Ni ipi miti bora ya kilimo cha mbao?

SWEET RIZIKI

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
288
385
Wakuu, kichwa habari chahusika.

Wenye uzoefu na Kilimo cha miti ya mbao tunaomba kujuzwa ni miti gani bora yenye kutoa mbao nyingi.
Inakua kwa muda gani.

Baadhi ya miti michache nilowahi kusikia ni Sapras, Mitiki ila sijui ABC's zake.

Natanguliza shukrani.
 
Wakuu kichwa habari cha husika.
Wenye uzoefu na Kilimo cha mbao tunaomba kujuzwa ni miti gani bora yenye kutoa mbao nyingi.
Inakua kwa muda gani.

Baadhi ya miti michache nilowahi kusikia ni Sapras, Mitiki, Gravilia ila sijui ABC's zake.
Natanguliza shukrani.
Masahihisho: Kilimo cha miti ya mbao na sio kilimo cha mbao .... by the way hiyo MITI BORA ndo penye UTATA hapo
 
Kuna mtu alitoa uzi humu nikawasiliana nae yupo morogoro anauza miti mbali mbali ya mbao, tena bei chee kabisa.
 
Wakuu kichwa habari cha husika.
Wenye uzoefu na Kilimo cha mbao tunaomba kujuzwa ni miti gani bora yenye kutoa mbao nyingi.
Inakua kwa muda gani.

Baadhi ya miti michache nilowahi kusikia ni Sapras, Mitiki, Gravilia ila sijui ABC's zake.
Natanguliza shukrani.
Naomba nitoe kamchango kadogo, kuna kitu kinaitwa rotation time kwa kila mti, rotation time ni kipindi ambacho mti hufikia maturity kwa ajili ya kutoa mbao.

1. Eucalyptus ni kama miaka 23
2. Pines ( zilizo nyingi) ni miaka 23 pia
3. Cyprus ni 26
4. Mtiki ni 26 hivi

Naweza kuwa nimekosea kidogo, ila rotation time iko over 20yrs kwa miti mingi. Chini ya hapo utapata kwa kutumia GMO au improved seeds.
 
Hiyo miaka umetia chumvi kwa sana,pine hiyo miaka 7 watu wanavuna na mitiki ni miaka 15 sio 26 ingekua hakuna mtu anapanda hyo miti.
 
Ni kweli kwa IMPROVED SEEDS. You can real harvest in 10 years. Swali langu kwa mtoa post labakia anaposema MITI BORA alimaanisha nini?
 
Hiyo miaka umetia chumvi kwa sana,pine hiyo miaka 7 watu wanavuna na mitiki ni miaka 15 sio 26 ingekua hakuna mtu anapanda hyo miti.
Data za miaka 7 na mitiki miaka 15 umepata wapi?, mimi nimezitoa TTSA. Bila kutumia improved seeds/GMO huvuni miti ya mbao kwa ubora unaotakiwa chini ya miaka 20. Mitiki na Cyprus inakula miaka ya kutosha. Labda acrocarpus unaweza vuna baada ya miaka kumi.

Ila kama unavuna kwa kuibaka miti sawa, hata miaka miwili inawezekana.
 
Naomba nitoe kamchango kadogo, kuna kitu kinaitwa rotation time kwa kila mti, rotation time ni kipindi ambacho mti hufikia maturity kwa ajili ya kutoa mbao.
1. Eucalyptus ni kama miaka 23
2. Pines ( zilizo nyingi) ni miaka 23 pia
3. Cyprus ni 26
4. Mtiki ni 26 hivi
Naweza kuwa nimekosea kidogo, ila rotation time iko over 20yrs kwa miti mingi. Chini ya hapo utapata kwa kutumia GMO au improved seeds.
Ahsante mkuu kwa mchango wa kitaalam hiyo ni Bank ya uhakika. Mbona niliwahi sikia ni kama miaka 10 - 15.
 
Yenye mazao mengi, mbao imara na inayokomaa kwa muda mfupi mkuu.
Miti ya mbao inayokomaa kwa haraka mara nyingi hutokana na MBEGU ZILIZOBORESHWA yaani IMPROVED TREE SEEDS lakini kwa uchache sana yaweza kutokana na HALI YA HEWA, HALI YA UDONGO na KIASI CHA MAJI ambacho mti huo wapata.

Kwa mti kuzaa mazao mengi mara nyingi yatokana na AINA YA MBEGU hasahasa IMPROVED TREE SEEDS na BETTER TENDING OPERATIONS (matunzo bora tangu kitaluni [tree nursery] hadi shambani [plantation ])

Lakini pia mazao mengi yaweza tokana na kuusubiria mti hadi ufikie ROTATION AGE (time) yaani KUKOMAA KWA MTI tayari kwa kuvunwa, maana wakulima wengine huvuna miti yao ikingali MICHANGA (immature trees) hiyo hupelekea MAZAO MACHACHE na MBAO DHAIFU/ZISIZO IMARA

Mwisho, MBAO IMARA moja ya sababu ishaainishwa hapo juu na nyingine ni kuwa na BETTER TREE NURSERY MANAGEMENT & TENDING OPERATIONS ( usimamizi bora wa kitalu cha miti na shamba la miti) bila kusahau AINA YA MTI (tree species)

