Ni jinsi gani gharama za maisha kupanda na mfumuko wa bei ulivyo guess taratibu zako za maisha?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Ndani ya miezi 12 tumeona mifumuko ya bei kuanzia bei ya mkate, unga, nyama hata nauli ya basi. Wengine wameamua kurudi kijijini kwa ugumu wa maisha na wengine wamehamia kwa ndugu kupunguza makali ya kodi ya nyumba.

Ukweli halisi matabaka yote ya watu yanahitajika mjini ili maisha yaende leo. Sisi wapika maandazi tuna umuhimu katika kundi la watu wa kipato fulani, wakila maandazi mawili na maji wanamshukuru Mungu na siku inapita kesho wanakwenda kwa matajiri kutafuta kibarua.

Mfumuko wa bei umebadilishaje maisha yako?
 
Ngoja tukae kimya...hawachelewi kuita watu Sukuma gang...and is this is just a begining.
 
Bora Tanzania. Nipo hapa ndola wali maharage ni kwacha 40 ni sawa na tsh 5500. Daladala kutoka town hadi indeke (km 6) ni kwacha 10 ni tsh 1380.
Nyanya fungu zikiwa tatu ni kwacha 10 = tsh 1380. Coca cola ndogo ya chupa ml 300 ni k7 = tsh 972. Mkate gram 500 ni k 17 = tsh 2360.
 
Nasubiria bei ya umeme kwa unit ipande, nisikie na bei ya mafuta mwezi huu itakuaje, nikamilishe bajeti ya kufungia mwaka huu...tukiendelea na hii KITABU ya "kuupiga mwingi"
 
Bora Tanzania. Nipo hapa ndola wali maharage ni kwacha 40 ni sawa na tsh 5500. Daladala kutoka town hadi indeke (km 6) ni kwacha 10 ni tsh 1380.
Nyanya fungu zikiwa tatu ni kwacha 10 = tsh 1380. Coca cola ndogo ya chupa ml 300 ni k7 = tsh 972. Mkate gram 500 ni k 17 = tsh 2360.
Mkuu mbona zambia masela wangu wako huko life wanasema liko chini sana..vitu bei chini sana

Sent from my SM-M305F using JamiiForums mobile app
 
Jirani yangu mke wake alijifungua mapacha mwaka wa jana, mwaka huu wamepata tena mapacha watatu. Gharama za hospitali ilibidi baba yake auze ng’ombe.

Maisha yao ni katika chumba na sebule, jamaa kila akipiga mahesabu ya familia ya watu saba ndani ya chumba na sebule. Ameamua arudi kijijini mzee amkatie shamba na kumkopesha mifugo.
 
Pole yake angesoma yasingemkuta haya yote
 
Back
Top Bottom