Ni ipi nafasi ya mwanamke katika muziki wa taarab?

Kipilipili

JF-Expert Member
May 25, 2010
2,272
1,876
Taarab tangu kale imekua ikibadilika.kutoka taarab asilia hadi taarab"baada usasa leo".mabadiliko hayo ni pamoja na kumchora mwanamke akigombea wanaume,malaya,akijisifu kumpoka mwenzie mume,amedhalilishwa kwa kufanywa km kinyago kiwekwacho jukwaan kicheze ili kufurahisha watu hasa wanaume!,mavaz yamwekayo nusu uchi na kucheza kusiko na "adabu".napata waswas juu ya muziki huu na maadili ya binti zetu na pia nafac hasi apewayo mwanamke.mf nyimbo km KINYAGO CHA MPAPURE,SANAM LA MICHELINI,MWANAMKE KHULKA,PEMBE LA NG'OMBE n.k
 
Kila jambo ndugu yangu linakwenda na wakati, kwa maana kwamba wakati ulipo sasa kila kitu kipo wazi taarabu za zamani zilikuwa sana na ifadhi ya lugha ndio maana kama ujui maana ulikua huwezi kupenda taarabu, lakini sasa taarabu zipo wazi kabisa hakuna hifadhi ya lugha kabisaaa, Sasa kwa akina dada au mwanamke wa sasa hasa uswazi kwetu, ugumu wa maisha, wivu wa maendeleo nk ndio fani zilizokuwepo sio kujishughulisha mwiko, sasa basi mazingira hayo na taarabu hizi zinalingana ndio maana zinawapenzi wengi na washabiki. na ndio kwenye kipato wanachopata kwa kucheza na kuonyesha miili yao. Kuna kazi ya ziada kweli mabinti wanapotea na kupotoka. Sasa ikiwa hata vyombo vya habari vinashabikia mambo haya si hatari hii utasikia matangazo KANGA MOKO NJOO UONE WATOTO NYONGA TEKETEKE....... haya matangazo kama hayo si hamasa tosha kwa mabinti. Taarabu za sasa hamna kitu HAKUNA NAFASI YOYOTE KWA MAADILI
 
Nakuunga mkono Bi.George!ukiduhushi na kusoma kwa utuvu yale yaliyomo ndani ya taarab ya leo utagundua uozo na kuvizwa kwa maadili ya jamii.nini kifanyike sasa kama hali ipo kama hvyo?
 
Hakika kwa sie waarab, tuna asli zetu na sirka zenu hususan katika hii adaat .

Hakika unaposema tungo za taarab zinatakiwa sizungumzie MAPENZI tu na si vinginevyo.Mwimbaji anakua mmoja na wengine wanakuwa waitikiaji. Watazamaji wanatulia kwenye vitu kusikiliza ushairi uliomo katika wimbo huo na pale unapohisi umekugusa basi unasimama taratibu na kwenda kutunza pesa lakini sio kucheza kama ilivyo sasa

Sasa siku hizi huko Bongo unaona taarab watu wanaimba kuzungumzia siasa na mambo mengine ya kijamii wakati watu wanacheza kama dance na waimbaji wanafanya kama miziki ya kibara.

Kwa huko Tanzania unaweza kuipata Taarabu aslia japo kidogo kutoka kikundi cha malindi na Culture vya zanzibar na kile cha JKT mgulani
 
Back
Top Bottom