Ni jambo la kushangaza kwa Mkurugenzi aliyeiba mabati kuendelea kuwa ofisini hadi muda huu

Mama sio lazima afanye kila kitu ndio maana anateua mawaziri ili wamsaidie. Mathalani hili suala la DED lipo chini ya TAMISEMI lakini waziri yupo kimya hata kukemea hajakemea au naye anasubiri maagizo kutoka juu?
Huo u-DED wenyewe umekuwa wa kugawana kama njugu kwa ndugu, jamaa na marafiki, bila shaka kuna kigugumizi cha kuchukua hatua kinahusika hapo....angekuwa jaffo ashamaliza mchezo hapo.
 
Mkurugenzi wa halmashauri ya gairo, bw Asajile Mwambambala aliyehusika katika wizi wa mabati zaidi ya 1100 mwaka huu mwezi wa saba alipaswa awe nje ya ofisi hadi muda huu. kwani kwa mujibu wa kanuni za maadili ya utumishi wa umma ni kosa kwa mtumishi yeyote wa serikali kujihusisha na wizi au ubadhirifu wa mali yoyote ya kiofisi au mali ya umma

Kwahiyo nilitegemea katika hatua za awali, wizara ya Tamisemi ambao ndio mamlaka yake ya nidhamu wawe wamemwandikia barua ya kumsimamisha kazi mara moja mkurugenzi huyo ili hatua zingine ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwa makosa aliyoyatenda

Badala yake mkurugenzi huyo hadi muda huu bado yupo ofisini na mwezi huu wa tisa anasubiri kulipwa mshahara ambao kimsingi ni kodi ya wavuja jasho aliowaibia mabati.

Je, kitendo hiki cha DED kuendelea kubaki ofsini kinatoa tafsiri gani?

Au labda waziri mwenye dhamana anakubaliana na kitendo hicho kilichofanywa na DED ndio maana anachelewa kuchukua hatua?

Je, mamlaka zake za uteuzi na nidhamu kuchelewa kuchukua hatua ni kutengeneza mwanya wa kuja kumsafisha baadaye ionekane hakuhusika katika kufanya ubadhirifu?
Huko ni kada wa ccm,istoshe ccm wote ni majambazi sugu
 
Keshasimamishwa kazi Leo.
 
Back
Top Bottom