Ni ipi nafasi ya Usalama wa Taifa ktk ubadhirifu kwenye Halmashauri hadi imefikia Rais na Waziri Mkuu ndio wagundue?

kwahiyo kazi yao ni kufuatilia namna ufisadi unavyofanyika mpaka mwisho then ndio watoe taarifa?Hawana jukumu la kuzuia ufisadi usifanyike?
Uwezi kuzuia tabia ya mtu aliyozaliwa nayo.
Tabia ni kama ngozi,rushwa,wizi,ufisadi au ubadhilifu wa Mali za Serikali ni hulka tu ya mtu kujinufaisha mwenyewe.
Watu wa namna hiyo yawezekana hapo zamani walikuwa ni wachoyo,wadokozi na wabinafsi kwa wenzao.
TISS hawawezi kuzuia kwa sababu sheria zote zipo mbali na amri kumi za Mungu,hivyo ili wabaini inabidi jambo litendeke kwanza.
Sina hakika kuwa hata kama ni wewe unaweza kuota tu jambo then asubuhi unalizuia.
Kwa ufupi ufanyaji kazi wowote kwenye weledi hauitaji hisia/tetesi kama ndio kielelezo cha tukio.
 
uko hivi viongozi wa TISS wanajulikana uko halmashauri kwaiyo deal likipigwa hao hao viongozi wa TISS wanakula mgao, kwa nachotokea hawa watendaji wa TISS wadogo ndio huchoma uko juu usifikilie TISS ni maraika ni binadamu wana njaa na shida kama wewe
tena njaa kali sana si tunawajua!?
 
Maeneo makuu ya kazi za Idara ya Usalama wa Taifa ni kukusanya na kuchambua habari za kiusalama zinazohusiana na ujasusi (espionage),uzandiki (subversion),uhujumu (sabotage) na ugaidi (terrorism). Lakini jukumu la Idara hiyo si kukusanya taarifa hizo na kuzichambua tu bali pia kuzuwia matukio hayo yanayofahamika kama matishio ya usalama wa taifa..
 
Jana nilimsikia Mh. Rais kwenye Mkutano mmoja huko Sumbawanga nadhani akiwataka Mkuu wa mkoa na Viongozi wote Waende kusikiliza kero za Wananchi...

Nilimsikia akisema "Nikiondoka msinisindikize, mbaki kusikiliza kero za Wananchi"
Then nikamsikia akisema "Afisa Usalama wa Wilaya yuko wapi? Na wewe nenda pale...... Ilitakiwa ujue hizi changamoto na kuzizuia kabla.......!

So nadhani kazi ya Tiss sio tu ku report Ila pia kuzuia pia mabaya yasitokee .....
Naomba nikufahamishe na kukurekebisha kidogo. DSO huwa anaripoti kwa RSO na sio moja kwa moja kwa Rais
 
Hamna kitu hicho wewe. Sioni kazi ya TISS zaidi ya kufuatilia vyama vya upinzani vinafanya nini?. Report zote zinaibuliwa na wananchi mahala husika hakuna cha TISS wala usalama hapo


njoo unywe beer wewe mambo ya TISS waachie MAGUFULI na MAJAALIWA
 
WanaJF, mnakumbuka uchafu na uozo mwingi wa ufujaji wa fedha za umma ktk Halmashauri zetu zinazofichuliwa na Waziri Mkuu na wakati mwingine Rais Magufuli mwenyewe.

TISS wamejaa kila mahali nchini na nashindwa kuelewa kwanini hali hii itokee hadi viongozi wakubwa ndio wanakuja kufanya ufichuzi. Rejea Mkoa wa Morogoro na Singida ktk ziara za Majliwa.
Nimetoka kuangalia ya Nachingwea muda huu nafungua JF nakutana na huu uzi. Balaa, ile rais kuamua hadi kutembea sokoni na stand kunjustfy matumizi ya pesa ya miradi ya halmshauri basi ni tatizo.
 
WanaJF, mnakumbuka uchafu na uozo mwingi wa ufujaji wa fedha za umma ktk Halmashauri zetu zinazofichuliwa na Waziri Mkuu na wakati mwingine Rais Magufuli mwenyewe.

TISS wamejaa kila mahali nchini na nashindwa kuelewa kwanini hali hii itokee hadi viongozi wakubwa ndio wanakuja kufanya ufichuzi. Rejea Mkoa wa Morogoro na Singida ktk ziara za Majliwa.
Mbona nasikia Wakurugebzi wa hizo Hakmashauri nao ni Tiss?
 
Back
Top Bottom