Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,014
- 1,498
Salaam kwenu waheshimiwa.
Nimetafakari kwa kina kadiri ya ufaham wangu ila sijafanikiwa kupata jibu moja lisilo na shaka na kujikuta nikibaki na "labda" Naamini hapa nyumbani kwa wasomi naweza kupata jibu lisilo na shaka.
Mataifa mengi yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi na uhakika wa kuhudumia watu wao ikiwemo Japan, uingereza, Amerika na mengineyo wameweka ukomo wa idadi ya watoto wa kuzaliwa kwenye kila familia moja, yaani Mume na mke wameruhusiwa kuzaa watoto ama mmoja, wawili au watatu na si zaidi ya hapo na hawaruhusiwi kabisa kuzaa watoto wengine zaidi ya wale walioruhusiwa na mamlaka.
Lakini hapohapo wanaruhusiwa kuasili (kuchukua watoto wakulea)kutoka katika Mataifa mengine na kuishinao kama watoto wao wakuwazaa wakiwahudumia kila kitu, ninachotaka kujua hapa ni nini lengo la kuwawekea watu wao ukomo wa kuzaa?
Maana mimi binafsi nilidhani wamelenga kupunguza ongezeko la watu kwenye mataifa yao lakini watapunguaje ikiwa wanaruhusiwa kuchukua watoto kwenye mataifa mengine na kuwaingiza nchini mwao!?
Au labda lengo ni kulinda afya za akina mama zao kwa kuwazuia wasizae watoto wengi!? Au kuna jingine lolote lililofichwa!? Tafadhali, Wakuu napenda kujua mitazamo yenu.