Ni ipi mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kutatua tatizo la ajira nchini Tanzania?

Mtamba wa Panya

JF-Expert Member
Aug 6, 2017
695
1,712
Habari ndugu zangu,

Sote tunafahamu ukubwa wa tatizo la upatikanaji wa ajira nchini kwa miaka ya hivi karibuni. Kwa kipindi tulichopo, hakuna tofauti baina ya msomi wa masters na aliyeishia darasa la pili, maana wote wanakimbilia kazi primitive zisizohitaji ujuzi wowote wa kielimu (mfano kuendesha bajaji).

Nchi zote zinazojitambua na zinazojali watu wake, zimeweka kipimo maalumu cha kutambua idadi ya wananchi wake wasio na ajira, kipimo hiki huitwa unemployment rate ( a.k.a unemployment index). Je, Tanzania kipimo hiki tunacho? Au hatuoni umuhimu wa kujua idadi ya nguvukazi isiyotumika kukuza uchumi wa nchi i.e unutilized human resource.?

Kutokana na ukubwa wa tatizo naomba kufahamu, je, serikali yetu ya awamu ya tano ( a.k.a serikali ya wanyonge ) ina mipango gani ya muda mfupi na muda mrefu katika kutatua tatizo hili?

Najua serikali haiwezi kukosa mipango katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo mfano kwenye suala la ukusanyaji mapato, imeweka target ya kukusanya Tsh 2,000,000,000,000/= kwa mwezi.

Je, vipi kuhusu ajira hasa kwa vijana?

Ahsante!
 
HAKUNA AWAMU BUTU KAMA HII YA 5 HASA KATIKA SUALA NYETI KAMA LA AJIRA MBALI MBALI ZA SERIKALINI
 
Naona nyuzi hizi za wahitimu kukosa ajira zimekuwa nyingi sana tutamaliza miaka mitano bila maandamano kweli kama mwanzo tu hali hii
 
Tutamkumbuka MAGUFULI kwa anavyo haribu fursa za kiuchumi kwa kuwawekea wawekezaji mazingira magumu ya kibiashara.
Buriani Quality Group, Buriani Fast Jet, Precision Airways, Buriani Habari Cooperation, Buriani miradi ya gesi...... Nyie wote mmetuletea mtaani watu wasio na ajira
 
Habari ndugu zangu,

Sote tunafahamu ukubwa wa tatizo la upatikanaji wa ajira nchini kwa miaka ya hivi karibuni. Kwa kipindi tulichopo, hakuna tofauti baina ya msomi wa masters na aliyeishia darasa la pili, maana wote wanakimbilia kazi primitive zisizohitaji ujuzi wowote wa kielimu (mfano kuendesha bajaji).

Nchi zote zinazojitambua na zinazojali watu wake, zimeweka kipimo maalumu cha kutambua idadi ya wananchi wake wasio na ajira, kipimo hiki huitwa unemployment rate ( a.k.a unemployment index). Je, Tanzania kipimo hiki tunacho? Au hatuoni umuhimu wa kujua idadi ya nguvukazi isiyotumika kukuza uchumi wa nchi i.e unutilized human resource.?

Kutokana na ukubwa wa tatizo naomba kufahamu, je, serikali yetu ya awamu ya tano ( a.k.a serikali ya wanyonge ) ina mipango gani ya muda mfupi na muda mrefu katika kutatua tatizo hili?

Najua serikali haiwezi kukosa mipango katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo mfano kwenye suala la ukusanyaji mapato, imeweka target ya kukusanya Tsh 2,000,000,000,000/= kwa mwezi.

Je, vipi kuhusu ajira hasa kwa vijana?

Ahsante!
Kama mtoa mada umeshindwa kutambua fursa za ajira zinazotengenezwa na serikali hii basi unapaswa kurudi shuleni.
Mradi mkubwa wa umeme utafungua fursa za ajira kwa sababu kwanza utavutia uwekezaji wa viwanda kwa sababu nishati itakuwa inapatikana kwa uhakika. Viwanda vikifunguliwa ajira zitatengenezwa nyingi sana. Pili viwanda vilivyopo vitaweza kuzalisha bidhaa kwa gharama nafuu sana na kufanya bidhaa zetu kupiku soko kwa sababu ya kuuzwa kwa bei nafuu. Bidhaa za Viwanda vyetu kwa sasa zinashindwa kushindana bidhaa za nje kwa sababu gharama za utengezaji ziko juu. Iwapo umeme utapunguza gharama za uzalishaji utafanya bidhaa za Tanzania kuuzwa kwa wingi sana katika masoko ya nchi jirani. Hivyo kuongeza uzalishaji kwa maana hiyo viwanda vitaajiri watu zaidi, na biashara nayo itapanuka na kutoa ajira zaidi.
SGR, ujenzi wa SGR ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi. Kwa sababu mosi reli hii itaiunga Tanzania na nchi jirani kama vile DRC, Burundi Uganda and Rwanda. Hii itafanya bidhaa za Tanzania kusafirishwa kwa gharama nafuu sana na kuteka masoko katika ukanda huu.
Pili reli hii itasaidia katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kutokana na upatikaji wa masoko ya uhakika vijana wengi wataajiriwa.
Ufufuaji wa viwanda vya zamani. Serikali inampango kabambe wa kufufua na kuendesha viwanda vilivyokufa baada ya kupatiwa wawekezaji. Viwanda hivi ni kama cotton ginnery, viwanda vya nguo, viwanda vya ngozi. Ufufuaji wa viwanda hivi utatengeneza ajira.

Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
 
Bint Usisahau kupita Lumumba ukachukue buku7 yako.
 
Umetoa majibu ya kisiasa.

Bado hujataja mipango ya serikali kutatua changamoto ya ajira.

Mfano kijana ana kipaji cha ubunifu au wazo la ajira, serikali inamsaidia vipi? Au kazi ya serikali ni kukusanya mapato tu?
 
hii ni hoja ya muhimu sana , na pengine ni suala pasua kichwa kwa serikali hii na nchi zilizoendelea. mi nina hoja 2
1. watu wachangie mawazo yao kwasababu kwa kweli kwa mtu aliyemaliza chuo akakosa ajili ni stress kwa kwenda mbele
hasa ukizingatia muda mrefu amepoteza shule na mambo ya mtaani hayajui.
2. ubunifu na kujiajiri ni kipaji kama ilivyo kuimba, hivyo watu waliojariwa mawazo ya ubunifu wayawasilishe wizara ya kazi na ajira na nna uhakika kama wazo liko vizuri watawezeshwa.
3. Serikali itenge fedha za miradi ya kurahisisha kujiajiri na kuajiriwa mfano mwalimu nyerere alifungua mashamba akaweka miundombinu ya maji, yale mashamba mpaka leo yanaajiri watu wengi sana, kwanini tusiongeze mashamba kama hayo, hata kama maji hayopo karibu vichimbwe visima, kwani mji kama dodoma maji yake yanatoka wapi ? si visima.
4. wazo la Magufuli la kujenga viwanda lilikuwa zuri naona kama watu wamemshauri ahamasishe wafanyabiashara ndo wajenge, ni sawa na si sawa, kuna viwanda serikali ingejenga na kuvipangisha. mfano kule pwani viwanda vya samaki vingejengwa halafu vifaa bora vya uvuvi vingegawiwa kwa vikundi vya vijana wasio na ajira.
5. maeneo ya kufugia yangetengwa na kuboreshwa watu wafuge hata kimasai kisha vianzishwa viwanda vya kuchakata nyama na maziwa, we angalia NIDO ilivyo jaa madukani wakati tunaongoza kwa mifugo AFRIKA. we angalia nyama za makopo zinatoka nje wakati ng;ombe wamejaa. uarabuni kuna soko la kufa mtu la nyama.
 
Mzee baba ni umbwa kama umbwa zingine! Hana mbinu za kuajiri watu! Labda tujaribu 2026! Ila vijana nyie wajinga sana tukiwa vyuoni na nyie huwa mko msitari wa mbele kuimba mapambio ya CCM wacha muipate fresh!
 
Kama mtoa mada umeshindwa kutambua fursa za ajira zinazotengenezwa na serikali hii basi unapaswa kurudi shuleni.
Mradi mkubwa wa umeme utafungua fursa za ajira kwa sababu kwanza utavutia uwekezaji wa viwanda kwa sababu nishati itakuwa inapatikana kwa uhakika. Viwanda vikifunguliwa ajira zitatengenezwa nyingi sana. Pili viwanda vilivyopo vitaweza kuzalisha bidhaa kwa gharama nafuu sana na kufanya bidhaa zetu kupiku soko kwa sababu ya kuuzwa kwa bei nafuu. Bidhaa za Viwanda vyetu kwa sasa zinashindwa kushindana bidhaa za nje kwa sababu gharama za utengezaji ziko juu. Iwapo umeme utapunguza gharama za uzalishaji utafanya bidhaa za Tanzania kuuzwa kwa wingi sana katika masoko ya nchi jirani. Hivyo kuongeza uzalishaji kwa maana hiyo viwanda vitaajiri watu zaidi, na biashara nayo itapanuka na kutoa ajira zaidi.
SGR, ujenzi wa SGR ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi. Kwa sababu mosi reli hii itaiunga Tanzania na nchi jirani kama vile DRC, Burundi Uganda and Rwanda. Hii itafanya bidhaa za Tanzania kusafirishwa kwa gharama nafuu sana na kuteka masoko katika ukanda huu.
Pili reli hii itasaidia katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kutokana na upatikaji wa masoko ya uhakika vijana wengi wataajiriwa.
Ufufuaji wa viwanda vya zamani. Serikali inampango kabambe wa kufufua na kuendesha viwanda vilivyokufa baada ya kupatiwa wawekezaji. Viwanda hivi ni kama cotton ginnery, viwanda vya nguo, viwanda vya ngozi. Ufufuaji wa viwanda hivi utatengeneza ajira.

Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
Porojo as usual.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom