Ni jambo gani linakukera kwenye Redio za Tanzania?

kuna mambo yanakera sana. Kuna wakati nilijikuta nasikiliza kipindi cha michezo cha kiingereza cha tbc, kilikuwa kinarushwa jioni/usiku.

kilikuwa na watangazaji wawili wa kiume wakiongea kiingereza. Ilikuwa ni dhahiri watangazaji hawa hawajui lugha hii.

Sijawahi kusikia kiingereza kibovu km kilichokuwa kinatumiwa na hawa watangazaji wa radio ninayoamini ilipaswa kuwa kioo kwa radio zingine hapa nchini.

Wakati mwingine unajiuliza "hawa si waongee kiswahili tu" maana wanachoongea sio kiingereza bali walikuwa wanatafsiri kiswahili kwenda kiingereza tu.

Inatia shaka sana kama haya yanaweza kutokea kwenye radio kongwe yenye hazina ya uzoefu na utalaam wa mambo ya habari.

Tatizo watu wanaochukuliwa kwenda kutangaza wanakuwa hata hiyo taaluma ya utangazaji hawana , wanaokotwa okotwa tu ndiyo maana tunasikiliza vioja tu.
 
Back
Top Bottom