Jum Records
JF-Expert Member
- Jun 30, 2014
- 547
- 551
Habarini wana JF, ni jambo gani la ujasiri wa kiwango cha juu sana ambalo uliwahi kufanya kiasi kwamba mpaka leo hii ukikumbuka unajiona mwamba...? Mimi binafsi jambo la ujasiri kufanya ni kutibu mbwa wa mama Mmoja ambae ma dr kibao wa mifugo walishindwa kumtibu akapona...wakawa wanamkimbia yule mama..wakat mwingine akiwapigia simu hawapokei..akikutana nao njiani kwa bahati wanamchenga...lakini mimi baada ya kumwona yule mbwa nikamwambia mama yule mmiliki usinipe pesa kwanza mpaka mbwa wako apone...nikakomaa nae kwa dawa siku 5, nikifuatilia dose vizuri pia nikihakikisha anakula vizuri kwa gharama zangu...baada ya siku 5 yule mbwa akapona kabisa....mama yule hakuamini yeye na familia yake...nikapewa pesa ndefu sana..na mtaani nikapata sifa balaa...ni jambo ambalo huwa najisifu sana maana ma dr wengi wenye uzoefu wa mifugo walishidwa... Share na wewe jambo lako la ujasiri uliofanya!!!