Ni jambo la kushangaza kwa Mkurugenzi aliyeiba mabati kuendelea kuwa ofisini hadi muda huu

msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
839
1,472
Mkurugenzi wa halmashauri ya gairo, bw Asajile Mwambambala aliyehusika katika wizi wa mabati zaidi ya 1100 mwaka huu mwezi wa saba alipaswa awe nje ya ofisi hadi muda huu. kwani kwa mujibu wa kanuni za maadili ya utumishi wa umma ni kosa kwa mtumishi yeyote wa serikali kujihusisha na wizi au ubadhirifu wa mali yoyote ya kiofisi au mali ya umma

Kwahiyo nilitegemea katika hatua za awali, wizara ya Tamisemi ambao ndio mamlaka yake ya nidhamu wawe wamemwandikia barua ya kumsimamisha kazi mara moja mkurugenzi huyo ili hatua zingine ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwa makosa aliyoyatenda

Badala yake mkurugenzi huyo hadi muda huu bado yupo ofisini na mwezi huu wa tisa anasubiri kulipwa mshahara ambao kimsingi ni kodi ya wavuja jasho aliowaibia mabati.

Je, kitendo hiki cha DED kuendelea kubaki ofsini kinatoa tafsiri gani?

Au labda waziri mwenye dhamana anakubaliana na kitendo hicho kilichofanywa na DED ndio maana anachelewa kuchukua hatua?

Je, mamlaka zake za uteuzi na nidhamu kuchelewa kuchukua hatua ni kutengeneza mwanya wa kuja kumsafisha baadaye ionekane hakuhusika katika kufanya ubadhirifu?
 
Twende taratibu mkuu, imethibitika DED ndiye mwizi au uhusika wake ni kutokana na kwamba yeye ni kiongozi na alitakiwa kusimamia mabati yasiibiwe hivyo kuibiwa mabati kimetafsiriwa kama uzembe wa DED kwahiyo anaunganishwa?
mkurugenzi aliiba mabati
 
Huyu ni kada mtiifu
Twende taratibu mkuu, imethibitika DED ndiye mwizi au uhusika wake ni kutokana na kwamba yeye ni kiongozi na alitakiwa kusimamia mabati yasiibiwe hivyo kuibiwa mabati kimetafsiriwa kama uzembe wa DED kwahiyo anaunganishwa?
 
uzembe wa DED
hakuna mahali, from the very beggining lilitamkwa neno uzembe. It was THEFT in capital letters. Wiziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Huyo ujue hajaiba hayo mabati,bali alipakaziwa tu
Hivi unajua huo wizi umechunguzwa na kutolewa ripoti na jeshi la polisi?

Kwahiyo unataka kusema jeshi la polisi wameongopa na wanataka kumbambikia DED kesi ya wizi?
 
Back
Top Bottom