Ni jambo gani linakukera kwenye Redio za Tanzania?

mike2k

JF-Expert Member
May 12, 2016
1,458
3,127
Mimi naanza na hawa Clouds Media Group

Clouds FM mnazingua sana kwa jinsi mnavyoi promo hiyo show ya fiesta mnakera sana tangazo kila baada ya dakika nne.

Hakuna cha maana mnazungumza ni fiesta tu. Yaani radio yenu haina maana yoyote ni issues za fiesta muda wote. Mnaboa sana.

Njia pekee ya kuvutia watu kwenye tamasha sio kuharibu vipindi vyenu ni kuwork smart tu. na watangazaji walivyo wavivu nao kila dakika wanazungumzia hiyo show as if ni sherehe ya kitaifa.

Lazima mtambue kuwa sio wote wanaosikiliza hiyo radio wanayo access ya kufika kwenye hilo tamasha hasa sisi wa mikoani.

Mfano mimi huku rombo hilo tangazo la fiesta na hayo maelezo ya fiesta ni non sense hayana faida yoyote kwangu zaidi ni kero tu. Mimi ninachokihitaji ni taarifa. nahitaji information.

Pili:

RADIO ONE.jpg


Radio one (IPP MEDIA) na studio yao ina muonekano wa ovyo sana. studio haina mvuto kabisa. Bi Joyce kama mkuu wa superbrand mnapaswa kuboresha hii studio iwe na muonekano wa kisasa ili muweze kustream online kisasa.

Atleast iwe kama ya Wasafi Katika Radio zenye on air studio kali Tanzania, probably wasafi fm ni namba moja Tanzania.

What future hold for radio?
Modern society is image-obsessed, so radio can maintain its individuality by not following suit.

From the very beginning, the advantage of radio has been its ability to boost the imagination via the content being broadcast.

Adding images to its content could make it lose its charm and scar the future identity of radio itself.
 
Watangazaji wengi wanachukua chukua tu taarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii na kuzitangaza. Nyingi zikiwa ata hazina vyanzo vya kueleweka.

Kuna hii nyingine unakuta watangazaji wako zaidi ya wawili studio wanaendesha kipindi basi ova genge la wahuni ni makelele kila mtu kujiona mjuaji wanabishana wenyewe kwa wenyewe yaani ova hawapo ON AIR.

Na sababu nyingine nyingi ndio zinazochangiaga nisisikilize sana radio.
 
Ase kuna radio Inaitwa Kill Fm. Ipo Kilimanjaro haijasambaa sana. Watangazaji wa ajab ajabu. Kelele kelele mingi. Hasa kuna kipindi kinaendeshwa na chali mmoja wa kiume ila tabia za kike. Radio inakua na kipindi cha mipasho ni redio hiyo kweli. Afu mtangazaji mwanaume
 
Mad Max, Kuna kipindi wasafi fm wanaokota upumbavu mtandaoni na kuwasomea watu kama ni kweli vile, utasikia mtangazaji akisoma tena kwa uhakika kuwa Tupac yupo hai, maendeleoa ya Marekani yameletwa na aliens (viumbe kutoka sayari nyingine), UKIMWI umetengenezwa na wazungu, na upumbavu mwingine mwingi
angesoma hata pande zote mbili anagalau wanao propose hizo theories na wanaokanusha, kisha msikilizaji mwenyewe ndio aamue kuamini ama la na kumchcochea afanye utafiti zaidi, sio kuaminisha umma ni kweli
 
Kipindi kimoja kua idadi kubwa ya watangazaji mwishowe kelele tupu, pia kuzungumza jambo kiholela hata lenye uhitaji wa taaluma na kutotumia lugha fasaha ya kiswahili wanakera sanaaaa
Kila mtangazaji ana kiswahili cha kichuga halafu kiswahili kimarekani
You know unajua
I got yuuuu nimekupata mzee
Listen listen sikiliza

Na takataka Kama hizo kuigana igana sasa Dah unaweza kuhisi wanahama stations

Kipindi cha masaa ma3 (saa Moja wadhamini nusu saa makelele nusu saa mambo ya instagram robo saa majungu kwa watu wa tofauti dakika 20 vibwagizo hawajapiga singeli dakika 5 za mwisho ndio content hapo ndio utasikia malizia malizia habari ya mwisho wenzetu wameshaingia tuwaage wasikilizaji)
 
Kuna jamaa anasauti pana sana yupo hapo nimekuwa namsikiliza mara chache nikipita kwenda mby somebody jakobo...kumbe nao upupu tu
Kuna Radio station tunayo kwetu huku makambako inaitwa" Ice" fm makambako ni madudu mtupu
 
Watangazaji kufanya hoja muhimu mzahamzaha...mtu kafa wanataka waifanyie comedy hiyo taarifa...alafu Hawa watangazaji wengi hawana tabia ya kusoma Wala kusikiliza taarifa ya habari.. hawajui kinachoendelea duniani..wao zaidi ya kuingia insta sijui Kama wanavyanzo vingine vya kupata taarifa na ndio maana kwao kila kitu Ni matani..wanakera na kuchekacheka na kelele sana ovyo.
 
Kuna hiyo magic radiio wakiingia salma msangi na wenzake kelele nyingi mipasho mingi nyimbo nyingi hawa kutulia kuleta habari ovyo sana ikifika saa nne huwa nafunga redio siwasikilizi magic
 
Back
Top Bottom