Ni ipi miti bora ya kilimo cha mbao?

Upo wapi? Kwa mkoani iringa wilaya ya mufindi. Miti aina ya mlingoti ndio bora zaidi. Kwanza inakua haraka. Pili mbao zake zinatumika katika uselemala. Ngoja tusubiri na wadau wengine wanasemaje kuhusu hilo

Sent using samsung galaxy grand prime pro
Hivi huko mufindi mashamba yapo je bei gani kwa eka?
 
Naomba nitoe kamchango kadogo, kuna kitu kinaitwa rotation time kwa kila mti, rotation time ni kipindi ambacho mti hufikia maturity kwa ajili ya kutoa mbao.

1. Eucalyptus ni kama miaka 23
2. Pines ( zilizo nyingi) ni miaka 23 pia
3. Cyprus ni 26
4. Mtiki ni 26 hivi

Naweza kuwa nimekosea kidogo, ila rotation time iko over 20yrs kwa miti mingi. Chini ya hapo utapata kwa kutumia GMO au improved seeds.
acha kupotosha watuuu, paina miaka 6 na kuendelea unavuna!! tena mbao zilizokomaa kabsaa.
 
Data za miaka 7 na mitiki miaka 15 umepata wapi?, mimi nimezitoa TTSA. Bila kutumia improved seeds/GMO huvuni miti ya mbao kwa ubora unaotakiwa chini ya miaka 20. Mitiki na Cyprus inakula miaka ya kutosha. Labda acrocarpus unaweza vuna baada ya miaka kumi.

Ila kama unavuna kwa kuibaka miti sawa, hata miaka miwili inawezekana.

Hizi data ametoa TWAWEZA ni sahihi kabisa ila pia inategemea hali ya udongo
Na Hali ya hewa
 
Je, eucalyptus inakubali kupandwa mkoa wa Kigoma? Naona ipo mingi na nilikua na mpango wa kupanda. Na je, soko lake likoje?
 
Hivi huko mufindi mashamba yapo je bei gani kwa eka?

Hivyo inarange kutoka 100,000 hadi 500,000 kwa shamba bila Miti idadi ya hekali zinazingatiwa zaidi.
Pia bei inategemea na vitu vingi kama ubora wa ardhi, umbali toka barabarani na miundombinu ya ardhi yaani kama ni mlima mkali au tambalale.
 
Back
Top Bottom