Ni jambo gani lishawahi kukutokea ukasema hautakuja kuamini katika mapenzi?

mishamusic2

Member
Feb 4, 2021
51
43
Nilisomea udereva, katika hustle zangu nilifanikiwa kuajiriwa kwenye makampuni ya asafirishaji wa mafuta kwenda nchi jirani kama congo, zambia Et el.

Kwa namna yoyote ile nilipambana zaidi kuyaweka maisha sawa, ilimradi familia yangu iishi poa, ikiwa pia familia ya mke wangu (Salma). Nilifanikiwa kujenga nyumba bora , kununua gari kutembelea na kumfungulia mke wangu salon kubwa ya kike jijini Dar, kiufupi nilifanya kila kitu kwajili ya furaha ya mke wangu na familia kiujumla.

Katika mihangaiko yangu sikufanikiwa kudumu katika makampuni niliyokuwa nikifanyia kazi mana pesa zote izo nilizipata kwa njia ya uwizi wa mafuta (kushusha pipa 3 kila trip) kitu kilichofanya kuingizia makampuni hasara kubwa i was taking Risk ili kutoboa tu, nilifukuzwa makampuni yote makubwa ya Dar.

Nilihisi mabadiliko kwa mke wangu jambo lililofanya nijiulize shida nini? Kutaka kufanya uchunguzu, Nilihisi nachezewa draft labda kwakua sikuwa mtu wa kushinda nyumbani, Mapema alfajiri siku niliyotakiwa kusafiri nilimuaga mke wangu akanipa mabusu na baraka tele kunitakia safari njema, niliondoka nyumbani na mizigo yangu. Lakini plan yangu ilikuwa nisiondoke iyo siku, nilienda mjini nikapoteza muda mida ya saa nne usiku nikarudi nyumbani, nikakaa seblen nimezima taa naendelea kupombeka.

GHAFLA! nikasikia gari limeingia parking watu wawili wakiongozana, wakaingia seblen taa ikawashwa PAAP!! maskini Mke wangu kashikana kiuno na boda boda wake huku wamelewa pombe sana, nilipata mshtuko nikamruhusu yule kijana aondoke kwa amani, nikamchukua mke wangu nikamwambia akaoge bafuni, kimawenge akaoga akamaliza, nikamuita nikalala nae kitandani mpaka asubuhi bila kufanya chochote... Kulivokucha nikamwambia akushanye kila kilicho chake na kuamua kumrudisha kwao kijijini.

Mimi mapenzi basi tena, saivi mke wangu aliyebaki ni POMBE tu (kali), huyo hatonisaliti kamwe sina furaha tena, SIWEZI KUAMINI KATIKA MAPENZI.
 
Sikuhiz ni kawaida kucheatiwa.tena bodaboda wanatukula balaa.Ndo maana wanavamiwa ovyoovyo
 
Chai ya rangi hii.......madereva hawa hawa ninaowajua niliwahi kuwasimamia Total? Madereva hawahawa wa mfano wa Sunshine Transportation? Tuache utani na ghorofa
 
Back
Top Bottom