Ni ipi kashfa ya kujadili kati ya hawa makatibu wakuu wawili?


N

Njaare

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2010
Messages
1,080
Points
1,195
N

Njaare

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2010
1,080 1,195
Wana JF!

Nimekuwa nikifuatilia mijadala inayoendelea kuhusu Katibu Mkuu wa CHADEMA kuwa na kadi ya CCM. Kwa mujibu wa katiba ya CCM, mwanachama atakoma uanachama wa CCM kama atajiunga na chama kingine na sii kurudisha kadi.

Pia kwa siku za hivi karibuni, tumesikia kuwa shehana kubwa ya meno ya tembo imekamatwa huko mashariki mwa Asia. Tumesikia kuwa meli iliyosafirisha shehena hiyo inamilikiwa na Katibu mkuu wa CCM. Sheria zetu zinaitaka serikali kuvitaifisha vyombo vitakavyojihusisha kusafirisha maliasili zilizopatikana kwa njia haramu (Ujangili). Mpaka leo hatujapata taarifa yoyote kuhusu kutaifishwa kwa meli hiyo.

Je, kati ya makatibu wakuu hawa ni nani ana kashfa ya kujadili? Ni nani atakuwa anajihusisha na uhalifu?
 

Forum statistics

Threads 1,285,946
Members 494,834
Posts 30,880,154
Top