Ni ipi adhabu ya Mbunge aliyevunja kiapo alichoapa bungeni?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,285
8,197
Habari za leo ndugu zangu,

Natumai nyote muwazima.

Mimi ndugu yenu nimekua nikiona mara baada ya viongozi kuteuliwa na Rais, inatengwa siku tena maalum ya kuwaapisha. Katika hiyo siku nimekua nikiona wanainua mkono mmoja juu alafu kuna maneno fulani wanayatamuka. Na mwisho wanamalizia kwa kusema "Eee mwenyezi Mungu nisaidie".

Lakini pia kwenye bunge la kwanza la awamu ya tano, niliona spika wa bunge akiwaapisha wabunge waliochaguliwa na wananchi. Vivyo hivyo pia naliona kazi ngumu sana ya kuwaapisha ikifanyika. Mbunge mmoja alikua akiinua mkono mmoja juu, kuna maneno alikua akiyasoma alafu mwisho anamalizia kwa kusema "eee mwenyezi Mungu nisaidie".

Na wakati wa kuapa nalikua nikisia baadhi ya wabunge wakisema nitalitumikia taifa langu kwa uaminifu mkubwa ndani na nje ya nchi.
Nitaheshimu katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Sasa hapa chini nina maswali machache yanayohusiana na maada nzima niliyo ielezea kwa kina hapo juu.

Swali 1:
Je, katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania inaruhusu mbunge au kiongozi yeyote kumtukana Rais wa Jamuhuri akiwa nje ya mipaka ya Tanzania.

Na je, mbunge au kiongozi aliye apa inatakiwa apewe adhabu gani akimtukana au kumdhihaki Rais?

Swali 2;
Je, katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania inaruhusu mwananchi au kiongozi kuwasema vibaya viongozi wa taifa lake kwa mataifa au kwa viongozi wa mataifa mengine.

Na je, mbunge au kiongozi aliye apa inatakiwa apewe adhabu gani anapo lisema taifa vibaya kwa mataifa mengine?

Swali 3:
Je, katiba ya jamuhuri wa Muungano wa Tanzania inaruhusu mwananchi au kiongozi kulisema vibaya taifa lake kwa mataifa au kwa viongozi wa mataifa mengine.

Na je, mbunge au kiongozi aliyeapa inatakiwa apewe adhabu gani anapowasema vibaya viongozi wa taifa lake kwa mataifa mengine?

Swali 4:
Ni muhimili upi unatakiwa kutoa adhabu hizo? Je, ni ule ulio mwapisha au ni mahakama?

Swali 5:
Je, yule aliyemwapisha anayo mamlaka ya kwenda kumshitaki kiongozi huyo aliyelisema taifa na Rais vibaya? Je aliyemwapisha anayo mamlaka ya kuikumbusha mahakama punde inapochelewa kutoa maamuzi?

Swali 6:
Je, aliyesemwa vibaya ikiwa labda ni serikali yenyewe au ni Rais au ni kiongozi mwingine. Je, ana haki ya kwenda kushitaki mahakamani au kuwakumbushia kuharakisha shauri hilo?

Swali 7:
Kama tunavyo jua pia kama ikitokea kuna kiongozi labda amezuia fedha ambazo benki ya dunia (WB) au Taasisi ya fedha ya Kimataifa (IMF) either kwa kuiandikia benki ya dunia au IMF barua bila kuwashirikisha wananchi ambao hizo fedha zinawalenga wao au bila kuishirikisha serikali au bila kulishirikisha bunge. Je, wananchi wanayo haki yeyote ya kumpeleka mahakamani mtu huyo. Au Je wanayo haki ya kukumbushia kwa mahakama kama inachelewesha shauri.

Na je kiongozi wa namna hiyo anaye wasaliti wananchi adhabu yake ni ipi?

Wakuu nahitaji majibu ya mwaswali haya. Nataka kuelewa jinsi ambavyo mambo yanaenda katika siasa.

Wakuu nimeuliza maswali hayo kwasababu kuna viongozi na baadhi ya wa Tanzania wamekuwa wanaitukana serikali kwa vile wako nchi za nje na wengine wamekuwa wakimdhihaki Rais wakiwa nje ya nchi. Lakini pia kuna viongozi wengine wamekuwa wakiifanyia lafu serikali ya wananchi wa Tanzania. Hao viongozi wamekuwa wakishirikiana na mabeberu kuzishika ndege zetu, muda mwingine wamekuwa wakishirikiana na mabeberu kuzuia na kukwamisha fedha za maendelea ambazo tumekuwa tukipewa na Taasisi za fedha za kimataifa.

