Ndugu wadau wa sheria nmekuwa na kesi ya madai, mimi nikiwa mdai. Miezi 6 iliyopita nilitafuta fundi welding nikampa kazi na pesa jumla tsh 1,200,000 ili anitengenezee fens za kuweka juu ya ukuta wa ngome ya nyumbani kwangu. Kilichotokea fundi hakufanya chochote km nilivyotarajia. Nilichukua hatua za kuwasiliana na ndugu wa karibu yake maana n mtu tunayefahamiana ili watusaidie kutatua shida hiyo haikufanikiwa hivyo baadae ikanibidi kufungua kesi mahakamani ambapo mdaiwa alifika na kukiri na hivyo hakimu kumuamuru alipe pesa hiyo ndani ya siku 30.
Ninaomba kupewa uelewa juu ya kesi kama hii je ikiwa mtu huyu hatolipa chochote hadi hizo siku 30 zitakapokwisha nifanyeje??
Pili, hakimu aliniambia baada ya hizo siku ikiwa mdaiwa hatokuwa amefanya chochote bs niende nikakazie hukumu, je hii inamaana gani??
Tatu, hakimu aliniuliza km mdaiwa ana mali zozote anazomiliki, je hii ina maana gani? Na km hana mali mwendelezo wa kesi hapo utakuaje au ndo nakuwa nmepoteza haki yangu?