambo ya maadili mema katika utendaji hayaanzi chini, ila huanzia juu.Mfano mzuri ni nyumbani, baba na mama wanapokuwaa na tabia njema, watoto wanarithi, wazazi wakiwa na tabia mbaya watoto wanarithi pia,ndio maana sisi ni matokeo ya malezi ya wazazi wetu, ndio maana familia nyingine husali pamoja, familia nyingine ni ugonvi kila siku.Hivyo hata kwenye utendaji wa kufanya kazi serikalini, usiseme mwanachi asipokee rushwa, inatakiwa aone tabia za babayake anavyo ichukia rushwa na namna anavyo washughulikia wanao toa na kupokea rushwa.Binadamu nikiumbe kinacho ishi kulingana na nyakati, kina tegemea sana nyakati ili kiendane mazingira, ukitaka kujua ninachoongea kina maana gani angalia kauli za viongozi alio wateua magufuli, wengi ndio hawa hawa walishiriki katikamaamuzi ambayo leo wote tunamlaumu kikwete kuyachukua, wengi wa watendaji wa serikali ile tunayosema ilikuwa na maamuzi mabaya asilimia kubwa ndo hawa hawa aliokuanaonao magufuli, lakini angalia ndimi zao zillivyo geuka wote wanaongea kama wameshuka mbinguni leo, nini kimetokea, kwa sababu baba anaendesha familia ni si yule tena ni mwingine na amekuja na taratibu zake nyingine kwahiyo ili ubaki salama inabidi ubadilike, kinyume chake utakuwa jiwe la chumvi, hawa hawa walisema miaka kadha iliyopita kwambaelimu bure ni ndoto, sasa kawaulize leo vipi elimu bure inawezekana au laa.Kwahiyo ni kwamba anacho fanya maagufuli si jambo jipya kwa wanao elewa mamboila ni jipya kwa wasiopenda kutafakari nakupima mambo kwa mapana yake. Nchi hii inawachapakazi wengi sana, inategeme dereva yukoje, kalewa chakari, au kichwa chake kiko vizuri kwakuwa alilala usiingizi wakutosha kabla hajachukuwa motokaa, na kuelekea kule kwenye maendeleo tulipo kubaliana atupeleke. Siku njema Mungu ibariki Tanzania na Dunia iwe sehemu salama ya kuishi.