Ni hujuma au hata Petrol Station hazitoi tena risiti za kielektroniki

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
2,792
2,000
Wakuu wakati wa mwenda zake maduka yalifikia hatua za kukulazimisha kabisa kuchukua receipt ya electronic.

Baada ya Mwenda zake kuondoka maduka karibia yote yalikoma kutoa labda baadhi ya maduka tu.

Sasa nashangaa hata Petro station nazo zimeanza kuto kutoa receipt.

Hahaa kitu Mama asicho kijua watanzania kulipa kodi kwa hiari sio utamaduni wao na ni kitu kisicho wezekana.

Kama sasa tu hata receipt hazitolewi tena huo ulipaji kwa hiari utatoka wapi?
 
Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
5,923
2,000
Naunga mkono, nmenunua mafuta total ya morocco pale, nimenunua wese la 50k nikapewa risiti sasa kuicheki home nakuta ya elfu30. Na wakati inatoka nilikua naiona kwa macho
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,337
2,000
Nchi imeanza kujiendea kwa auto pilot, hata zile mbwembwe za mawaziri kuzunguka mikoani kukagua miradi hakuna tena.
 
Iringakwanza

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
731
1,000
Naunga mkono, nmenunua mafuta total ya morocco pale, nimenunua wese la 50k nikapewa risiti sasa kuicheki home nakuta ya elfu30. Na wakati inatoka nilikua naiona kwa macho
Unazani mfanyabiashara gani atakupa risiti ya bei uliyonunulia bidhaa labda atakuwa chizi
Watu wengi msichokijua wafanyabiashara wanawakwepea kodi nyinyi wateja bidhaa tunazonunua nyingi sio bei halisi ni ya chini sana
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
17,716
2,000
Bavicha wanafurahia sana hali hiyo maana wanasema hapo anakomolewa marehemu na mataga.

Na pia kitendo hicho kinarudisha hela mtaani ili wawe wanaziokota
 
Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
5,923
2,000
Unazani mfanyabiashara gani atakupa risiti ya bei uliyonunulia bidhaa labda atakuwa chizi
Watu wengi msichokijua wafanyabiashara wanawakwepea kodi nyinyi wateja bidhaa tunazonunua nyingi sio bei halisi ni ya chini sana

Enzi za magu haikwepo hii
 
Sakhalala

JF-Expert Member
May 2, 2011
556
500
Kwa kweli itabidi mama Samia ajipange upya au amtoe mtu kafara kwani watu wamepoa sana kwenye utoaji wa kodi. Ni ukweli kwamba madukani receipts hazitolewi na hata ukidai wanakushangaa na kukuzodoa. Vile vile hata TRA yaelekea wamesusa kufuatilia suala la kodi. Tunajua nia ya mama ilikuwa njema sana ila watanzania bado kulipa kodi bila shuruti kwani sasa hivi hata kwenye magroup ya Whatsap ya Wafanyabiashara wanasema kabisa kuwa sasa wamepumua kwani watu hawadai risiti tena. Ifike mahali watu waelewe kuwa kutotoa risiti ni kosa la jinai na inabidi TRA wakamate watu kadhaa na wawashughulikie kisheria ili iwe mfano kwa wengine kwani vinginevyo serikali itafikia ishindwe kulipa mishahara ya watumishi wake sembuse kutoa huduma zingine za msingi.
Vile vile ili kujenga ari ya kulipa kodi kwa hiari ni lazima serikali ikaonekana inashughulikia ubadhirifu kama ulioripotiwa kule WIzara ya Fedha hivi karibuni na wananchi wakataarifiwa tamati ya chunguzi zinazifanywa na hatua zilizochukuliwa, vinginevyo hata moyo wa kulipa kodi utashuka sana kwamba kodi inayolipwa inachezewa na baadhi ya watu na hawachukuliwi hatua. Pia ni vizuri sasa ifike mahali kila mtanzania alipe kodi bila kujali wadhifa wake. Haiingii akilini kuambiwa Mbunge na Raisi pamoja na ukubwa wa vipato vyao eti hawalipi kodi - hii inavunja moyo na kupelekea wengine kujitahidi kukwepa kulipa kodi na wengine kufanya ubadhilifu kwa hasira ya kuona wenye vipato vikubwa hawalipi kodi na hao hao wanahimiza wengine wenye vipato vidogo kulipa kodi.
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
3,923
2,000
Wakuu wakati wa mwenda zake maduka yalifikia hatua za kukulazimisha kabisa kuchukua receipt ya electronic.

Baada ya Mwenda zake kuondoka maduka karibia yote yalikoma kutoa labda baadhi ya maduka tu.

Sasa nashangaa hata Petro station nazo zimeanza kuto kutoa receipt.

Hahaa kitu Mama asicho kijua watanzania kulipa kodi kwa hiari sio utamaduni wao na ni kitu kisicho wezekana.

Kama sasa tu hata receipt hazitolewi tena huo ulipaji kwa hiari utatoka wapi?

E0NhMwdXIAAW0HL.jpeg
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,666
2,000
Mwisho wa siku itaanza kuzungusha bakuli kwa so called mabeberu ili hata mishahara ilipwe
Tunakoelekea mmh
 
Iringakwanza

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
731
1,000
Enzi za magu haikwepo hii
Nani aliyekudanganya maduka mengi tu kariakoo ukijifanya unataka risiti halisi wanakugomea kuuza bidhaa TRA walikuwa wanapika data mashirika mengi yalikuwa yanaishidwa kujiendesha mikopo ya kimya kimya ndio ilikuwa inatubust
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
59,002
2,000
Petrol station gani hiyo isiyotoa receipt...

Machine zao bila mfumo wa receipt kufanya kazi mafuta hayatoki...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom