Ni huyu huyu Makonda ninayemjua au macho yangu?

Hiv huyu makonda alowafanyaga nini baadhi ya watz? Mbona ni mtu ana maisha yake tu mwacheni?
Ungekua wewe ndiye makonda ungekataa kufanya aliyokua anayafanya alipokua madarakani? Mwacheni aishi kwa aman jaman mungu pekee ndo anahukumu
Kamuulize pompeo wa Marekani atakujibu aliwafanyia nini watanzania
 
Hata kama unayofuraha ya kuanguka kwake Kigamboni lkn hayo maelezo marefu uliyoandika hayana ukweli.

Kama yanaukweli ni sehemu ndogo sana. Itoshe kusema ni mchapakazi , mbunifu na asiyeogopa . Alichokumbana nacho kisiasa huwatokea wanasiasa wengi

Namuona akichomoza tena!!!
Mbona hujasema na lile alilolisema pompeo?
 
Wakuu, mwezi mmoja nyuma nilikutana na msafara Mwenge wa kufa mtu, msafara uliokuwa unaelekea Ubungo ukiwa na Magari zaidi ya mia moja yakiwa yamesheheni polisi, Magereza, Jeshi la Wananchi, Usalama wa Taifa, makada yote ya wanaCCM Dar, vigogo wote wa serikali Dar, msafara uliokuwa na mbwembwe za kila aina na ving'ora vya kuogofya.

Msafara huo uliokuwa na polisi wa lining'inia pembeni mwa milango ya Magari na brigedi ya UVCCM, ulikuwa unaelekea Ubungo kwa kupita hiii barabara ya Mlimani City, ni moja ya misafa yenye mbwembwe na ya hatarii niliyowahi shuhudia katika maisha yangu iliyokuwa na idadi kubwa ya Magari na watu walining'inia kwenye milango ya Magari ikijumuisha speed ya kukimbia na ving'ora vyenye sauti ya kuogofya.

Wakuu, leo hiii nimekutana na makonda akiwa hana mlinzi, hana ving'ora wala wasaidizi akionekana mtu wa kawaida na mwenye woga woga akiwa anatazama huku na huku kwa kupitia miwani dizani ya wale wazee wa kuangalia watu kwa kutumia kwenye upenyo wa juu ya miwani yaliyovaa wakisingizia kuwa miwani wamevaa kwaajili ya kusomea tu.

Wakuu ilibidi nifute vizuri vumbi kwenye uso Wangu ili niweze kuona kama kweli mtu huyu anaeonekana mbele yangu ni Makonda au nimepata shida ya macho niligundua kuwa ni yeye, ilinibid nipige simu kwa mmoja wa watu tuliokuwa nao siku ile ya ule msafara kuuliza kuwa hivi ule msafara ulikuwa ni wamakonda kweli? Akanihakikishia kuwa alikuwa yeye.

Wakuu, leo ndio nimegundua kuwa kweli lile somo nililofundishwa kule Msalato Secondary School kwamba dunia inazingua katika muhimili wake ni kweli.

Wakuu, tumuachie MUNGU kwa kila jambo hapa duniani yeye ndie anaejua muda siku na saa, maisha tunayoishi hapa duniani ni record ya mchezo wa mpira tulioucheza uliokuwa unatazamwa na mwenyezi MUNGU pekee na ndie anaelewa mwisho wa matokeo ya mpira uliochezwa na kila mmoja wetu, daaah!

Kupitia huyu bwana lazima watawala wajifunze kitu hapa, kuna kitu MUNGU amekionesha kupitia kwa huyu makonda ila wenye uwezo wa kuelewa wataelewa na wenye uwezo mdogo wa uelewa hawataelewa kilichotokea ila MUNGU hapa alikuwa na maaana yake, ujue MUNGU anaweza kukushusha chini kwa muda wa siku moja tu au week tu kwa nia ya kukuonesha kitu au kwa nia ya wenzio kujifunza halafu baadae akakupandisha.

Lazima tujifunze kuhusu madaraka kuwa ni dhamana maaana huyu walifika mahali wakasema kuwa anamadaraka kumzidi Waziri Mkuu pasipo kujua kuwa Waziri Mkuu hata akistaafu atalindwa maisha yake yote.
Inamaana ulikuwa hujui jina lake? Anaitwa Naibu rais so yuko zaidi ya VP
 
Oh hata tofauti ya l na r hujui! Nduki
Achana na hizo r na L, kwa nini unafikiria kuuwa tu? Usikimbilie kuuwa jiulize why huyo mtu atukanwe? Kwani ndio wa kwanza kushika madaraka Tanzania hiii?
 
Hata kama unayofuraha ya kuanguka kwake Kigamboni lkn hayo maelezo marefu uliyoandika hayana ukweli.

Kama yanaukweli ni sehemu ndogo sana. Itoshe kusema ni mchapakazi , mbunifu na asiyeogopa . Alichokumbana nacho kisiasa huwatokea wanasiasa wengi

Namuona akichomoza tena!!!
Haitakuja kutokea ukashiriki mauaji ya raia halafu ukabaki usisemwe, sio rahisi na issue Kama hiyo itakuandamaa daima katika maisha yako yoooote hadi Kwa familia na watoto wako maisha yao Yote, wewe Kama una madaraka fanya siasa za ushindani, mtu akitoa hoja jibu hoja Lakini ukianza kutumia bunduki za serikali na kuuwa watu, hiyo laaana itakuandama maisha yako yooote, hivi unaua mtu Alie na wapenzi, Ndugu Jamaaa na marafiki kisa una madaraka, hiyo kitu utafurahia maisha Kwa muda ila sio muda wote
 
Wakuu, mwezi mmoja nyuma nilikutana na msafara Mwenge wa kufa mtu, msafara uliokuwa unaelekea Ubungo ukiwa na Magari zaidi ya mia moja yakiwa yamesheheni polisi, Magereza, Jeshi la Wananchi, Usalama wa Taifa, makada yote ya wanaCCM Dar, vigogo wote wa serikali Dar, msafara uliokuwa na mbwembwe za kila aina na ving'ora vya kuogofya.

Msafara huo uliokuwa na polisi wa lining'inia pembeni mwa milango ya Magari na brigedi ya UVCCM, ulikuwa unaelekea Ubungo kwa kupita hiii barabara ya Mlimani City, ni moja ya misafa yenye mbwembwe na ya hatarii niliyowahi shuhudia katika maisha yangu iliyokuwa na idadi kubwa ya Magari na watu walining'inia kwenye milango ya Magari ikijumuisha speed ya kukimbia na ving'ora vyenye sauti ya kuogofya.

Wakuu, leo hiii nimekutana na makonda akiwa hana mlinzi, hana ving'ora wala wasaidizi akionekana mtu wa kawaida na mwenye woga woga akiwa anatazama huku na huku kwa kupitia miwani dizani ya wale wazee wa kuangalia watu kwa kutumia kwenye upenyo wa juu ya miwani yaliyovaa wakisingizia kuwa miwani wamevaa kwaajili ya kusomea tu.

Wakuu ilibidi nifute vizuri vumbi kwenye uso Wangu ili niweze kuona kama kweli mtu huyu anaeonekana mbele yangu ni Makonda au nimepata shida ya macho niligundua kuwa ni yeye, ilinibid nipige simu kwa mmoja wa watu tuliokuwa nao siku ile ya ule msafara kuuliza kuwa hivi ule msafara ulikuwa ni wamakonda kweli? Akanihakikishia kuwa alikuwa yeye.

Wakuu, leo ndio nimegundua kuwa kweli lile somo nililofundishwa kule Msalato Secondary School kwamba dunia inazingua katika muhimili wake ni kweli.

Wakuu, tumuachie MUNGU kwa kila jambo hapa duniani yeye ndie anaejua muda siku na saa, maisha tunayoishi hapa duniani ni record ya mchezo wa mpira tulioucheza uliokuwa unatazamwa na mwenyezi MUNGU pekee na ndie anaelewa mwisho wa matokeo ya mpira uliochezwa na kila mmoja wetu, daaah!

Kupitia huyu bwana lazima watawala wajifunze kitu hapa, kuna kitu MUNGU amekionesha kupitia kwa huyu makonda ila wenye uwezo wa kuelewa wataelewa na wenye uwezo mdogo wa uelewa hawataelewa kilichotokea ila MUNGU hapa alikuwa na maaana yake, ujue MUNGU anaweza kukushusha chini kwa muda wa siku moja tu au week tu kwa nia ya kukuonesha kitu au kwa nia ya wenzio kujifunza halafu baadae akakupandisha.

Lazima tujifunze kuhusu madaraka kuwa ni dhamana maaana huyu walifika mahali wakasema kuwa anamadaraka kumzidi Waziri Mkuu pasipo kujua kuwa Waziri Mkuu hata akistaafu atalindwa maisha yake yote.
Makonda hakuelewa kuwa cheo ,dhamana na madaraka ni karama za Mungu.
Yatumie vizuri na yatakuinua, yatumie vibaya yana kuangamiza.

Katika umri mdogo nilio nao nimeona mtu mkubwa zaidikuliko Makonda, tena mwenye madaraka makubwa zaidi ya kiserikali na kifedha.
Yeye huyo kiongozi aliyatumia madaraka vibaya sana, akiwafanya wake zake masekretari wake, tena bila aibu, wanawake ambao kimsingi ni wake za watu.

Alionea watu wengi sana, wengine kufukuzwa kazi kwa majungu aliyokusanya kupitia wapambe wake.
Muda si mrefu mambo yakamgeuka vibaya !
Godfather wa huyo kigogo alikuja kuuwawa katika mazingira tatanishi.
Jamaa huyo mkuu akaanza kuwindwa kama panya na vyombo vya dola.

Na Mungu alivyo wa ajabu, jamaa akapata hadi kansa iliyompeleka fasta.
Muda si muda akafariki.
SOMO:
Mungu akikupa madaraka, yatumie vyema kwa kutukuza uwezo wake.Mungu akiyaondoa, hata nzi anakudhalilisha.

Makonda ana bahati, amepewa muda wa kujutia makosa yake.
Hii stori ni ya kweli kabisa.
 
Na kama Baba Mungu kakubariki watoto... watoto wako ni ORIGINAL.. sio km wa Michael Jackson
Amenizid nini? Yani umeshikwa akili. Mimi Nina masters degree mbili yeye alifeli form four, halafu unasema kuwa ananizid kila kitu unajitambua lakini? Hiyo ni moja tu nimekupa bado vingne vingi ninavyomzid, usikariri juu ya pesa, maisha sio pesa tu wewe.
 
Labda tuwe na akiba ya maneno........na tabia ya kuhitimisha maisha ya watu.....
Kimya kingi kina mshindo......na labda yajayo yanafurahisha.......
 
tunaoumia ni sisi tuliojipa kazi ya uchawa wa kumtetetea makonda mitandaoni alipokuwa mkuu wa mkoa wa dar es salaam.

tulihakikisha tunamtetea kwa nguvu zote katika kila upuuzi na ukatili aliokuwa akiufanya kwa jamii.
 
Sababu ya yeye kutokuwa na ulinzi wa vile sahivi si inajulikana? Si kiongozi tena. Hata Magu akitoka madarakani naye ataachwa kulindwa hivyo. Vivyohivyo kwa viongozi wote waliopita. Sasa sijui kilichokukaliza kushangaa shangaa ni nini hapo. Kafanye kazi huko!
Wewe unaujua ulinzi wa raisi mstaafu ns previledge zake mpaka anaingia kaburini??
 
Back
Top Bottom