NI IPI NAFASI YA MWANANCHI KUFIKISHA MAONI YAKE KWA SERIKALI IKIWA BUNGE LINAENDESHWA KWA HISIA ZA U

Oct 7, 2015
86
108
HABARI ZENU WAUNGWANA !?
siasa-300x206.jpg

Ni imani yangu umeianza vyema Jumatatu yako,na nusu ya pili ya mwezi may.Ni kwa muda sasa tumekuwa tukisikia na wakati mwingine kuona wawakilishi wetu kule bungeni wakisimama kidete kutetea maslahi ya vyama/chama chake kuliko zaidi anavyotetea shida na matatizo ya wananchi wake.

Hali hii haijaanza kwenye awamu hii ya tano na bunge hili la 11,hii ni tangu kwenye bunge la 10 na serikali ya awamu ya nne,chini ya rais mstaafu Jakaya Kikwete.Na imeanza kuota mizizi mikubwa kiasi hata wale walio bungeni wanahisi kazi yao kubwa ni kusupport either CCM ama UKAWA, pasipo kujali ni suala gani haswa linalojadiliwa.

Mahaba ya chama zaidi kuliko wananchi ambao ndio waajili wa mbunge ,yamekua imara zaidi kipindi hiki ambapo upinzani ndani ya nchii umekua kiasi kwamba sasa mahaba hayo yanatishia kuwepo kwa taifa moja la watu wamoja watakao na wanaosimama kwa umoja.

Maslahi na malengo ya taifa yamekuwa yakipewa nafasi ndogo zaidi na nguvu ndogo kwa wajumbe kuboresha Tanzania ya miaka 50 ijayo. Je sasa wananchi wa kawaida wakimbilie wapi kutoa maoni yao kwa maendeleo ya taifa lao.
 
Back
Top Bottom