Ni ipi nafasi ya Usalama wa Taifa ktk ubadhirifu kwenye Halmashauri hadi imefikia Rais na Waziri Mkuu ndio wagundue?

Kwani hawewezi kuzuia wizi huo na badala yake kichongea watu?
Endelea kujidanganya Mkuu, hao jamaa wako kila idara za serikali. Mnasuka mpango wa kupiga pesa pamoja kumbe wanawasoma tu, siku kiongozi mkubwa akifika anakuwa anafahamu kila kitu...

Na kuwatambua mbona ni kazi ndogo sana, hao ndio informer sasa...
 
Hapa ndo unafikia khatma ya kusema jf kuna watu wenye upeo finyu kuliko ufinyu wnyw
TISS ni watazamaji tu na kamwe hutajuq lini walijua uozo huo. Hii huwasaidia kujua ukubwa wa mtandao husika. Lakini usidhani ni kwa kila kitu ni watazamaji la hasha. Mfano TISS wakipata fununu kuhusu utekaji wa mtu kijasusi na wao si wahusika huuzima mchezo kimya kimya. Matukio kama hayo ni nadra kutokea. TISS wako very critic KATIKA kuyachambua mambo wakagundua hili au lile laweza kuhatarisha usalama wa nchi hukuweka katika screen zao wakichech movie na kukabidhi walinzi wengine kuingilia kati wao wakiwa kama watchdogs tu.
 
TISS ndo wanaowatonya japo pia ndo hao hao viongozi wapigaji coz wateuliwa asilimia kubwa kama sio wote ni member wa TISS a.k.a watu wa mfumo. Ndo maana huwa naona ni kama mchezo wa maigizo wanatufanyia sisi wanachi wa kawaida.
 
Ni sahihi kabisa kwanza inabidi ujue TAKUKURU ndo haohao TISS vilevile na wateuliwa i.e wakuuu wa idara hapo halmshauri aslimia kubwa ni hao hao TISS ndo wanaopewa mashavu.
Inawezekana hao ndio wanamjulisha Rais au Waziri mkuu. Shida kubwa ni jinsi watu wanavyolindana kwenye hizo issues za wizi wa mali ya umma.
Ni ngumu mno kuchukuliana hatua. Inawezekanaje Takukuru hawajui hayo yanayoendelea? Je ni halmashauri ngapi zina matatizo ya wizi na ubadhilifu? Maana bila kumaliza matatizo kama hayo, maendeleo hatutaweza kuyafikia.
 
Soma act ya TISS wewe, kwa akili zako ulitaka TISS wakigundua ndio wafanyie kazi wao wenyewe? Mbona wa bongo wengi ni akili ndogo hivi kazi ipo kweli kweli
 
Wao wanachakata taarifa,halafu wanakabidhi kwa wahusika ili hatua stahki zichukuliwe.Kipindi hiki wako macho sana ndugu yangu.
Hawajawahi kuacha kuwa macho tangu iumbwe Tanzania,sema kipindi hichi wanasikilizwa mno na kupewa kipaumbele.
 
WanaJF, mnakumbuka uchafu na uozo mwingi wa ufujaji wa fedha za umma ktk Halmashauri zetu zinazofichuliwa na Waziri Mkuu na wakati mwingine Rais Magufuli mwenyewe.

TISS wamejaa kila mahali nchini na nashindwa kuelewa kwanini hali hii itokee hadi viongozi wakubwa ndio wanakuja kufanya ufichuzi. Rejea Mkoa wa Morogoro na Singida ktk ziara za Majliwa.
Sasa ndiyo ujue kazi nzuri ya TISS PM na Rais wanasoma taarifa zilizofanywa na hao wanaume wa kazi underground.

Na hutamjua TISS kamwe ni nani hapo ndani ya ofisi yako
 
Back
Top Bottom