Na ili hali watu hao wanajulikana, tupo nao, sasa kwanini wasipewe adhabu kwasababu wanaenda kinyume na viapo vyao?

Wenu katika ujenzi wa taifa

Meneja wa Makampuni
 
Wakuu nisaidieni majibu ya swali langu. Najua mpo wanasiasa mbali mbali humu. Nisaidieni majibu mwanasiasa mwenzenu.
 
Wakuu nisaidieni majibu ya swali langu. Najua mpo wanasiasa mbali mbali humu. Nisaidieni majibu mwanasiasa mwenzenu.
Kwamba na wewe umepitishwa na chama chako hivyo unategemea kwenda kufanya mojawapo ya hayo uliyoorodhesha hapo?by the way.

Ukiwa kama ni m'bunge uliyeapishwa pale mjengoni na ukawa kambi ya upinzani jua ukifanya mojawapo ya hayo utatolewa nje ya ukumbi na kufunguliwa mashtaka either uhujumu uchumi or uhaini au utatishiwa amani uunge juhudi kisha watakusubiri kwenye kura za maoni.zaidi ukiwa na access zakuwapata Mashinji, Mtulia, Mtolea, Lijuakali na wengineo utawauliza kuhusu hii theory, huko walipo vichwa vinawauma hawajui waliunga juhudi au walivunja juhudi.

Lah kama ni wa chama tawala mtafute kijana wa kuitwa Makonda/Bashite atakupa taarifa za madhara ya kumdharau boss wako anayekuweka mjini.hope nimesaidia kidogo japokuwa mimi siyo mwanasiasa!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba na wewe umepitishwa na chama chako hivyo unategemea kwenda kufanya mojawapo ya hayo uliyoorodhesha hapo?by the way.......

Ukiwa kama ni m'bunge uliyeapishwa pale mjengoni na ukawa kambi ya upinzani jua ukifanya mojawapo ya hayo utatolewa nje ya ukumbi na kufunguliwa mashtaka either uhujumu uchumi or uhaini au utatishiwa amani uunge juhudi kisha watakusubiri kwenye kura za maoni.zaidi ukiwa na access zakuwapata Mashinji,Mtulia,Mtolea,Lijuakali na wengineo utawauliza kuhusu hii theory...
Ahsante kwa mchango mkuu
 
Kama kionozi anafanya vitu vibaya hakuna sehemu katiba ina sema kumkosoa rais wa nchi ni kosa ila kuitukana nchi ndio shida
 
Huyo atakuwa ni msaliti na hukumu ya msaliti Ni kifo tu haina mjadala
Wewe ni nani hadi utoe hukumu ya kifo kwa mwananchi mwenzako?

Je unajua kuwa ni mahakama pekee inayoweza kutoa hukumu ya kifo kwa mwananchi yeyote atakayeonekana amefanya kosa la jinai, linalostahili adhabu hiyo?
 
Kwamba na wewe umepitishwa na chama chako hivyo unategemea kwenda kufanya mojawapo ya hayo uliyoorodhesha hapo?by the way.......

Ukiwa kama ni m'bunge uliyeapishwa pale mjengoni na ukawa kambi ya upinzani jua ukifanya mojawapo ya hayo utatolewa nje ya ukumbi na kufunguliwa mashtaka either uhujumu uchumi or uhaini au utatishiwa amani uunge juhudi kisha watakusubiri kwenye kura za maoni.zaidi ukiwa na access zakuwapata Mashinji...
Mkuu nimeuliza maswali hayo kwasababu kuna viongozi na baadhi ya wa Tanzania wamekuwa wanaitukana serikali kwa vile wako nchi za nje na wengine wamekuwa wakimdhihaki Rais wakiwa nje ya nchi. Lakini pia kuna viongozi wengine wamekuwa wakiifanyia lafu serikali ya wananchi wa Tanzania.

Hao viongozi wamekuwa wakishirikiana na mabeberu kuzishika ndege zetu, muda mwingine wamekuwa wakishirikiana na mabeberu kuzuia na kukwamisha fedha za maendelea ambazo tumekuwa tukipewa na Taasisi za fedha za kimataifa.

Na ili hali watu hao wanajulikana, tupo nao, sasa kwanini wasipewe adhabu kwasababu wanaenda kinyume na viapo vyao?
 
Wewe ni nani hadi utoe hukumu ya kifo kwa mwananchi mwenzako?

Je unajua kuwa ni mahakama pekee inayoweza kutoa hukumu ya kifo kwa mwananchi yeyote atakayeonekana amefanya kosa la jinai, linalostahili adhabu hiyo?
Ndio maana nilimuuliza hilo lipo kwenye katiba.
 
Back
Top Bottom