Kwa ushauri zaidi waone

a)WAKALA WA MBEGU WA TAIFA (Tanzania Tree Seeds Agency - TTSA)

b)TAASISI YA UTAFITI WA MISITU TANZANIA (Tanzania Forestry Research Institute- TAFORI)

c)TAASISI YA UENDELEZAJI MISITU (Forestry Development Trust-FDT)

d)MPANGO WA UPANDAJI MITI (Private Forestry Programme-PFP)

Note: Taasisi mbili za mwanzo (TTSA na TAFORI) ni TAASISI ZA TAIFA na mbili za mwisho (FDT na PFP) ni TAASISI ZA KIGENI
 
Njoo mafinga ninauza miti ya mbao aina ya piner ukitaka yakufuga ipo heka ni kaki 9 miti ina umri miaka mi nne
 
Naomba nitoe kamchango kadogo, kuna kitu kinaitwa rotation time kwa kila mti, rotation time ni kipindi ambacho mti hufikia maturity kwa ajili ya kutoa mbao.

1. Eucalyptus ni kama miaka 23
2. Pines ( zilizo nyingi) ni miaka 23 pia
3. Cyprus ni 26
4. Mtiki ni 26 hivi

Naweza kuwa nimekosea kidogo, ila rotation time iko over 20yrs kwa miti mingi. Chini ya hapo utapata kwa kutumia GMO au improved seeds.

Kila aina ya mti hutegemea na udongo wa sehemu husika
 
Mimi nashuhudi kutoka field (Shambani). Pines ni miaka 7-8 imekomaa vizuri kwa kuvunwa. Hiyo ya miaka 15 sijawah kukutana nayo.
Kiongozi hiyo miaka 7-8 kwa pinus yawezekana kwa IMPROVED TREE SEEDS .... lakini kwa UNIMPROVED ONES muda huo bado ni IMMATURE TREES .... japo mtaiona imekomaa ....

Ukitaka uione pinus ilofika miaka 10 na zaidi nenda SAO HILL FOREST PLANTATION
 
Mimi nashuhudi kutoka field (Shambani). Pines ni miaka 7-8 imekomaa vizuri kwa kuvunwa. Hiyo ya miaka 15 sijawah kukutana nayo.
Hapa umetupa mwangaza, tukuombe utupie na kapicha kidogo ka Pine au ni ile inazaa mbegu bila matunda. Pia vipi hiyo ni ya kisasa au ya mkoloni.

Ahsante
 
Miti ya mbao inayokomaa kwa haraka mara nyingi hutokana na MBEGU ZILIZOBORESHWA yaani IMPROVED TREE SEEDS .... lakini kwa uchache sana yaweza kutokana na HALI YA HEWA, HALI YA UDONGO na KIASI CHA MAJI ambacho mti huo wapata .....

Kwa mti kuzaa mazao mengi mara nyingi yatokana na AINA YA MBEGU hasahasa IMPROVED TREE SEEDS na BETTER TENDING OPERATIONS (matunzo bora tangu kitaluni [tree nursery] hadi shambani [plantation ]) ....

Lakini pia mazao mengi yaweza tokana na kuusubiria mti hadi ufikie ROTATION AGE (time) ... yaani KUKOMAA KWA MTI tayari kwa kuvunwa, maana wakulima wengine huvuna miti yao ikingali MICHANGA (immature trees) .... hiyo hupelekea MAZAO MACHACHE na MBAO DHAIFU/ZISIZO IMARA ....

Mwisho, MBAO IMARA moja ya sababu ishaainishwa hapo juu .... na nyingine ni kuwa na BETTER TREE NURSERY MANAGEMENT & TENDING OPERATIONS ( usimamizi bora wa kitalu cha miti na shamba la miti) ... bila kusahau AINA YA MTI (tree species) ...

Kwa ushauri zaidi waone ...

a)WAKALA WA MBEGU WA TAIFA (Tanzania Tree Seeds Agency - TTSA) ...

b)TAASISI YA UTAFITI WA MISITU TANZANIA (Tanzania Forestry Research Institute- TAFORI) ...

c)TAASISI YA UENDELEZAJI MISITU (Forestry Development Trust-FDT) ...

d)MPANGO WA UPANDAJI MITI (Private Forestry Programme-PFP) ....

Note: Taasisi mbili za mwanzo (TTSA na TAFORI) ni TAASISI ZA TAIFA na mbili za mwisho (FDT na PFP) ni TAASISI ZA KIGENI

Kaka asante kwa kusaidia kutoa elimu hii, wadau wengi wanapata taarifa toka vyanzo ambavyo si sahihi, matokeo tunapata mazao feki yasiyo na ubora.

Naomba niseme, ukitaka taarifa sahihi za miti pita TTSA Iringa, TTSA Lushoto, TTSA Morogoro na TTSA Arusha. Tusipoteze muda, wakati majibu sahihi yapo ktk taasisi hizo. Toa taarifa na habari za kisayansi kwa kutoa reference official. Kinyume na hivyo ujue unadanganya.
 
Back
Top Bottom