Ni inchi gani ikitolewa Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa imara?

jiwekuu770

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
2,247
1,634
Habari,

EAC ilianza miaka na kuvunjika 1978, kwa kutokea kwa vita ya tanzania n Uganda. Miaka 40 baadaye EAC imekua dhaifu na iliyovurugwa kuliko jumuiya nyingine yoyote. Kifupi haina muelekeo ; wala mpango wa kuileta pamoja. Imeenda mbali na nje kabisa ya mategemeo na malengo

Nini yalikua malengo ya jumuiya hii

- Common market/Soko la pamoja-Hapa ndipo maigizo yanapoanzia Mwaka 2020 kenya ilipiga marufuku bidhaa za chakula kama mahindi kutoka tanzania na uganda....tupo bado kwene common market? Sidhan. Hili na visa vingi vilivyotokea tz na kenya,
Kenya na uganda!! Pasikuusahau mgogoro wa kisiwa wa uganda na kenya ktk ziwa victoria.

- Common language/Lugha ya pamoja- swahili ni lugha ya pili kenya kuongelewa na idadi kubwa ya wakenya
Ikiwa n lugha ya kwanza tanzania ,ikiongelewa kama lugha ya taifa
  • Wakat uganda ni portion ndogo sana ikiongelewa
  • Rwanda na Burundi??
  • South Sudan? Hatujui kama wa hata idea of what going on
  • Common currency/fedha moja hapa ndyo kizungumkuti hamna progress hata ya 1% towards common currency !! Swali je n kweli kwamba hizi nchi ziko huru au n shinikizo kutoka magharibi

- One nation/nchi moja EAF STATE hii ni kazi kuliko hata ngamia kupenya kwenye tundu la sindano

YALIYOJIRI
Kenya imekua ikijitahid kuikandamiza Tanzania ikihofia itachukuliwa nafasi yake ya sasa As Tanzania the East africa economic giant
Rwanda imekua ikifanya spying wa majiran zake.
Burundi imekua inashindwwa hata kutoa ada.
S.Sudan haielewi hata kinachoendelea.

Unadhan tulikosea wap?? Au tutoe nchi gan?

East africa ya nchi tatu ilikua strong na powerful kuliko ya sasa


zitto junior Mshana Jr Allan Clement abackuk abagabo Abawali Baba Farheen Hit Man 47 hiltonh247 Netanyauu KAGAMEE kenyanah TANZANIA PATRIOT South Sudan Uganda Patriot
 
Pamoja na madhaifu bado kuna umuhimu wake (sahau kuhusu kutozingatiwa protocols)
-nasafiri ndani ya jumuiya kwa urahisi tofauti na kusingekua na jumuiya
-kufanya biashara (sahau written inter trading protocols😅)
Yangu makubwa ni hayo
 
Tunafanya nazo biashara na kusafiri kirahisi isitoke hata moja, tunafaidika SANA, SADC na EAC, hapana wasiondoe hata moja.
Natamani hata DRC ingetumbukizwa humu.

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Tunafanya nazo biashara na kusafiri kirahisi isitoke hata moja, tunafaidika SANA, SADC na EAC, hapana wasiondoe hata moja.
Natamani hata DRC ingetumbukizwa humu.

Everyday is Saturday.............................. :cool:
DRC ilishaomba na inajadiliwa naamini soon itakuwa mwanachama
 
Hii EAC ni ya wanasiasa tuu, kwenye watendaji na utendaji wa mambo kama usimamizi wa sheria na kanuni mambo ni yale yale na ndio maana kila siku nchi wanachama wanaanzisha vikwazo vyengine vya biashara visivyo vya kiushuru (NTBs) suala ambalo linadhorotesha maendeleo ya sekta binafsi kufanya biashara ya ndani ya ukanda baina ya nchi wanachama.

Kila uchao nchi washirika wanakaa vikao kupitia na kujadiliana namna ya kutokomeza changamoto mbalimbali, Tayari hadi sasa Kenya na Tanzania wameshakaa mara 4 na ya tano ndio hii ya tarwhe 26 hadi 30 Mei, 2021 walichokaa Arusha Tz katika ukumbi wa mikutano AICC ARUSHA.
 
Tunafanya nazo biashara na kusafiri kirahisi isitoke hata moja, tunafaidika SANA, SADC na EAC, hapana wasiondoe hata moja.
Natamani hata DRC ingetumbukizwa humu.

Everyday is Saturday.............................. :cool:

DRC ILipropose kujoin in EAC block!! Plus somalia
Nafikir bado wanareview
 
Zanzibar syo nchi mkuu, zanzibar ni sehem ya tanzania
Kama ilivo tanganyika zote zinaunda Tanzania

So TANZANIA IPO EAC BLOCK YES
Zanzibar ni nchi, ndio maama ina serikali yake, (SMZ - Serikali ya Mapinduzi Zanzibar)
Ndio maana nauliza kama Zanzibar ni mwanachama wa EAC na anaweza kufanya maamuzi yenye manufaa kwake hata kama yanaiumiza Tanzania Bara (formerly Tanganyika ambayo kwa sasa sio nchi)
 
Aliye iingiza Sudani Kusini kwenye jumuia alipaswa kuiingiza na Somalia. Kiujumla Sudani Kusini na Rwanda zilipaswa kutohusiswa kwenye jumuia.
 
Back
Top Bottom